Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Kama mama yako ameshindwa kutoa maamuzi kwenye huo mgogoro, jaribu kushirikisha wazee, ikishindikana kabisa..kubaliana na ndugu zako. Mali zinatafutwa lakini uhai ukipotea umepotea.
 
Mara nyingi baadhi ya makabila, baba akifariki, mtoto wa kwanza ndiye mmiliki
Wewe utakuwa mtu wa kanda ya ziwa, uchaggani mtoto mdogo wa kiume ndiyo mrithi au mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi baba hadi siku ya mwisho.

Sheria za mirathi za serikali hazifuati hiyo taratibu au mila ya kanda ya ziwa au ya uchaggani.

Hapo kwa kesi ya huyu mdau aisikilize nafsi yake na jinsi anavyo taka kuishi na nduguze lakini kimsingi hiyo nyumba ni ya kwake.

Marehemu baba yao alifanya makusudi kuandika jina la mtoto wa mwisho kwa kuamini anaweza kufa wakati bado huyu mdogo hajajiimarisha kiuchumi anahitaji kitu cha kumsaidia apate elimu , mtaji na mengineyo hadi atakapo simama kiuchumi mwenyewe.

Akikubali kuuza hiyo nyumba, wakauza na zingine zote, na kama yeye bado hana hata kiwanja au nyumba kama nduguze wakubwa basi laana ya baba yao itamuandama yeye, nduguze na mama yao kwa kutoheshimu nia yake (marehemu) juu ya kumtunza mleta mada hadi asimame kiuchumi.
 
Kifupi hiyo nyumba ni yako, usikubali kuuza hadi nawe uwe na nyumba yako kisha hapo ukubali kuuza na ugawane sawa na nduguzo.

Kwa kuwatoa hofu nduguzo wasione wewe ni mbinafsi basi muandikiane mkataba wa kisheria hiyo nyumba ukifa leo watoto wako hawatakuwa wamiliki pekee wa hiyo nyumba bali itakuwa nyumba yao pamoja na nduguzo watakao kuwa hai au kwa waliokufa watoto wao wana haki ya wazazi wao.
 
Ndugu wadau

Poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa...
Pole mkuu, Marehemu baba yako hakuwa mjinga kuandikisha jina lako kwenye hati ya nyumba, simamia hilo na usiyumbishwe!

Atakayetumia nguvu kubwa kujaribu kubatilisha maamuzi aliyofanya mzee basi wewe usishiriki katika hilo, waache wafanye wenyewe. HAKI yako haitapotea kamwe, kama kuna LAANA itawahusu wao wenyewe
 
Pole mkuu, Marehemu baba yako hakuwa mjinga kuandikisha jina lako kwenye hati ya nyumba, simamia hilo na usiyumbishwe!

Atakayetumia nguvu kubwa kujaribu kubatilisha maamuzi aliyofanya mzee basi wewe usishiriki katika hilo, waache wafanye wenyewe. HAKI yako haitapotea kamwe, kama kuna LAANA itawahusu wao wenyewe
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi hiyo nyumba ni mali yako.

Mwenye mali hutambuliwa kupitia hati halali yenye kubeba jina la mwenye mali husika.

Baba hakuandika jina lako kwa bahati mbaya, bali alidhamiria (fikiria tena hili).

Naamini, kwa sababu nyumba iko katika jina lako, basi hakuna anayeweza kuuza isipokuwa wewe mwenyewe au kwa ridhaa yako.

Aisiye na umiliki wa mali hawezi kuiuza mali hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Mahakamani upate haki yako hiyo ni nyumba yako na hakuna wa kuigusa mzee wenu alikuachia wewe usikubali nenda kashitaki mahakano
 
Yaani wanafikiria kuuza wakati mzee kafa kaziacha?? Kwenye suala la mali ndo huwa unakuja kushangaa kwamba hivi huyu ni ndo yule kaka yetu au Dada yetu tuliyependana mzee akiwa hai?? Watu hubadilika utu hupotea na kuwa wanyama ,kwanza hapo mtarogana mtatupiana vipqnde vya majini,kwa ushauri wangu kama unajiweza kimaisha kidogo kubali muuze ili mjinasue laasivyo mtakufa mkome
 
Hapo anapoishi saiv ni wapi?hawezi kuendelea kuishi hapo hapo ? watoto hawawez mjengea yake ?

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa majibu yako yanaonesha either 1. Unaelewa ila ni mtu wa roho ya dhuluma kama mabro wa mtoa mada, 2. Au huna uelewa wa mambo yanatakiwa yaweje kikawaida, 3. Au huna uzoefu na tabia za ndugu kwenye mambo haya ya mirathi.

Hapo Jamaa hatakiwi kuwaamin hao Mabro, yaan nyumba ikiuzwa kila mtu akachukua chake mama anaweza akaanza kusumbuliwa tu, kila mtu anamrushia mpira mwenzie amtunze, Halaf vijana wenyew inaonekana bado hawana maisha na ustaarabu kivile hivyo hapo Bi mkubwa cha kujihakikishia uhakika wa maisha inabidi asimamie nyumba zisiuzwe basi.

Ila mambo yako ya "aah si atatunzwa tu na wanae..." Ni mawazo rahisi sana na wengi wanaotoa mapendekezo hayo ni vigeugeu au hawajielewi. Nisamehe ila na wasiwasi na watu kama wewe.
 
Asante Sana Sasa wanaibuka Hawa mabro wanataka iuzwe tugawane hela. mama nae Kama hajui kitu ndo nabaki njiapanda mzima mzima.
Mama yako lazima asifungamane na yeyote ili kuepuka kutengwa na wanae ,,,ila funguwa kesi ya mirathi fasta,,,halafu huko mahakamani ndy utapata haki yako. usiogope mkuu.
 
