Ndugu yangu anataka kunidhulumu ardhi niliyorithi toka kwa mzee. Naombeni msaada wa kisheria

Ndugu yangu anataka kunidhulumu ardhi niliyorithi toka kwa mzee. Naombeni msaada wa kisheria

Brother nenda kwa mtaalam jizindike kwanza wewe na Mali yako maana vita inakuja. Baada ya hapo fanya michakato ya kisheria. Pole sana.
 
Mimi mzee alikata kamba Kama miaka 8 imepita nilikuwa nasimamia Mali zake alipoondoka duniani sikupata kitu lakini nashukuru aliniambia kabla kile kingetokea baadae baada ya yeye kuondoka na akasisitiza nipambane tu ili nije kutunza wadogo zangu.

Hayo maneno nikiyakumbuka tu huwa nakuwa focused hatari Sana. Yalikuwa maneno machungu Sana lakini ndio nilikuwa napewa dira ya maisha yalivyo.
 
Daah, muda mwingine Undugu kazi sana!!...Mpaka kikao kinatoa maamuzi hayo hakukuwa na ushahidi wa maandish juu ya mgawanyo huo wa mali za mzee.?
Ushahidi kuhusu mgawo wa mali upo kwenye muhtasari wa kikao cha ukoo lakini hatukuweza kwenda kufungua shauri la mirathi mahakamani.Je huu muhtasari una nguvu yoyote kisheria na pia naweza kuutumia kama ushahidi?
 
Hao walioshiriki hicho kikao cha ukoo umewashirikisha?
Ndio nimewashirikisha baadhi akiwemo baba yetu mkubwa ambaye aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi na ndugu wengine baadhi lakini sio wote
 
A
Muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi ya ugawaji mali za marehemu ndio utakaokuwa ulinzi wako,kama kikao kilifanyika kienyeji mtafute mwanasheria umuelezee waitwe hata ndugu walioshuhudua huo ugawaji,then akuongoze kufungua shauri mahakamani la kumshtaki kama hatamwelewa mwanasheria wako
Asante kwa ushauri mkuu. Ubarikiwe sana
 
Ndio nimewashirikisha baadhi akiwemo baba yetu mkubwa ambaye aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi na ndugu wengine baadhi lakini sio wote
Kama muhtasari wa kikao cha ndugu upo na msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa yupo hai na yupo upande wako sioni athari yoyote zaidi ya huyo nduguyo kukupotezea muda na rasilimali tu.

Labda ungekuwa unapambana na mtu mzito mwenye pesa za kuhonga watu.
 
Una nakala ya kikao kilichofanya mgawanyo wa mali? Mlipitia mahakamani?

Fuata taratibu za kuwasilisha nyaraka za zako na za kifo cha baba yako mahakamani, maliza huo mgogoro kabla ndugu wengine hawajalingana nae wakakudhulumu

Huyo ndugu yako anaweza akawa mlevi lakini asiwe mjinga!
Nakala ya muhtasari wa kikao ninayo mkuu lakini mahakamani hatukwenda kwa sababu sikutegemea kama siku moja yangejitokeza haya
 
Weka namba yako ya simu usaidiwe kwa urahisi zaidi!!
Kama maelezo yapo hivyo hivyo, kwamba hujabakisha wala kuongeza basi KESI YAKO NI LAINI MNO.....

NB: kikao cha mirathi kilikaa?
Kila kitu kipo kama nilivyoeleza na kikao cha mirathi kilikaa na nakala ya muhtasari wa hicho kikao ninayo
 
Nakala ya muhtasari wa kikao ninayo mkuu lakini mahakamani hatukwenda kwa sababu sikutegemea kama siku moja yangejitokeza haya
Tafuta cheti cha kifo cha babako, uwe na cheti chako cha kuzaliwa, na hiyo nakala ya kikao... Nenda mahakama ya mwanzo watakuelekeza cha kufanya. Hakikisha mnamalizia kila kitu mahakamani ikiwa ni pamoja na kuuza na kugawana vilivyobaki

