kizaizai dah hivi kaka nitajie msanii ambaye hatokuja kuchuja au kufulia yyt yule duniani, diamond ni brand haja ajiriwa anatumia brand zake (WCB, CHIBU, Diamond platnumz). Kangaza karanga, chibu kwa hiyo ana share tena ya kudumu vizazi na vizazi, hivi Dr dree ana hit gani sasa hivi billboard lkn still anauza headphones zake beat by dree na dree hana kiwanda wala mashine za kuzalisha phone ila ana asilimia yake mpaka anaingia kaburini kwa sababu brand yake ya Dr dree , Michael Jordan sasa hivi kastaafu basketball hasikiki kama zamani lkn yy na Nike wameingia mkataba wa kutumia brand yake Jordan kuuza viatu ila Kuna asilimia Nike wanamlipa Jordan kwa sababu wanatumia brand yake Jordan, kumbuka Jordan hana kiwanda, hivyo hivyo Kanye West anauza viatu kupitia brand yake yeezy na ameingia mkataba na Adidas, Kuna asilimia Kanye anaingiza, hao wote Kanye, Jordan na Dr dree hawasikiki lkn bado wanaendelea kupiga ela kupitia brand zao walizo zipromoti mpaka wanaingia kaburini na hata vizazi vyao vitakuwa bado wanaendelea kuingiza hela kwa sababu yao sijui unanielewa. Kama unafuatili future ya dunia ijayo hasa ktk maswala ya mziki mauzo mengi yatakuwa online, ndio ipo hivyo CD watu wameichoka, kwa diamond anapiga ela ktk website yake ya wasafi. Com kama ilivyo kwa Jay Z kwa tidal na kama umenunua hasa Hizi compyuta ambazo ni toleo jipya hamna CD ROM wanatumia USB ports sijui unanielewa ndio mambo yanavyofanyika ktk dunia ya sasa, promote brand yako sasa hivi ukiwa ktk peak position of your talent ili hata kesho ukistaafu au ukifulia unaendelea kupiga ela kama wafanyavyo akina Dree, Diddy, Kanye, Beckham nk. Hivi kama unafuatilia mpira kwa nini Ronaldo anahangaika sana kufungua bidhaa zenye label ya CR7(viatu, boxer), kijana funguka hata ww kesho ukiwa maarufu promote brand yako ili kesho ukikaa pembeni ela inaingia kupitia brand yako. Unaweza kweli ukachuja lkn brand ikaishi vizazi na vizazi, kama hujui hamna kazi ngumu kama kubadilisha brand ya bidhaa ambayo ishakubalika sokoni na ukaipa jina jipya,kwani ni risk kubwa sana na unaweza ukatumia gharama kubwa kuiprimoti na ukafeli, ukasababisha mauzo kushuka au hata kampuni kufa kama unabisha hebu tafuta watu wa marketing wakupe darasa ndio utaelewa. Sasa kama hiyo komenti yako inaongozwa na msukumo wa timu zetu hizi umekosea kwani hata siku moja huwezi ua brand hata kama baadaye ukifulia ni hayo, kama ukibisha endelea kukaa na ubishi wako kama wale wafuasi wa mange, kila kitu mange kasema.