Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Katika wote niliosoma mawazo yao walau wewe umetoa ushauri kwa experience wengine hawajawahi hata fanya biashara wanatoa ushauri fake, wengine wanafanya biashara na wanajua nini cha kufanya ila wamempuuza huyu jamaa.
Ngoja niendelee kusoma maoni.
 
Hilo la lodge uko sahihi unakula hela mpaka unazeeka ipo tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Chukua hizo mil200, acha kazi.

Fanya biashara za mazao, kuuza vifaa vya magari,kuuza vifaa vya ujenzi.
Wekeza nusu tu ya hiyo pesa,nyingine hifadhi sehem iliyo salama zaid
 
Hapo ndipo tunapokuja kuona kuwa elimu haijakusaidia kabisa katika ukombozi wako wa fikra.
Mfumo wetu wa elimu ni mizaha mitupu ayseee.
Hivi wabongo mnahitaji bilioni ngapi mjue mmetoboa ayseee?
Hivi 200M kisa kuacha kazi ndo ya kuandikia na post hapa JF kweli muraa??
Mbona hilo swala haliitaji hata kufikiria hata sekunde moja muraa!!?
Upewe nini sasa muraa ujue umetoboa ayseee ??
Ulisoma ili iweje sasa kama suala dogo namna hii kulipatia ufumbuzi wewe mwenyewe tu linakushinda?
Wewe ni wakukuzaba na makofi muraa akili ikukae sawa?
Mabaharia kitaa wanasaka 10M tu waache utumwa wa ajira eti wewe unaulizia kuhusu 200M ayseee??

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Nimegundua kumbe tatizo la Watz ni mawazo si mtaji... Tumeshindwa kumshauri mtu namna ya kuwekeza milioni 200?

Ndugu yangu hakuna mkate mgumu mbele ya chai... Mambo yako mengi ya kufanya inategemea wewe una interest na eneo gani ..

Cha kwanza baada ya kuona interest yao, tafuta biashara zilizopo mjini na uangalie wapi ambao panalega lega..

Pita kwa benki yao, waulize wametoa mikopo kwenye maeneo gani na kwa nini ???

Biashara zipo nyingi na zinayumba yumba .... Mimi kwa mtazamo wangu...Ikiwa kwenye biashara ya vilainishi.... Tafuta makampuni makubwa kama TOTAL ENERGIES, ORYX , BP , ENGINE na mengineyo , omba kuwa wakala wao wa bidhaa za vilainishi....

Vilevile usisahau kuwa na mtu mzoefu kwenye eneo hilo...... Lakini uwe na wewe mwenyewe uwe na uwezo wa kusoma mchezo au eneo hilo la biashara ...

Maeneo ya uwakala wa bidhaa mbalimbali na kuzisambaza yanafaaa.. Uwakala na usambazaji wa bidhaa za maduka, ukinunua akina Mo, AZANIA, Bahkressa ... Bidhaa mbalimbali ikiwemo maji, vyakula nk.....

Maeneo ni mengi usicheze mbali na uwakala wa bidhaa na usambazaji... Maeneo hayo siku zote na daima yana changamoto ya mitaji...

Eneo jingine .. Pita pita mitaani angalia guest zilizopo maeneo yenye mzunguko wa watu ..... Fanyia ukarabati na ingia mkataba na mwendeshaji anakupa chako kila week..

Unaweza kuwekeza kwembe kumbi za sherehe ... Kwa mtaji wa Million 20- 30 , ukilenga kumbi za watu 200-300, ukumbi utakodishwa kwa 600,000- 800,000 kwa wiki... utapata events 2-3 kwa wiki hukosi 1,800,000 kwa ukumbi mmoja ....

Unaweza kupata sehemu ya mapato ya mtoa huduma za chakula kwenye ukumbi huo au kuwa na catering yako mwenyewe na hata mtu wa mapambo anaweza kukulipa kwa biashara anayopata kila week kwenye ukumbi wako..

Ukiona inafaa na umeanza kuelewa mchezo, unaweza kuscale zaidi, kuongeza zaidi na zaidi..... Hauna mwisho.

