Cash Generating Unit
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 13,286
- 39,418
Ndugu zangu Wajasiriamali, wafanyabiashara vipi hali za biashara huko kwenu zikoje? Kadri siku zinavokwenda naona maluweluwe biashara inazidi kuwa ngumu halafu ukicheki unatakiwa ulipe kodi ya pango, huku TRA wanataka kodi zao, mara manispaa wanakagua leseni hujakaa vizuri watu wa taka na fire wanataka pesa ukicheki biashara ngumu hakuna wateja yaani daah mpaka unaona kizunguzungu. Bank unadaiwa yaani tabu tupu.
Nagoli hapa Kariakoo nauza mashuka/mapazia ila naona dalili za kufunga nicheki sehemu nyingine au niangalie upepo wa biashara nyingine vipi kwenu huko ndugu zangu biashara zikoje au mimi nimelogwa?? Ila ndugu zangu karibu wote wanalia biashara ngumu.
Kiukweli toka Mama aingie madarakani biashara zimekuwa ngumu sana sio hii nilikuwa na biashara ya kuuza lubricants za magari pale Kamata ilibidi nifunge nilikuwa sipati faida kabisa.
Ndugu zangu upepo kwenu unavumaje?