Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Nyumba yako hiyo, kwa hali ilivyo sasa hivi sikushauri uiuze kabisa utajuta. Labda kama ipo vijijini huko ila kama ni mjini usijefanya hilo kosa, hela wagawane kwa sababu ipi? Nyumba yako alafu uuze ugawe pesa? Waende wale bata hela za bure ubaki huna nyumba wala huna kitu. Don’t make that mistake kabisa
 
We jamaa bana, yani mama akae na hao watoto 8 Kwenye nyumba moja , wewe leo unauliza watoto 8 watamtunzia wapi mama mmoja wakati nyumba zipo 4, na kuna wengine wanamalizoa ujenzi kwa maelezo ya dogo, zinaweza kua hata zaid ya nyumba 7, zooote hizo mkose pa kumtunzia mama ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu raha yamama mtunzie kwenye nyumba yake sio yeye aje akae kwako labda kiwe nikikongwe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zako zinahesabika kwa stori hii.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hapo ninacho kielewa ni kua kwanza hiyo nyumba sio urithi kutoka kwa baba yako hiyo nyumba alikupa wakati yupo hai usiuze hiyo nyumba ni Mali yako pili wakati wa mgawanyo wa Mali zingine ambazo ndio urithi wenu mnatakiwa kugawana nao pasu kwa pasu huo ndio urithi wenu

Maana ya ww Mze kukupa nyumban inaonekana hao ndugu zako wametumia vingi vya mzee kwa miaka mingi na ww hiyo nyumba ndio zawadi yako pambana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi kwa manung'uniko yako maana kiuhalisia ilibidi iwe nyumba yako, lakini nakushauri tumia busara sana kama unapenda familia yeni iwe na mustakabali mzuri huko mbeleni. Ninaimani hizo nyumba 3 pia zimeuzwa na kwenye mgao ulipata mgawanyo sawa na wenzio, kama ni hivyo kuepusha shari nakushauri kubali tu iuzwe na mgawane ili maisha yaendelee vizuri, Hakuna ugomvi mbaya kama ugomvi wa ndugu hasa katika kugombea mali.

Fumba macho muombe Mungu awasimamie hili lipite salama na maisha yaendelee kama kawaida. Riziki ipo kwa Mungu na kama ipo ipo tu mwanadamu ataichelewesha tu
 
Mkuu inabidi ufunguke zaidi tukupe ushauri wa kibusara.
Kwa mfano kwa sasa unaishi kwenye hiyo nyumba inayotaka kuuzwa? Na kingine je ikianza vita ya kuburuzana mahakamani umejipangaje?maisha yako kiujumla yapoje kama ni mtu wa kuhangaika kuitafuta hela ya kula tu kesi ni ishu nyingine.

Kwa kifupi hiyo nyumba ni ya kwako kwa upande wa kisheria. Ila kwenye mambo hayo watu huwa hawakubali kirahisi hata kama utashinda mahakamani watakutafuta kwa njia zingine tofauti hadi wakupate wakukomoe.

Nilishawahi kushuhudia watu wakiuliwa kwa vifo vya utata kwa sababu ya ugomvi wa mali ya urithi. Nishawahi kushuhudia mtoto na baba yake mzazi wanagombana ugomvi wa kufa mtu na kubebana na madifenda ya polisi kwa sababu ya mali ya urithi kisa ilitokea babu alifariki na katika mali zake aliandika jina la mjukuu,baba mtu akawa hataki kusikia hiyo habari,basi palichimbika bila jembe mwisho wa siku mjukuu alishinda kesi kwa mtiti sana.

Na huyo mjukuu naye alikuwa mbabe na bangi mtu halafu yupo kijeshi. Mwisho wa yote ita wazee wenu wenye busara mkae kikao na mkubaliane utaratibu wa mauzo na mgawanyo utakuwaje,na je nyumba ngapi ziuzwe?na kila mtoto atanufaika vipi?

Hiyo ndio suluhisho usiwe mgumu sana watakuua. Unaambiwa katika hii dunia ili uishi kwa amani unatakiwa kubalance maisha uwe katikati vinginevyo ukiwa mgumu sana watu watakuvunja na ukiwa mlaini sana watu watakuminya, kwa hiyo usiwe mgumu sana na wala usiwe mlaini sana.
nashukuru Sana kwa mwongozo. Kama nilivyotangulia kusema kuwa mzee alikufa ghafla.

kuhusu Mali nyingine ninazojua nje ya nyumba hizo nne Ni pikipiki Moja na bajaji Moja tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAENI KIKAO CHA FAMILIA NA CHAGUENI MSIMAMIZI WA MIRATHI PELEKENI MUHTASARI MAHAKAMANI,AKISHATEULIWA MSIMAMIZI AFANYE KAZI YA KUGAWA MALI.VINGINEVYO HALIA ITAKUWA MBAYA SIKU ZA USONI.
 
naona Mambo Yanazidi kuwa makubwa.

nikikomaa Mambo yatakuwa meeeengi Sana,

nikipotezea nakuwa nimejidhurumu mwenyewe na nitaumizwa na hii hali vibaya mno,...
Hivi nikuulize wewe na ndugu zako wote ni wa mama mmoja au wengine ni wa nje?

sasa kisheria iko hivi baba akifa watoto hawaruhusiwi kuuza nyumba hadi na mama naye afe.

Sema tu mama yako anawaonea aibu hao kaka zako ila akiwakazia hakuna nyumba itauzwa.
Nilishawahi kuona mfano wa kesi kama hiyo baba alikufa watoto wakaanzisha vurugu kwa mama yao ili nyumba iuzwe walivyopelekwa mahakamani walichemka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Su mkubaliane muuze hizo zingine tatu ili hiyo yenye jina lako aishi mama yenu?

Labda pia hiyo yenye hati yako ni ya thamani zaidi kuliko .pengine hizo zingine ni mabanda

kumbuka pia unapigana vita na ndugu zako na wewe uko pekee yako.
 
Tafuta chako ndugu usitake uhasama na ndugu zako uza nyumba kajenge ya kwako,ww hapo hujachangia hata msumari wa bati shida iko wapi? Watu 8 kwanini ww upate nyumba peke yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyempa ndiye alitakiwa aulizwe ameona nini ambacho wewe hukujui kama Baba
 
Family comes first,busara tu ingetumika.
 
unanifokea bure chief MZEE ndo aliandika mmiliki wa hii nyumba inayogombaniwa Ni mimi, Sasa ndo hivyo akatangulia mbele za haki bila kuliweka wazi kwa watu wote Ila nyaraka ndo inaonyesha. hapa najaribu kuangalia Sheria na taratibu zinasemaje ili nijue Kama Ni kukubari iuzwe tupate hela wote ama Hawa wanataka kuniibia kijanja.
Tafuta chako ndugu usitake uhasama na ndugu zako uza nyumba kajenge ya kwako,ww hapo hujachangia hata msumari wa bati shida iko wapi? Watu 8 kwanini ww upate nyumba peke yako

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada na wengine, someni hicho kitabu na myafuate hayo yalioelekezwa na wabobezi wa sheria. Utakuja kunishukuru baadae. Pia inabidi mfuate kanuni za mirathi (kwa mtoa mada) na wengine tuliobaki tuandike wosia kuepuka migogoro
 

Attachments

Back
Top Bottom