Chukua kama 10-15 millioni unazunguka Tanzania ukisoma fursa na kuangalia ..... Usiweke mawazo mgando kwa maeneo fulani fulani.. Siku hizi kuna wilaya au centers kwenye wilaya mpya kuna fursa sana, ni wewe mwenyewe kufungua macho na usifanye biashara ya motivational speakers unapiga faida kwenye karatasi, tena field..

Haya ni mawazo, lakini utamu wa ngoma ni kuingia mwenyewe kucheza.
 
200m ni nyingi but pia ni ndogo

1. Ni nyingi kama wewe tayali mfanyabiashara so unaiweka kwenye biashara ambayo tayali ipo so unaiongezea mtaji na kukuza hiyo bishara hapo uhakika mtaji wako utakuwa na utatoboa

2. Ndogo kama huna idea na mambo ya biashara wala huna biashara inayoendelea so unataka hiyo 200 ndo ukaanze 0 kufungua biashara
Hapo risk ya kufail ni kubwa sana kuliko ya kufanikiwa
Kufail ni 80% na kufanikiwa ni 20%

Ingewezekana ungefanya iv
Akupe 50 m then uanziehe biashra angalau mwaka mzima unaanguka na kusimama taratibu utaanza kuwa mzoefu wa biashara na kujua wap mtu anafail na wap anafaulu hapo hata akikuongeza 100 au 150 iliyobaki utakuwa na uhakika wa kuendeleza ulipoanzia

Bro usijekudanganywa na motivation spekear au washaur sijui wa bank wanakuongoza kwenye biashara sijui kukufundisha never
Biashara haifindishwi unapambana ya hela yote huko ndani unafail na kunyenyuka na hapo ndo unakomaa
 
Sawa Mkuu 😂
Kuna mtu kasema elimu yetu inatuandaa kufanya kazi za kuajiriwa, sio kujiajiri. Mimi ni graduate lakini ona ninashindwa kujua la kufanya.

Hata hivyo tayari uamuzi wa kuacha kazi nimefanya, suala kubwa kwangu ni nizitumieje hizo Tshs 200M ili nifanikiwe? Wengi hapa naona pia wanakwama
 
Umeongea mambo yamenigusa sana. Ndio nimeelewa kwa kweli Tanzania tunasoma ili tuajiriwe!
 
Reactions: y-n
Koma Komaa ndugu idea itapatikana, hiyo fursa usiiachie hata kidogo.
 
Mkuu ninashida na wewe pls niruhusu nije PM ndugu
 
Mkuu Kwanza unabackground na biashara. Kama huna na huna discipline na usimamizi wa hela, hapo kaa chini Kwanzaa usikilize roho yako inatakaje manake very soon motivational speaker wa kilimo cha matikiti maji, Mara sumu za nyoka watakuja. Kuwa makini
 
Mkuu muamala ni wa ukahika kabisa. Hapo hakuna hofu yeyote.
Kwani wewe mwenyewe ungependa uwe/uitwe nani kati ya majina haya mawili? Mwajiriwa (Mtumwa/Kijakazi) na Mwajiri (Mtawala/Bosi)?

Kama unapenda uendelee kuwa Mtumwa wa kila kitu, endelea na kazi. Na kama unataka kuitwa CEO, basi pokea huo mzigo faster. Shughuli/biashara za kufanya zipo nyingi sana.
 
Mkuu mie ni graduate, lakini sijasomea mambo ya biashara, na sijawahi kufanya biashara yeyote ile. Niliwahi kulima mazao nikafeli vibaya mno hata hela ya mtaji haikurudi kutokana na kuanguka kwa soko la mazao
 
Bujibuji acha mzaha, this is serious, nategemea hekima zako!😄

By the way, wife anapinga kabisa suala la kuacha kazi!
Kama umeoa na una watoto baki na kazi yako ya kuajiriwa (Tshs. 1.5M). Unaoneka huna plan.

Tshs. 200M sio nyingi kama haujui nini cha kufanya. Unaweza kujikuta umebakiwa na 10M baada ya miaka 5.
 
Mwambie umeacha...Akutumie hiyo hela, uipokee...uanze Kitu utakacho fikiria...Mbeleni mambo yakikaa sawa, unaacha.

Hofu yetu ni kuwa unaweza acha, na asikupe hiyo hela...Na wewe pia usijiaminishe sana kupewa hiyo hela.

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…