Ndugu wanataka tuuze nyumba yenye Hati ya jina langu baada ya mzee kufariki

Mkuu kwanza jua nyumba ni yako personal uliyopewa na baba yako. Hivyo hakuna sheria ya kuhiusisha na familia .Hao ndugu zako wanalijua hilo ndio maana wanataka iuzwe ili mbaki na hizo tatu zenye ufamilia ndipo mtakuwa sawa.

Maoni yangu kwako, kwanza ondoa tamaa ya mali ya urithi, mchukue mama yako alafu waambie ndugu zako wagawane hizo nyumba na mali zote zilizobaki na wewe usihitaji chochote zaidi ya hiyo nyumba uliyoanfikishwa.
 
Hiyo nyumba tayari ulikuwa umeipewa na mzee wako hata kabla ya kufariki kwake.Hao ndugu hawastahili kupata chochote kutoka kwenye hiyo nyumba.
 
Kama hati unayo mkononi we nenda mahakamani waje hapo wapige stop hakuna kuuzwa kitu.

Kuna familia zina matatizo sana yaani wanapenda kuuza vitu mwenye navyo akisepa

Nashukuru kwetu tuko wachache na tunaelewana sana makubaliano yetu kuboresha maeneo yote ya wazee maana yako marketable places na
 
kiufup ndugu si kila jambo.linatatuliwa kisheria saa nyingine unanafasi ya kutatua kifamilia nyumba hio mzee wako alipatia jasho kwaajili ya kunufaisha watoto wake wote kwaiyo kuandikwa jina lako kuna weza kuwa faida kwako nakuwanyima haki wengine lakini kizazi chako wewe kitapata tabu.ukiondoka duniani ndugu yangu tumia busara kwenye hili
 
Kisheria unaweza ukawashinda ndugu zako Ila upande wa pili wa shilingi inabidi uwe fiti sana la sivyo watakutanguliza ana uwe ndondocha wakulee wenyewe. Kuwa makini
Achaa kumtisha mwenzio, kama nyumba ziko nne,kwa nini nyumba ilioandikwa kwa jina la dogo ndiyo iiuzwe kwanza!? Hao ndg wana tamaa na wakae kwa kutulia, sheria itachukua mkondo wake,ni swala la muda tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…