Ndugu wananiita mchawi wakati walilelewa na baba yangu mzazi

Nilipoona paragraph ya kuonyesha wewe ni mwanaume, nikachoka ghafla.
1. Kwa umri wako huo unamshawishi mama aombe talaka ili mkaishi wote! Unaishije na mke wa mtu?
2. Hiyo degree yako ni uchafu tu. Nenda kaichome maana haijakukomboa kabisa.
3. Hebu umshukuru baba yako kwa kukufukuza hapo nyumbani. Pengine akili yako itapata akili kidogo, maana hujielewi bado.
 
Kwa hakika kwa kutumia parameter zote nadhani hauko sawa na nadhani tatizo lako liko katika malezi. Nahisi huyo mama yako hajawahi kukupenda isipokuwa amekuwa akijipendekeza kwako ili awe mwema kwako na baba yako awe mbaya sana na hii hutokea katika familia zetu nyingi tu za kiafrika. Kwa ushauri wangu kama huna radhi za mmoja wa wazazi wako hutokuja kuishi kwa raha na kufurahia maisha hata kama utakuwa raisi wa nhi. Mimi sio mkristu lakini kuna sehemu kwenye bibilia inasema waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani. Wala hawakusema baba au mama aliyekutendea vizuri tu ndo umuheshimu au aliyekujengea ghorofa labda. Kama mzazi wako hakutimiza wajibu wake atahukumiwa na muumba na sio wewe. Ukianza kutamani mali za ndoa kugawana mwishowe utaulizwa kwanini usiolewe wewe ili udai talaka vizuri na kwa uhuru. Na hata ingetokea wazazi wako wakachana na kugawana mali na si mahari kama ulivyoandika, basi mali hizo ni za mama yako na sio zako. Wanaokuona hauko timamu nadhani wako sahihi.
 
Miaka 37 lakini kula kulala na degree mkononi!!
Si hivyo tu unakula njama utenganishe ndoa ya wazazi wako.
Mzazi akiwa na mtoto kama wewe ni hasara tu.
Maelezo yote uliyojaza hapa yanakuonyesha ulivyo na matatizo kichwani
Aliyekwambia kuwa wewe ni mchawi hajakosea, wewe ni zaidi ya mchawi
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi ni kijana wa miaka 37 kwetu tumezaliwa 2 tu, ila kuna ndugu zangu kama wanne (4) walilelewa na baba yangu mzazi katika makuzi yao, baada ya baba yangu kunifukuza nyumbani miezi 5 sasa imepita kisa tu nilimbembeleza kujiunga na chama changu cha mapinduzi, vile vile kupelekea kumfukuza na mama yangu pia ambaye alikuwa mara kwa mara uenda kudhuria vikao vya chama chetu cha mapinduzi, mimi nilimshauri mama yangu aende mahakaani kudai taraka ili waachane na baba wagawane mahari ili mimi na mama tukatafute sehemu yetu tukae tuepukane na manyanyaso ya baba

Mama baada ya kuondoka kwa baba alikuwa akikaa kwa dada yake ambaye anaishi maeneo ya Kijichi, sasa siku ya Jumamosi mama alinipigia simu kuwa anaenda kwa baba kudai taraka, baba akikataa kumpa taraka moja kwa moja anaenda mahakamani, siku ya Jumapili mama alienda moja kwa moja nyumbani kwa baba kudai taraka, ila kilichotokea ni kuwa mama tangu aende kwa baba pale nyumbani hajanijulisha chochote kile na nilikuwa nikipiga simu hapokei, jana jioni ndio aliniambia kuwa basi ameghailisha mambo ya taraka, ndugu zangu niliishiwa nguvu sana maana mama huwa ananisikiliza sana kwa kila kitu, nikahisi ndugu zangu watakuwa wanamchezea kiuchawi

Kumbukeni ndugu zangu sina kazi wala kibarua nahishi kwa marafiki tu, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yeyote yale nina degree ya marketing nimesoma pale UDSM-UDBS, nilitegemea hiyo hela ya mama akigawana mali na baba baada ya kupewa taraka na mimi nipate mtaji, nimeumia sana ndugu zangu, mpaka kupelekea ndugu wa upande wa baba kuniita mimi mchawi

Naombeni mwenye kazi yeyote anisaidie ndugu zangu napitia hali ngumu sana kimaisha na baba hanitaki kabisa kwake kisa tu nipo chama cha mapinduzi na alinitimua wakati mimi ni mtoto wa pekee wa kiume kwake, nilishamshtaki ofisi za kata ila kata wakasema mimi sina akili timamu, na najua baba aliwapa pesa wale viongozi wa ofisi ya kata ili kunikomoa na kuto kunisikiliza malalamiko yangu

Kwa sasa nipo Dar es Salaam Boko. Mwenye connection anisaidie
Kwa haya maelezo uliyotoa huwezi pata connection hata kidogo , mbona unaonekana Kama huna akili vizuri tu
 
Wewe kweli mchawi😂😂😂😂😂 yaani unataka mama yako na baba yako waachane ili wagawane mali halafu mama yako akupe mtaji!!!!???
Seriously??
 
Sasa kwanini uhami hicho chama umekua mzee? Yaani hata baba ako anakuzidi fikra na degree yako. Yaani unang'ang'ana na Lichama limetuongoza miaka nenda rudi na hapo ulipo hata ajira huna eti wewe ni mwanachama wa ccm nenda kwa mwenyekiti wa ccm akupe ajira maana yeye ndio anaongoza nchi.
Hawezi pewa kazi huyu
 
Naungana na viongozi wa kata kwamba huna akili timamu
Kuna uzi umeleta juzijuzi ukisema una milioni sijui kumi unataka kujenga, nilikuzuzua pale kwa uongo wako leo hii umekuja tena kutuonyesha ulivyo chizi kichwani
 
Izi degree za udsm wawe wanawapima ata mkojo watu wa kuwapa.we jamaa ata ushauri siwezi kukupa ntaonekana akili kama zako
 
Back
Top Bottom