Mama yako lazima asifungamane na yeyote ili kuepuka kutengwa na wanae ,,,ila funguwa kesi ya mirathi fasta,,,halafu huko mahakamani ndy utapata haki yako. usiogope mkuu.
Unakwenda mahakamani kutafuta nini wakati wewe ndio mmiliki na una hati miliki?
 
Ndugu wadau

Poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa.

Naomba niende moja kwa moja kwenye shida yangu, tarehe 24/2/2020 Kama familia tulipata msiba wa kuondokewa na MZEE wetu aliyetangulia mbele za haki kwa kifo Cha ghalfa.

Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu kuomba msaada wa ushauri ni kwamba, enzi za mzee alifanikiwa kuwa na watoto nane na wote wa tumbo moja kwa maana ya mama mmoja, huku akiwa na mali ambazo ni nyumba nne, tatu akiwa kaandika majina yake kamili huku nyingine moja akaandika hati ya jina langu kwa sababu Mimi ndo mzaliwa wa mwisho.

Baada ya mzee kufariki na hakuacha wosia wowote maana ilikuwa ghafla ndo wameibuka kaka zangu wakubwa wawili wanataka nyumba yenye hati yangu iuzwe pesa igawanywe pasu kwa pasu ili waweze kufanya Mambo mengine ikiwemo kumalizia ujenzi wa nyumba zao ambao umesimama. nimejaribu kumuuliza mama ili nijue hii imekaaje kaishia kunipa majibu ya kawaida Sana kwamba (yeye hana mamlaka na mali alizoacha mzee maana ni zenu watoto mkiamua kuuza mali yoyote ni sawa).

Wakuu kilichonileta hapa ni kutaka kujua hii imekaaje kwa mujibu wa sheria ili nijue mapema isije ikawa shida huko siku za mbele kutuhumiana dhuluma au kujaribu kuvuruga mahusiano ya familia kwa Jambo la kawaida.
.....................

Kwamba nyumba ina hati ya jina langu..

Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye hati ya jina langu badala ya hizi nyingine zenye majina ya baba.

"Mama anasema hana mamlaka na mali alizoacha mzee maana ni za watoto, wakiamua kuuza sawa wakiamua kuacha sawa".

Hapa naona kama kakwepa kujibu swali langu la msingi nililotaka kujua kama kuandikwa kwenye hati ya nyumba ina maana nyumba ni yangu ama sio yangu.


Shukrani
Nyumba sio yako Bali Ina jina lako. Hyo ni ya familia na ndio maana baba yako hakukwambia kua amekupa nyumba. We unaonekana una tamaa. Iuzwe mgawane na wenzako mkuu
 
Nyumba sio yako Bali Ina jina lako. Hyo ni ya familia na ndio maana baba yako hakukwambia kua amekupa nyumba. We unaonekana una tamaa. Iuzwe mgawane na wenzako mkuu
Hivi una akili timamu? Unaelewa maana ya tittle deed?

Au hicho kichwa unafugia nywele tu?
 
Nyumba sio yako Bali Ina jina lako. Hyo ni ya familia na ndio maana baba yako hakukwambia kua amekupa nyumba. We unaonekana una tamaa. Iuzwe mgawane na wenzako mkuu
Ajue nina tamaa halafu aniandike???[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Hapo kuna maswali ya kujiuliza

1. Japo marehemu baba anajua ana watoto 8 na ana nyumba 4, kwanini aliamua kukupa wewe nyumba yako kwa kuandikisha Hati ya nyumba yenye jina lako? Hili swali mama anaweza kulijibu, wazee wa karibu na mzee wanaweza kulijibu, kaka/dada wa mzee wanaweza kulijibu, babu na bibi zako wanaweza kulijibu, hata na wewe kutokana na mazingira mliyoishi hapo nyumbani unaweza kulijibu

Kwa uelewa wangu kuna Mila za baadhi ya makabila (kama watu wa kaskazini) , mtoto wa mwisho ndiye anayeachiwa mji wa mzee. Hivyo kama baba ameamua kukuachia nyumba kwa jina lako ina maana hapo ni NYUMBANI, sasa nyumbani hapawezi wala hapatakiwi kuuzwa.

2. Je baba alikuwa anamiliki nyumba tu, je mgawanyo wa mali zake nyingine upoje, je hao watoto wengine hawajapata zaidi mgawo wa mali nyingine ukilinganisha na wewe? Inawezekana kuna viwanja, mashamba n.k. yana Hati zenye majina ya ndugu zako

Usikurupuke kukubali kuuza kabla hujapata majibu ya maswali hayo
Ushauri wako mzuri ila asiwe king"ang"anizi sana aisee isije kumletea shida maana hata mama nae yuko njia panda, kama vipi waweke mali zote mezani wagawane pasu kwa pasu ili Amani iwepo kwenye familia.
 
Nyumba yako hiyo, kwa hali ilivyo sasa hivi sikushauri uiuze kabisa utajuta. Labda kama ipo vijijini huko ila kama ni mjini usijefanya hilo kosa, hela wagawane kwa sababu ipi? Nyumba yako alafu uuze ugawe pesa? Waende wale bata hela za bure ubaki huna nyumba wala huna kitu. Don’t make that mistake kabisa
Daaah Mr Graph ujue unaweza kumtia kwenye shida kijana wa watu? kama hao ndg zake njaa njaa itakuwa hatari sana aisee bora kuuza tu hiyo nyumba wagawane pasu pasu!!!!
 
Back
Top Bottom