Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Alijisemea wa ukae akili za kuambiwa changanya na zako, Kuna washiliki wa bigbrother walishinda mipesa wapo wapi? Mmoja juz alikuja kwenye msiba wa ndugu yake, hata Mimi mchovu naafazari.
 
Okay, na hilo eneo ni wapi, Dar, Dodoma, Arusha? Kuna mtu alisema Arusha hizo Tshs 200 ni kiwanja kimoja!
 
Alijisemea wa ukae akili za kuambiwa changanya na zako, Kuna washiliki wa bigbrother walishinda mipesa wapo wapi? Mmoja juz alikuja kwenye msiba wa ndugu yake, hata Mimi mchovu naafazari.
Ndio hao jamaa yangu anasema wanaitwa come easy go easy, hawawi serious na hizo hela kwa kuwa hakuna risk factor!
 
Project namba tu kwamba kufunga crusher ya kusaga mawe kupata kokoto na Changarawe nje nakuwa karibu na macontractor ikiwemo kuwapa tip na commission KILA wakipata Kazi nawasambazia kokoto za ujenzi.
 
Mkuu, kuacha kazi sio uamuzi wangu, ni sharti la sponsor! I give you USD 100,000 only if you are willing to quit your job and seriously pursue business, commit to it. You cant have both, your job and the USD 100,000.
Hapa ndo Tanzania bro
Mtengenezee fake papers..

Akija unachuka likizo unakaa kwny ile biashara ndogo uloanzisha

Mfano mini supermarket...
Wenye uzoefu watasema
 
Ndio mawazo yangu. Lakini hiyo bashara ni biashara gani basi? Nina mtaji nataka niingie huko.
Hujawahi fanya biashara ndio maana. Hapo una hofu kibao ya kushindwa. Sikuambii ni ipi. Nakushauri tafuta mtu aliyefanikiwa katika biashara na unaemumini awe mentor wako. Hela zipo katika biashara ndugu. Na hiyo biashara ni ile ambayo mwenyewe unashiriki sio ambao hujui chochote.
 
Biashara ya magari au kilimo kwa anaeanza sio nzuri yafaa kwa mzoezi na pili mwenye hela ya ziada.
Biashara ya mabus, daladala zaidi ni kama kutafuta prestige real investors hawezi weka msingi wake kule
 
Mimi kwa akili yangu nafikiri ungetafuta viwanja sehemu nzuri na hot
Jenga nyumba mbili halafu uziuze kama unaona hela itakata anza na moja ya 3 bed
Hapo utaanza kupata experience ya ujenzi
Kazi kwa sasa usiache kabisa kwani ujenzi ni kutafuta mjenzi muaminifu na wanapatikana ukiuliza hata humu

Baadae ukifanikiwa utajisogeza kwenye viwanja ghali na sehemu nzuri zaidi na kujenga tena
Mwisho unaweza kuwa mnunuzi na muuzaji wa majengo kila sehemu Tz na utasafiri sana na kula maisha na wife
Hapo vipi
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Ni milioni Mkuu. Actually amesema atanipa USD 100,000.
Changamsha akili bro
Kwani kakushikia bastola?!
Kwani ulimuomba?

Hii ni fursa ya wewe kutoka kimaisha itumie vizuri kwa namna inayokufurahisha na kukunifaisha wewe zaidi

Niache kazi kwani nilikuambia siipendi kazi yangu
Angejua hajui wallahy!
 
