Ndugu yangu anataka kunidhulumu ardhi niliyorithi toka kwa mzee. Naombeni msaada wa kisheria

Ndugu yangu anataka kunidhulumu ardhi niliyorithi toka kwa mzee. Naombeni msaada wa kisheria

mjegejo

Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
84
Reaction score
114
Niko 'frustrated' naomba mniwie radhi kama uandishi na mpangilio wa hoja yangu utashindwa kueleweka kwenu.

Ni hivi,

Mimi pamoja na kaka yangu mkubwa tumbo moja na baba tulikuwa tukiishi vizuri lakini uhusiano wetu ulianza kuingia doa baada ya mzee wetu kufariki.

Baada ya mzee kufariki kilikaliwa kikao cha ukoo na agenda kubwa ilikuwa ni kugawa mali za urithi ambapo katika kikao hicho walengwa wakubwa nilikiwa mimi pamoja na huyo kaka yangu.

Kwakuwa kifo cha mzee wetu kilitokea ghafla na hakuacha wosia wowote wa maneno wala maandishi, ukoo uliadhimia kugawa mali za urithi kwa utaratibu wa kimila. Ambapo iliamuliwa kuwa, kwakuwa sisi ni wa matumbo ili kuepuka mgogoro wa baade nyumba tuliyokuwa tukiishi na mzee iuzwe na pesa itakayopatikana tugawane kwa usawa. Nje na nyumba hiyo pia mzee aliacha viwanja viwili vya wazi ambapo tuligawiwa kila mmoja cha kwake.

Baada ya mgawanyo huo wa mali kaka yangu alienda kuishi kwao na mama yake mzazi na mimi nilienda kuishi na mama yangu kwenye nyumba ya kupanga. Baadae nilifanikiwa kujenga nyumba kwenye kiwanja changu cha urithi nilichokabidhiwa ambapo tunaishi hadi sasa.

Shida iliyojitokeza ni kwamba baada ya ule mgao wa viwanja kumalizika huyu kaka yangu yeye alimaliza akauza kiwanja chake na kwakuwa ni mtu wa 'tungi' pesa yote iliishia kusikojulikana na sasa ameanza kumendea kiwanja changu kwa madai kwamba ni cha kwetu wote na hiyo nyumba iliyomo ilijengwa na mzee. Katika madai yake anataka hicho kiwanja changu tukimiliki wote wawili au tukiuze alafu pesa tugawane.

Kufuatia sakata hilo nashindwa kabisa kumwelewa huyu kaka yangu. Hivyo basi nakuja kwenu wana jamvi kuomba msaada wa kimawazo na kisheria juu ya hatua nazopaswa kuchukua. Pia naomba kujua utaratibu wa kufuata ili niweze kutambulika/kumiliki kihalali ardhi ambayo haijapimwa.

Mawazo yenu ni muhimu wadau
 
Tunatoana roho yarabiiiihkwa mali alizoacha babaaaaah ×2

Huo wimbo huwa unaonesha mali ya urithi haijawahi kumuacha mtu salama.
Nashukuru kwa kibwagizo cha wimbo lakini ingekuwa vizuri endapo ungenishauri kwa chochote atleast nipate pa kuanzia
 
Muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi ya ugawaji mali za marehemu ndio utakaokuwa ulinzi wako,kama kikao kilifanyika kienyeji mtafute mwanasheria umuelezee waitwe hata ndugu walioshuhudua huo ugawaji,then akuongoze kufungua shauri mahakamani la kumshtaki kama hatamwelewa mwanasheria wako
 
Una nakala ya kikao kilichofanya mgawanyo wa mali? Mlipitia mahakamani?

Fuata taratibu za kuwasilisha nyaraka za zako na za kifo cha baba yako mahakamani, maliza huo mgogoro kabla ndugu wengine hawajalingana nae wakakudhulumu

Huyo ndugu yako anaweza akawa mlevi lakini asiwe mjinga!
 
Weka namba yako ya simu usaidiwe kwa urahisi zaidi!!
Kama maelezo yapo hivyo hivyo, kwamba hujabakisha wala kuongeza basi KESI YAKO NI LAINI MNO.....

NB: kikao cha mirathi kilikaa?
 
Mkuu pole sana,ila kwa hali hiyo basi washirikishe wazee wa ukoo waliohusika na kugawa mali hizo hapo mwanzo.Hao ndio watakaokusaidia kutatua tatizo hili
 
Mliandika muhtasari wa kikao n hayo makabidhiano!? Anakimendea kwa namna ipi anayohis yey itakuw halali!? Itisha kikao tena kam hamjaAndika muandike muhtasari n yeye awepo asaini nyaraka za kuidhinishwa kwa umiliki wako mbele ya wanandugu wote
 
mjegejo ameenda kujegeja kwanza, akirudi atajibu maswali yenu kuhusu muhtasari wa kikao cha mgao.

Asanteni.
 
Wajumbe wa kikao kulicuo gawa Mali hawapo ?

Kama wapo kuwe na kikao kingine kikihusisha wajumbe walewale bila kuongezeka hata mmoja ambae hakuwepo kwenye kikao Cha kwanza then muwaulize mgawanyo was Mali ulikuaje wao watasema


Lakini nawaza je katika kikao hicho hakukuwa na maandishi ?

Kama yapo yatumike

Mkishindwana basi ni kusonga mbele mahakamani mashahidi wako ni hao hao wajembe wa kikao Cha kwanza
 
Wewe bila shaka utakuwa ni wale binadamu wapole sana ndo maana nduguyo anataka kukuletea upuuzi
 
Kikao cha ukoo naimani kulikuwa na maandishi si ndivyo?
  • Kama ndivyo chukua hayo maandishi nenda kwa mwanasheria ukapate ushauri na jinsi ya kufungua shauri juu ya huyo ndugu yako
  • Kama hakuna maandishi, kusanya ndugu zako wa ukoo akiwepo mwanasheria waeleze maafikiano ya kikao kilichopita ili mwanasheria aliweke kisheria na kufanya nilichoshauri hapo juu.
Bila hivyo huyo kaka ako na kwasababu ushakiri ni mtu wa tungi na he has nothing to loose over the issue ataendelea kusumbua na mwishowe mtafikia tamati hata ya kudhuriana.
 
Kwanza itisha kikao au waombe wale waliosimamia mgawanyo wa Mali za baba yenu uwaeleze .Je,mligawana kwa maandishi ? Je,ilifunguliwa mirathi mahakamani au mlifanya kienyeji?
 
Back
Top Bottom