Salaaam.
Usimwamini ndugu yako kwenye kuweka akiba. Maisha ni kuishi na ili uishi vizuri unatakiwa utimiziwe maitaji au ujitimizie mwenyewe.
Kuweka akiba ya pesa na thamani ni moja katika jitihada ya kutaka kujitimizia maitaji yako hapo badae. Katika watu wanaorudisha nyuma kufikia malengo ni ndugu,jamaa na marafiki wakishajua umejiwekea kiasi fulani iwe bank au nyumbani watakuja kukukopa tu wakijua uwezi wanyima wanalalamika na shida zao mbalimbali,ukilazimika kuwasaidia toa pesa ambayo haitakuithiri na kulalamika kwa namna yoyote.
Usimpatie ndugu kiasi chochote kwa kumwamini atakutunzia kwakuwa wewe huwezi unahofia utatumia hakika na yeye pia ataitumia akiwa na matatizo yake. Hakikisha iwe siri yako usimwambie mtu yoyote zaidi ya 1 au 2 tu unaowaanini angalau 85% na iwe kwa ajili kama itatokea dharura yakupoteza maisha au kuugua.
Ndugu ni adui hai kwenye uchumi wako ishi nao kwa makini watakuyumbisha,ni ngumu kumdai ndugu yako wakaribu kiasi chapesa kwanguvu zote utaona aibu tu na utaonekana hauna utu ata kidogo. Tuwe makini na ndugu zetu katika kukuza vipato vyetu.
Tujitaidi kunawa mikono kwa maji safi na sabuni bila kusahau kuvaa barakoa.