Maji yapo shingoni, nimeamini watawala wengi mawazo yao ni kabla ya mapinduzi ya teknolojia, walifikiri kuzima internet basi ukatili wao waliokuwa wanaufanya miaka hyo ya zamani yatabaki gizani…mambo yamegeuka, vitu hadharani, sasa hofu zimewajaa, wanapata pressure kutoka kwa wananchi wao na mataifa ya nje, mbaya zaidi baadhi ya waliopo kwenye vyombo vya dola, wameshatoa hadi coordinates ya sehemu walipofukia miili ya watu.
Mpasuko kwenye vyombo vya usalama na ulinzi ni mkubwa, kwa wananchi ndo hapafai kabisa, hii ni hatari sio kwa uyu mama tu bali kwa genge lote la CCM, wanatafuta kila njia ya kurudisha vitu kwenye hali yake, ila haiwezekani sababu wahusika wameanikwa kwenye public, yaani serikali yote imeoza, namba 1 anatakiwa kuondolewa.