Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Dah nashukuru Mungu sijawahi kuiwazia nyumba yetu japo mie ndo last born na kwa mila zetu mtoto wa mwisho ndie mrithi wa mjengo.

Kwa sasa mshua anauboresha mjengo kila uchao nawaza tu zogo lake kati ya first borne brother na mama wa kambo litakuwaje japo sidhani kama ntashiriki kugombania. Nataka nijenge kwangu tu ili ile nyumba niipangishe huko mbeleni.

Bro mbona kama umemuwazia mzee ndio ataanza [emoji23]. Ukianza wewe hizo vurugu
Anyway better ku fight kupata chako maana cha urithi kinaweza kuja na maamuzi yoyote.

Alexander
 
Bro mbona kama umemuwazia mzee ndio ataanza [emoji23]. Ukianza wewe hizo vurugu
Anyway better ku fight kupata chako maana cha urithi kinaweza kuja na maamuzi yoyote.

Alexander
Hahahah tatizo kurogana ndio sitaweza mkuu maana bi. mkubwa mtu wa michezo.
 
Hapna nimeulzia maana naona una mipango ya kuipangsha mzee akifa kama vile umeahidiana na Maulana kuwa lazima atatangulia mzee kabla yako
Hahahah we jamaa bana hatuombei ila mambo hutokea naturally! Huenda nikapigwa hata na Scania nikarudisha namba. Maisha ni fumbo.
 
Hahahah we jamaa bana hatuombei ila mambo hutokea naturally! Huenda nikapigwa hata na Scania nikarudisha namba. Maisha ni fumbo.
Kama umeoajua mkeo anawaza kuwa utatangulia ipo siku atakwambia hivi ukifa utaniachaje na watoto
 
Kataa Mr kuo.ndiomaana baba aliandika jina lako kataa ukikataa wewe wote hawawez kuuza labda kama kunashida kubwa ikiwa kilammoja anataka iuzwe afu hela zikae mifkon mwake kataa
 
Mzee wako inaonekana alikupa kipaumbele sana kuliko wenzako as a last born, na inaonekana ulibweteka na hilo kiasi cha kuona wewe ni bora kuliko wenzako.

Naona una option mbili, moja ni ya wewe kwenda upande wa sheria kwa kuwa una hati sheria itakubeba na utashinda ila itakuacha na uhasama uliopindukia na hao ndugu zako

Option ya pili ni kukubali yaishe mgawane pasu na hao kaka zako , hii ipo kibusara zaidi na hakuna risk zaidi ya wewe kuanza maisha upya

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nyumba zote zikiuzwa.. yeye na mama yake wataishi wapi?

Hapana wasiuze zote wauze hiyo moja au hata tatu ila wahikikishe mama anabaki na nyumba moja, hakuna kitu sikipendi kama maugomvi ya urithi mwemye nacho hayupo ambao wapo wanagombani uatfikiri hwawezi tafuta chao
 
Poleni kwa msiba,

Haya mambo ya urithi na mirathi hasa kwa jamii zetu hizi n pasua kichwa sana...
Kuna jamaa yangu ameyaacha shamba la miti na vitunguu huko iringa akaniambia Zege la Nyasi kama ningechukua kitu kule ndugu wangeniua, nimewaachia kiroho safi mimi napambana mjini tu.

Hao ndugu watano wao wapo upande upi? Maana hapo wametoa sababu ya kihuni yakuwa uuze halafu wakamalizie majengo yao halafu wewe ubaki mweupe.

Nafikiri Ukiwakataa utanunua ugomvi ambao utawagawanya vipande ambapo si ajabu watakao kuunga mkono nao watataka faida kutoka kwako ambayo naona utaenda kuuza nyumba ili ugawane nao tena.

Hii ngoma naiona imekaa kimtego sana...

"Panapo fuka moshi , punde moto utawaka"
 
Mama yako ndio mbaya! Yeye ndio mkata mzizi wa fitna, neno lake ndio mwanangaza kwenu, kitendo cha kukaa kimya anamaanisha nini!?

Je hizo nyumba 3 walizouza ulichukua mgao? Km ulichukua mgao huna budi na hii mpige bei mwende pasu kwa pasu.

Ila hapo mbaya ni mama yenu, ugomvi wa mali ni kitu kibaya mnoo.
 
hapana mkuu nyumba hazijauzwa maana mzee kafariki juzi juzi tu.nimesema nyumba zote nne Moja Ina hati ya jina langu nyingine hati zote Zina majina ya mzee, Sasa Hawa wakubwa wanataka hii yenye hati la jina langu tuiuze zile nyingine zibaki hapo ndo nashindwa kuwaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuwa muungwana gawan na wenzio sawa, unaonekana unatamani hiyo nyumba ubaki nayo peke yako
subili kwanza. sionkiwa sikatai Bali nashangaa mawazo Yao yaani Moja kwa moja wameona hii iliyoandikwa jina lango ndo ya kuuza?

wangeanza kupendekeza ziuzwe nyingine halafu wafike kwenye hii kidogo ningewaelewa Sasa wameanzia kwangu halafu mwingine hawajagusa kabisa kwa Nini nisione na kufikiri Hawa Wana mawazo mengine Hawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapana mkuu nyumba hazijauzwa maana mzee kafariki juzi juzi tu.nimesema nyumba zote nne Moja Ina hati ya jina langu nyingine hati zote Zina majina ya mzee, Sasa Hawa wakubwa wanataka hii yenye hati la jina langu tuiuze zile nyingine zibaki hapo ndo nashindwa kuwaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu zako washenzi, iweje iuzwe yenye jina lako, halafu nyingine zitulie, wasilete ukhanithi.

Lakini mie naendelea kusimama pale pale, mbaya ni mama yenu, kitendo cha kukaa kimya si kizuri hata kidogo.
 
+1
Mama yao ndio tatizo, mkuu hawa watoto vitinda mimba huwa wanapewaga privileges zisizo na vichwa Wala miguu na huwa wanadharau sana wakubwa zao.

Hiyo ya kuuza nyumba ya dogo ni revenge tu baada ya kuteseka na makucha ya aliyekuwa baba yao na pengine hata hawana mpango na nyumba zingine
Sent
 
unanifokea bure chief MZEE ndo aliandika mmiliki wa hii nyumba inayogombaniwa Ni mimi, Sasa ndo hivyo akatangulia mbele za haki bila kuliweka wazi kwa watu wote Ila nyaraka ndo inaonyesha. hapa najaribu kuangalia Sheria na taratibu zinasemaje ili nijue Kama Ni kukubari iuzwe tupate hela wote ama Hawa wanataka kuniibia kijanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu uswahilini hakuna sheria,kuna jamaa kinondoni alikua kama ww,mtoto wa mwisho na alikua South Africa,ndugu zake wakataka kuuza nyumba yao akawake ngumu akarudi ni kichaa mpaka leo yupo pale mkwajuni unaweza kujifunza kwake,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom