Comrade!
Nimesoma uzi wako kwa makini na nimepitia commments zote.
Nimegundua mambo matatu (3)
1. Wewe ni mtu makini ( nimesoma comments zako)
2.Anayetaka kukupa pesa ni mtu makini sana na ameshakupima akaona kuna kitu ndani yako (Anataka aki push kibadilishe maisha yako)
3.Ushauri wa walioajiriwa na hawajawahi kufanya biashara kama wewe na ushauri wa wafanyabiashara "waliofanikiwa" una tofauti kubwa sana.
Ushauri wangu:
1.Usijaribu hata kwa bahati mbaya kumdanya huyo ndugu yako kwamba umecha kazi.
2.Usiombe zaidi ushauri kwa wafanyakazi wenzako ( tafuta watu nje ya mfumo wa kazi yako)
3. Muombe ( Ndugu yako) kabla ya fedha akupe muda atleast miezi mitatu kama unaweza kuchukua likizo bila malipo halafu
kabla ya kuomba ushauri wowote kwa yetote jifungie mahali tulivu ujiulize..
"hivi mimi ninaweza kufanya nini"
pambana uhakikishe unapata jibu la hilo swali wewe mwenyewe, ukishapata kile uwezacho tafuta mtu anayekifanya umwombe akusaidie uzoefu hata kwa kujitolea kufanya kazi zake bila malipo. Tafuta uzoefu kwa nguvu zote halafu anza kwa fedha zako hata kama ni milioni 1
Ukishaona changamoto, fursa, raha na karaha za hiyo kazi yako na kuzipatia ufumbuzi ndipo uache kazi na umwombe ndugu yako akupe hizo fedha.
Note;
Kwenye biashara mtaji si fedha pekee
Mtaji ni
1.Uaminifu
2.Ujuzi
3.Mtandao wa biashara husika
4.Fedha (ni ya mwisho)
Kosa wanalofanya watu wengi ni kuweka fedha mwanzo kabla ya vitu hivyo 3.
Usifanye kosa hilo.
All the best mkuu.!!
Sent from my SM-M115F using
JamiiForums mobile app