Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

Tatizo ni kwenye hiyo 50k unayompa kila wiki, ghetto la kujiachia na msosi wa uhakika, afanye kazi ya nini tena

Kazi ni kweli ndogo, muda mrefu wa kufanya kazi lakini sioni mantiki ya yeye kuona unamnyanyasa pasipo kuangalia jitihada unazoziweka ili aishi vizuri

Mkuu kama upande wako hauna tatizo lolote, usimpe chaguo, muambie aende huko ili akajue dunia inaendaje la sivyo utampoteza mazima
 
Mwache.
 
Unampa kila week 50,000, anakula na kulala bure hana stress in short, kama ni wewe ni me na yeye ni me jiandae atanawiri sana na atakugongea hata mkeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…