Ni Kama huna uwezo wa kubeba mimba ndio maana umeyaandika haya kana kwamba wanawake hao ndio waliokunyima uwezo wa kuzaa! Lau Kama una uwezo wa kuzaa uliwasiliana na hiyo mimba ya mtoto wako kuwa atakuwa mtu wa aina Gani! Usisahau nawe ni mwanamke na hao wanaotuhumiwa walizaliwa na wanawake Kama wewe!
Isitoshe wewe ni mkristo na unajua jinsi Mama Bikira Maria alivyokuwa anamlilia mwanaye Yesu wakati wa mateso yake na hakumuacha Hadi alipokata roho! Wewe Kama mwanamke unatakiwa uwape pole wenzako badala ya kuwadhihaki maana dhambi hiyo yaweza kuzaliwa nyumbani kwako! Acha dharau!