MR KUO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,678
- 3,818
Ndugu wadau
Poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa.
Naomba niende moja kwa moja kwenye shida yangu, tarehe 24/2/2020 Kama familia tulipata msiba wa kuondokewa na MZEE wetu aliyetangulia mbele za haki kwa kifo Cha ghalfa.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu kuomba msaada wa ushauri ni kwamba, enzi za mzee alifanikiwa kuwa na watoto nane na wote wa tumbo moja kwa maana ya mama mmoja, huku akiwa na mali ambazo ni nyumba nne, tatu akiwa kaandika majina yake kamili huku nyingine moja akaandika hati ya jina langu kwa sababu Mimi ndo mzaliwa wa mwisho.
Baada ya mzee kufariki na hakuacha wosia wowote maana ilikuwa ghafla ndo wameibuka kaka zangu wakubwa wawili wanataka nyumba yenye hati yangu iuzwe pesa igawanywe pasu kwa pasu ili waweze kufanya Mambo mengine ikiwemo kumalizia ujenzi wa nyumba zao ambao umesimama. nimejaribu kumuuliza mama ili nijue hii imekaaje kaishia kunipa majibu ya kawaida Sana kwamba (yeye hana mamlaka na mali alizoacha mzee maana ni zenu watoto mkiamua kuuza mali yoyote ni sawa).
Wakuu kilichonileta hapa ni kutaka kujua hii imekaaje kwa mujibu wa sheria ili nijue mapema isije ikawa shida huko siku za mbele kutuhumiana dhuluma au kujaribu kuvuruga mahusiano ya familia kwa Jambo la kawaida.
.....................
Kwamba nyumba ina hati ya jina langu..
Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye hati ya jina langu badala ya hizi nyingine zenye majina ya baba.
"Mama anasema hana mamlaka na mali alizoacha mzee maana ni za watoto, wakiamua kuuza sawa wakiamua kuacha sawa".
Hapa naona kama kakwepa kujibu swali langu la msingi nililotaka kujua kama kuandikwa kwenye hati ya nyumba ina maana nyumba ni yangu ama sio yangu.
Shukrani