Ndugu zangu nimeanza kujifunza kuhesabu kwa lugha ya kiarabu, tujifunze pamoja tuache kung'ang'ania kiingereza

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Nimeanza jifunza kuhesabu kwa kiarabu

Nimeona niwe tofauti na Wakristo wenzangu wanaoamini kuwa kiingereza ndiyo lugha sahihi zaidi kwao kuliko lugha nyingine

Kiarabu ni mojawapo ya lugha bora Duniani tena iliyotumika kushushia kitabu kitakatifu

Asubuhi ya leo nimeona tujifunze pamoja kuhesabu kuanzia moja hadi kumi

1. Wahedaa
2. Sania
3. Salatha
4. Alba
5. Hamsa
6. Sitaa
7. Sabaa
8. Samania
9. Tisaa
10. Ashara

Wanazuoni kama kuna makosa naomba mnirekebishe

Asubuhi njema wapendwa

Naomba ushauri wa njia bora zaidi ya kupata elimu hii muhimu
 
Kuhesabu pia lazima nivae kanzu na barakashia?
 
Why nijifunze kiarabu? Kwa faida gani na kwanini?
 
Yote kheri
 
Aliyekudanganya Quran imeshushwa ni nani?
 
Kuziandika umeshindwa pakubwa.Anza kujifunza kiebrania.
 
Kiarabu hakina faida yoyote kwa sababu hakuna kitu cha maana cha kiuchumi kitatoka uarabuni.

Sasa hivi jikite kwenye lugha za mashariki ya mbali kama China, Japan, Korea na nchi za mashariki ya mbali.

Uarabuni unajifunza kiarabu kikusaidie nini, hakuna economic potentiality, wabaguzi, watu wa hovyo.
 
Kiarabu ni muhimu sana ukijuwa kitakukufaishaje, binafsi natamani ningejuwa kiarabu kwangu ni deal kubwa.
 
Hatuhitaji mikariro hapa na hatuhitaji kusoma kitu kisichokuwa na faidaa

Hao wenye Lugha yao wenyewe wanahangaika na Kingerezaa ili wapate kulaaa .
So jitafakari maana utakufa maskini na utapata majinii
 
Ukujua kuandika na kuongea kiarabu kama Mimi sjui itakuwaje
Anyways....jayiiid👊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…