Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Nyumba tunayo Mkuu, huo mtihani nilishamaliza

Fine...

Kama basi kuna jambo lolote unafikiri kulifanya, au utashawishika kulifanya kulingana na utavyoshauriwa, basi wekeza 50% pekee ya hela utayopewa...

Acha 50% nyingine kama mtaji #2, utaotumia ama kuboresha ulichoanzisha kama kikifanikiwa au kuanzisha jambo jingine kama utaloanzisha awali halitafanikiwa...

200mil si pesa nyingi sana haswa ikipata matumizi (ni nyingi pale unapokuwa huna matumizi nayo yoyote), of course hii ni principle ya pesa
 
Ama assume leo hii unastaafishwa kwa manufaa ya umma utafanyaje?!
Ulipenda ufanye nini ukistaafu?

Hio fani unayofanyia kazi saivi unaweza jiajiri kwa fani hio hio?.
 
Jipe muda
Jiulize unafanya kazi kwa sababu gani
Hela?heshima?huna options?

And test each theory
Km usingekua na kazi ungefanya biashara gani ungeifanyaje?
Kwanini?unaipenda?utaiweza?
Vyote hivyo ni vitu tofauti

Kitu cha moyoni can go a long way

Jiulize why za kutosha!.,
That is really great. Nadhani humu JF nitafika, naanza kuona mwanga mwisho wa tunnel
 
Yaani kuna jamaa kaniambia exactly maneno haya. Kwamba Tshs 200 ni hela ndogo sana I have to be very careful nisi rush kuamua
Ni hela ndogo kwenye bussness yaani unatakiwa utulize akili sana maana unaenda kufanya kitu ambacho hujawahi kukifanya na kikupe mrejesho ni kama wastaafu wanavyopoteza hela kwenye bussness.
 
Chukua hiyo hela alafu weka kwamza fixed deposit huku ukiwaza nini chakufanya
Okay, ila kumbuka nikiichukua hiyo hela maanake sina kazi. Ila uzuri kuna hii nyingine ya mafao
 
Mimi ningekuwa wewe kwanza na chukua 150M nanunua bonds za 25 years ambazo gawio lake linazidi mshahara nilio nao sasa.

50M nawekeza kwenye biashara yoyote ambayo ningeweza kuifanya bila pressure. Hapa ningekuwa wewe naanza biashara ya ufugaji wanyama wakubwa kama mbuzi, ng'ombe na kitimoto natumia mtaji wa 40M tu kwenye hili.

Stage ya kwanza ni muhimu kwa sababu hata mambo yaende vibaya vipi unayo hakika ya kupata kipato zaidi ya mshahara wako bila wasiwasi.

Mambo yakinyooka kwenye biashara ya ufugaji unaweza kuongeza mtaji kwa kuuza sehemu ya bonds za kwenye uwekezaji wa mwanzo.
 
That is really great. Nadhani humu JF nitafika, naanza kuona mwanga mwisho wa tunnel
Navyojua mimi biashara its not about money first..

Its about the Whys,passion na kitu,higher purpose,to prove a point,to conquer a certain market nk...
Yani jitafakari kwa kweli

Then the dynamics za hela uje nazo baada ya hapo
Risk ni zipi
Utapambana nazo vipi
Serikali inakusimamia vipi utaenda nayo sawa vipi
So mambo ni mengi jipe muda
 
Mimi ningekuwa wewe kwanza na chukua 150M nanunua bonds za 25 years ambazo gawio lake linazidi mshahara nilio nao sasa.

50M nawekeza kwenye biashara yoyote ambayo ningeweza kuifanya bila pressure. Hapa ningekuwa wewe naanza biashara ya ufugaji wanyama wakubwa kama mbuzi, ng'ombe na kitimoto natumia mtaji wa 40M tu kwenye hili.

Stage ya kwanza ni muhimu kwa sababu hata mambo yaende vibaya vipi unayo hakika ya kupata kipato zaidi ya mshahara wako bila wasiwasi.

Mambo yakinyooka kwenye biashara ya ufugaji unaweza kuongeza mtaji kwa kuuza sehemu ya bonds za kwenye uwekezaji wa mwanzo.
True story...
I buy bonds,kimradi kidogo pembeni na kazi siachi...

Ndugu akitaka proof ntafoji hadi akili imkae sawa...

Sm people wanapenda kazi walizonazo haziwatesi.,

Akivimba nimrudishie hela yake namwambia nipe muda
In 6 years or so umerudisha hela ya bonds unampa chake
Unaendelea kufaidi incoming sums hadi mwisho
 
I say, kila mtu anasema hivyo, maana nilifikiria kulima viazi mviringo jamaa wanasema kuna watu wamefilisika wanunuaji wa ujumla wanajipangia bei wanavyotaka na serikali wala haiingilii!
Usijaribu kuwaomba ushauri wana-CCM.Watakuambia jembe halimtupi mtu.Eti uende kwenye kilimo wakati wao wapo kwenye lami wanaendesha viieeitii!
 
Ama assume leo hii unastaafishwa kwa manufaa ya umma utafanyaje?!
Ulipenda ufanye nini ukistaafu?

Hio fani unayofanyia kazi saivi unaweza jiajiri kwa fani hio hio?.
Halafu yaani umeongea point, maana ananiambia I have to learn to take risks. Anasema nikikataa nikaja kupoteza kazi yangu nisimwombe tena hiyo hela! I have to decide now!