Exactly! Nina hofu kubwa mno ya kufeli. Nina mke na watoto wadogo
 
Okay, na hilo eneo ni wapi, Dar, Dodoma, Arusha? Kuna mtu alisema Arusha hizo Tshs 200 ni kiwanja kimoja!
Arusha na Dar ndio Tza.Pengine huko plot zipo chini sana.
Dar watu wanayo mashamba yao na yamezungukwa na miji tayari mfano bunju,kigamboni,boko,nk.
Muhimu tu usiwe bahili kwa madalali wanajua viwanja vipo wapi
 
Biashara ya kununua government bond inawafaa wastaafu,ukistaaafu usifanye biashara kula maisha tu zikiisha ngojea kifo tu, biashara yafaa ujanani
 
Uoga wako ndio umasikini wako chukua muda hata wa mwaka mmoja ikijipanga kipi cha kufanya kitakachoweza kukupa return nzuri then uamue kufa au kupona kwamba hizo million 200 either zikupe utajiri au zikupe umasikini.
Kikubwa katika biashara kabla hujafungua angalia usalama wa mtaji kwanza hata kama mambo yakienda kombo kamwe mtaji usitetereke.
Biashara yenye faida kubwa kuliko kawaida usiifanye maana risk ya kupoteza mtaji mkubwa pia upo.

Ingia kwenye biashara pata ushauri kutoka kwa watu wenye uzoefu acha uzoefu na maarifa yao yalinde mtaji wako kamwe hutajuta.
 
Changamsha akili bro
Kwani kakushikia bastola?!
Kwani ulimuomba?

Hii ni fursa ya wewe kutoka kimaisha itumie vizuri kwa namna inayokufurahisha na kukunifaisha wewe zaidi

Niache kazi kwani nilikuambia siipendi kazi yangu
Angejua hajui wallahy!
Sijamwomba. In fact yeye anaona kama ananisaidia kutoka utumwa wa kuajiriwa hadi kuzeeka. Anasema hakuna mtu Tanzania anakuwa tajiri na kufanikiwa kwa mshahara. Lazima awe ni mwizi, mla rushwa au fisadi, na anajua mie ufisadi siwezi kufanya na hata hivyo kazi yangu sio ya kufanya ufisadi au rushwa hata ningetaka. Sana sana nikijiongeza ni trip ya mikoani ya kikazi na sio nyingi, labda mbili au tatu kwa mwaka.
 
Kanunulie woh bus Cruser ya utalii mil 190 ndani ya miezi sita ela inarudi yote utalii ni hot sana gari ikienda kazin inalaza mil 5 kwa wiki nunua hio hautajutia mkuu
 
Ushauri wangu, fanya biashara kati ya hizi
1.Fungua duka la vifaa vya Ujenzi hutajilaumu.
2.Fanya biashara ya vinywaji Soda,bia,na maji, unakuwa Wakala ,unafungua bonge la Depot yako.
3.Fanya biashara ya Mazao,nenda maeneo ya boda, mfano Tunduma jenga Godown lako, linaweza kula km Million 40,zinazobaki unakuwa mtaji wako wa kukusanyia Mazao vijijini,then unakuwa unakuwa unawauzia wafanyabiashara kutoka nchi Jirani.Biashara hii inalipa sana.
4.Nunua mashine kubwa ya kukoboa mpunga,pesa inayobaki nunua mpunga wako na kukoboa,then unauuza,pia unakuwa unawakobolea na watu wengine, aisee bonge la biashara.
5.Jenga Lodge sehemu nzuri,then fanya biashara Wewe mwenyewe, utakuja kunishukuru.
6.Nunua Semi trailer, kwaajili ya kubebea mizigo ya wafanyabiashara ndani ya Mwaka unanua nyingine.
 
Project namba tu kwamba kufunga crusher ya kusaga mawe kupata kokoto na Changarawe nje nakuwa karibu na macontractor ikiwemo kuwapa tip na commission KILA wakipata Kazi nawasambazia kokoto za ujenzi.
Mashine za ku-crush kokoto!
 
Basi jitafakari
Unapenda au hupendi hio kazi?
Inakutesa ama haikutesi
Ina future nzuri au la?

Biashara usikurupuke
Hata km ni msaada mtu asipangie maisha bwn wee
Panga mwenyewe what works for you...

Utumwa ni perception!!
Utajiri ni kuwa na vyanzo viwili ama vitatu vya kipato..

Yani niache kazi nikachome mahindi mtaani wkt i can do both..
Fikiria
 
Muoneni hili jinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…