Dingi alikuwa anatafuta namna ya kukutoa ukajifunze maisha akili ipevuke, umekua kiumri ila kiakili bado. Kwa umri wako, hata serikali ya mitaa wakaona hauko timamu.
Acha kujenga uadui kati ya watu waliokuwa pamoja na kusaka maisha wote hadi uzeeni, hao ni marafiki. Na mama yako hata hajarogwa, kakuona mpumbavu, na labda mzee wako, kamwambia ukweli, kijana ameshakua NGOJA MAISHA YAMCHAPE APATE AKILI, USIMDEKEZE. Ndio maana unaona mama yako naye kala kimya.
Kuwa graduate kusikuzuzue, ujione wewe ndio wewe, mjini ishu ni pesa. Haijalishi umeipata kivulin au juani, hela haina Alama ya jasho. Jichanganye, piga dili lolote, jimix na watafutaji tena wa kawaida, utaingia ktk ramani tu.
Kubwa zaidi, Weka shingo yako kwa MUNGU atakufanikisha.