In fact hata alijoke kwamba kwani wewe ulipokuwa unamchumbia shemeji angekutalia kwa kuwa ana mtu halafu aje akufuate baadae kwa kuwa mtu wake amemwacha ungekubali kumchukua?🤣🤣🤣
 
Kama utapata ushauri wa wafanya biashara hiyo fedha katika biashara pato la faida la mwezi 1, ni sawa na accumulation ya mshahara wako wa mwaka. Hapo nazungumzia biashara yenye return ndogo ya 10% kwa mwezi. Ukipata ya 20% pato la mwezi ni miaka 2. Uamuzi ni wako umasikini au utajiri.
 
Usijaribu kuwaomba ushauri wana-CCM.Watakuambia jembe halimtupi mtu.Eti uende kwenye kilimo wakati wao wapo kwenye lami wanaendesha viieeitii!
Kuna mtu kasema viongozi wetu wanatuambia vijana wetu wasitegemee kazi za ajira wajiajiri wakati wao wanadanganya na hata kuua ili waendelee kuwa na kazi walizonazo! Yaani ilibidi nicheke, maana nilikumbuka hawa jamaa wanavyokwenda Mlingotini Bagamoyo kulinda ajira zao wakati wanasema vijana wetu wajiajiri wasipende kuajiriwa!
 
Kama utapata ushauri wa wafanya biashara hiyo fedha katika biashara pato la faida la mwezi 1, ni sawa na accumulation ya mshahara wako wa mwaka. Hapo nazungumzia biashara yenye return ndogo ya 10% kwa mwezi. Ukipata ya 20% pato la mwezi ni miaka 2. Uamuzi ni wako umasikini au utajiri.
Ndio mawazo yangu. Lakini hiyo bashara ni biashara gani basi? Nina mtaji nataka niingie huko.
 
Halafu yaani umeongea point, maana ananiambia I have to learn to take risks. Anasema nikikataa nikaja kupoteza kazi yangu nisimwombe tena hiyo hela! I have to decide now!

In fact hata alijoke kwamba kwani wewe ulipokuwa unamchumbia shemeji angekutalia kwa kuwa ana mtu halafu aje akufuate baadae kwa kuwa mtu wake amemwacha ungekubali kumchukua?🤣🤣🤣
Kuna mdau katoa hapo ushauri wa 150m bonds 50m biashara
Ila mi nashauri na kazi usiache
Raha ya utajiri ni double or triple sources of income
1.bonds
2.biashara hio ya 50m tafta kitu simple tu kiwe kinaingiza hela ya kawaida tu
3.usiache kazi km unaipenda

Ndugu foji mabarua nk
 
Mimi ningekuwa wewe kwanza na chukua 150M nanunua bonds za 25 years ambazo gawio lake linazidi mshahara nilio nao sasa.

50M nawekeza kwenye biashara yoyote ambayo ningeweza kuifanya bila pressure. Hapa ningekuwa wewe naanza biashara ya ufugaji wanyama wakubwa kama mbuzi, ng'ombe na kitimoto natumia mtaji wa 40M tu kwenye hili.

Stage ya kwanza ni muhimu kwa sababu hata mambo yaende vibaya vipi unayo hakika ya kupata kipato zaidi ya mshahara wako bila wasiwasi.

Mambo yakinyooka kwenye biashara ya ufugaji unaweza kuongeza mtaji kwa kuuza sehemu ya bonds za kwenye uwekezaji wa mwanzo.

Nilitaka niandike hili jambo, nikaona nipitie kwanza isijekua tayari kuna mtu ameshaandika.

Kwa mtu asiye na uzoefu wa biashara, hatakiwi kukurupuka, idea nyingi zitakuja na kwa kuwa ana pesa, atapenda aijaribu kila moja, kuja kutahamaki pesa yote imekata.

Anunue bond za muda mrefu kama za 100M kisha 80 M aweke fixed ya mwaka. 20 M aanze kufanyia mradi mdogo.

Hasi mwaka uishe, atakua ameshapata uzoefu na uelekeo wa biashara, ataqeza kuchukua kiasi kwenye ile 80M bila kuathiri makubaliano ya fixed account. Hii itampa uwezo wa kupanua biashara kulingana na mahitaji.

Wakati huo 100M inaendelea kumpa interest kama kawaida.
 
Usiwekeze kwenye kilimo usiwekeze kwenye daladala.
Nunua ardhi sehemu potential ambapo ardhi ni ghali angalau eka moja kwa milioni 10 unapata eka 20.Zisajili kata viwanja panga mitaa chonga barabara weka nguzo za tanesco kila plot,weka plot number hapo hapo fungua ofisi huku ukianza mradi wa matofali na vifaa vya ujenzi.Anza kuviuza viwanja hivyo kwa cash na Mkopo KILA eka moja gawa viwanja 6 uza milioni 10 KILA kiwanja so heka moja unapata milioni 60 so kwa heka 20 utapata bilioni 1.2 unaendelea kununua mashamba mengine kwa plan hiyo hiyo.Ndani ya miaka 2 sio wewe tena.
Real estate ukiijulia inalipa sana.
Hii aina stress wala hasara we Kazi yako ni kuwapigia tu simu wateja.
Hakuna kupewa hati bila kumaliza kulipa, unaruhusiwa kujenga huku ukiendelea kulipa sharti vifaa vya ujenzi ununue kwangu.
 
Kuna mdau katoa hapo ushauri wa 150m bonds 50m biashara
Ila mi nashauri na kazi usiache
Raha ya utajiri ni double or triple sources of income
1.bonds
2.biashara hio ya 50m tafta kitu simple tu kiwe kinaingiza hela ya kawaida tu
3.usiache kazi km unaipenda

Ndugu foji mabarua nk
Mkuu, kuacha kazi sio uamuzi wangu, ni sharti la sponsor! I give you USD 100,000 only if you are willing to quit your job and seriously pursue business, commit to it. You cant have both, your job and the USD 100,000.
 
Back
Top Bottom