Hapo kuna maswali ya kujiuliza
1. Japo marehemu baba anajua ana watoto 8 na ana nyumba 4, kwanini aliamua kukupa wewe nyumba yako kwa kuandikisha Hati ya nyumba yenye jina lako? Hili swali mama anaweza kulijibu, wazee wa karibu na mzee wanaweza kulijibu, kaka/dada wa mzee wanaweza kulijibu, babu na bibi zako wanaweza kulijibu, hata na wewe kutokana na mazingira mliyoishi hapo nyumbani unaweza kulijibu
Kwa uelewa wangu kuna Mila za baadhi ya makabila (kama watu wa kaskazini) , mtoto wa mwisho ndiye anayeachiwa mji wa mzee. Hivyo kama baba ameamua kukuachia nyumba kwa jina lako ina maana hapo ni NYUMBANI, sasa nyumbani hapawezi wala hapatakiwi kuuzwa...