Hizo document toa copy na scan uzisave sehemu tofautitofauti. Usishangae siku ukazitafuta ulikozihifadhi na kuzikosa
 
Mbna kama una vitu unaficha inawezekana vp kaka yako atoke tu huko aanze kusema kiwanja chenu wote

Heb tueleze kuna kingine nyuma ya pazia
 
Kikao cha wanandugu hakihusiki kugawa Mali, chenyewe kina husika kuteua msimamizi wa mirathi ambae baadae atakwenda Mahakamani kuthibitishwa. Baada ya hapo kazi yake inakuwa kugawa Mali kwa wanao stahili.

Ushauri wangu, nenda kwa wanasheria watakusaidia kumaliza tatizo lako.
 
Kwa kutumia Nyaraka za Kikao kimila kilichotoa maamuzi.. nenda halmashauri waombe wakupe kibali cha kupima na hatimaye umilikishwe kisheria.

Mtafute mtaalamu akuandalie maelezo yanayojitosheleza ya ushawishi kwa mamlaka ikiwa nyaraka zako hazijitoshelezi... Je uliomba kibali cha kujenga!? Kwenye kiwanja chako!?

Hizi ni baadhi ya taarifa muhimu.. kama unaweza kumpata aliyeuziwa kiwanja na kaka yako.. ushahidi wa kugawana fedha za mauzo ya nyumba ya familia nk..

Sio kesi kubwa ni utulivu wa akili tu kwa anayekusimamia..
 
Tafuta cheti cha kifo cha babako, uwe na cheti chako cha kuzaliwa, na hiyo nakala ya kikao... Nenda mahakama ya mwanzo watakuelekeza cha kufanya. Hakikisha mnamalizia kila kitu mahakamani ikiwa ni pamoja na kuuza na kugawana vilivyobaki

Hizo document toa copy na scan uzisave sehemu tofautitofauti. Usishangae siku ukazitafuta ulikozihifadhi na kuzikosa
Asante kwa ushauri mkuu. Ngoja nianze huo mchakato
 
Mbna kama una vitu unaficha inawezekana vp kaka yako atoke tu huko aanze kusema kiwanja chenu wote

Heb tueleze kuna kingine nyuma ya pazia
Mkuu hakuna nilichoficha. Mi pia hii hali imenishangaza sana ila nadhani huyo ndugu yangu ameamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha alionao.
 
Kikao cha wanandugu hakihusiki kugawa Mali, chenyewe kina husika kuteua msimamizi wa mirathi ambae baadae atakwenda Mahakamani kuthibitishwa. Baada ya hapo kazi yake inakuwa kugawa Mali kwa wanao stahili.

Ushauri wangu, nenda kwa wanasheria watakusaidia kumaliza tatizo lako.
Ubarikiwe kwa ushauri mkuu
 
Nashukuru kwa kibwagizo cha wimbo lakini ingekuwa vizuri endapo ungenishauri kwa chochote atleast nipate pa kuanzia
Wahi kamshitaki mashahidi si unao(ndugu waliokaa kwenye kikao cha mgawanyo wa mali za mrehemu) Usisubiri akuwahi wewe maana utaenda mahakamani kama mshitakiwa.
 
Ushahidi kuhusu mgawo wa mali upo kwenye muhtasari wa kikao cha ukoo lakini hatukuweza kwenda kufungua shauri la mirathi mahakamani.Je huu muhtasari una nguvu yoyote kisheria na pia naweza kuutumia kama ushahidi?
Vyema kama nakala zipo...Kama walivyotangulia kukushauri wajumbe huko juu jitahidi kufata hatua za kisheria .
 
Mkuu Kama waraka wa kikao Cha ugawanywaji Mali unao na mashahidi wapo. Wahi kumshtaki anakusumbua na kukutishia.

Kwanza mtu mwenyewe chapombe nenda hata police tu wape kitu kidogo wamtishie akae selo hata wiki tu. Mbona atashika adabu.
 
Back
Top Bottom