Ndugu zangu kwenu biashara zinakwendaje?

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
Ndugu zangu Wajasiriamali, wafanyabiashara vipi hali za biashara huko kwenu zikoje? Kadri siku zinavokwenda naona maluweluwe biashara inazidi kuwa ngumu halafu ukicheki unatakiwa ulipe kodi ya pango, huku TRA wanataka kodi zao, mara manispaa wanakagua leseni hujakaa vizuri watu wa taka na fire wanataka pesa ukicheki biashara ngumu hakuna wateja yaani daah mpaka unaona kizunguzungu. Bank unadaiwa yaani tabu tupu.

Nagoli hapa Kariakoo nauza mashuka/mapazia ila naona dalili za kufunga nicheki sehemu nyingine au niangalie upepo wa biashara nyingine vipi kwenu huko ndugu zangu biashara zikoje au mimi nimelogwa?? Ila ndugu zangu karibu wote wanalia biashara ngumu.

Kiukweli toka Mama aingie madarakani biashara zimekuwa ngumu sana sio hii nilikuwa na biashara ya kuuza lubricants za magari pale Kamata ilibidi nifunge nilikuwa sipati faida kabisa.

Ndugu zangu upepo kwenu unavumaje?
 
Hakuna unafuuu, mambo mbaya
 
Mkuu kweli biashara kwa sasa ina changamoto cha msingi ni kubadili biashara tuanze kupeleka mahindi Kenya, maana hii ndio biashara haina kudorola.

Ugumu mwingine unasababishwa na wewe kuwa upande wa Russia.
 
Mkuu kweli biashara kwa sasa ina changamoto cha msingi ni kubadili biashara tuanze kupeleka mahindi kenya, maana hii ndio biashara haina kudorola,

Ugumu mwingine unasababishwa na wewe kuwa upande wa Russia.

Kwani Russia ametupa vikwazo sisi ndo wajinga tunaogopa kununua wese kwao afu bei chee
 
Mkuu juongeze huko huko kariakoo uwe na biashara za juu juu hata 3 ili mradi siku ziende. Usitegemee biashara moja.

Ishi kijanja ndugu yangu

Nilishapata mmoja nilikuwa nampa mzigo akakimbia na pesa zangu mpaka leo sijawahi muona, kuna plan B naifikiria nimepewa na makonki wa Kariakoo ukijifanya mwema sana kwa Tanzania hutoboi.
 
Nilishapata mmoja nilikua nampa mzigo akakimbia na pesa zangu mpaka leo sijawai muona, kuna plan B naifikiria nimepewa na makonki wa kariakoo ukijifanya mwema sana kwa tz hutoboi
Hapo hapo shikilia [emoji848]
 
Hakuna mtu anatoboa kwa kufuata sheria na kufanya Kila kitu kihalali. Jiongeze

Wakati wa Jiwe mlisema vyuma vimekaza, sasa bado kilio ni kile kile sometimes you have to look within sio kutafuta mchawi nani.
 
Nilishapata mmoja nilikua nampa mzigo akakimbia na pesa zangu mpaka leo sijawai muona, kuna plan B naifikiria nimepewa na makonki wa kariakoo ukijifanya mwema sana kwa tz hutoboi
Usianze kuroga tu
 
Kama Kariakoo unalia, je waliopo pembezoni mwa Mji?.
 
Ongeza sauti.....tushajadili humu. Biashara imedorola wakati wapambe wanaimba mapambio.
Bora nusu shari kuliko shari kamili, ngoja niendelee kula mshahara na posho awamu hii ya sita.

Niwakumbushe tu vijana wekezeni kwenye kilimo na ufugaji, mtakuja nishukuru siku moja.

Hutoona TRA akitaka kodi kwenye mauzo ya maziwa hata siku moja.
 
Mkuu mim TRA wanataka wanasumbua Mara sjui tukague stock aisee biashara naiona ngumu sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…