Uchaguzi 2020 Ndugu zangu wanaCCM kweli tulikosea, tuchutame

Uchaguzi 2020 Ndugu zangu wanaCCM kweli tulikosea, tuchutame

Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Hoja yake je ni ya uongo
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Unataka kutuaminisha kuwa ccm hakuna mtu mwenye akili anayeweza kuona mambo yasiyofaa ndani ya serikali au anayeweza kuhoji mambo yakienda ndivyo sivyo?
 
Man Mvua,

Kati ya makosa makubwa CCM watajilaumu kumuacha akazuia Shughuli za Vyama vya siasa na kudhulumu uchaguzi wa Serikali za mitaaa mwaka jana ndio matokeo yake tunayaona leo...
Makamanda, matokeo yatakayosomwa baada ya October 28 yatawashangaza pengine itabidi mjipange foleni mahospitalini kupima afya baada ya kupata shambulio la moyo. Msijipe matumaini ambayo hayapo kabisa.

Magufuli anashinda kwa asilimia 95% inaonekana hamuelewi kama Thomaso. Tundu lissu kupata kura 500,000 atakuwa amejitahidi sana. Poleni ndiyo ukweli huo japo unauma, subirini kipenga kipigwe mtapoteana kabisa.
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Sawa Mimi kamanda. Hilo linakuongezea nini katika maisha yako.
 
Hayo yasiyatamke kabisa badala yake ajikite kwenye ilani mpya.
 
Ahsante sana kiongozi ngoja tujipange upya. Tatizo kubwa lililotokea ni WALIOSHIBA kupewa mic huku WENYE NJAA kuambiwa wapiga deal.
 
Man Mvua,
Kama mnakili mna madhaifu yote hayo kwa Nini msikubali, kushindwa ili mkae pemveni, wachukue wapinzani
Hakuna kurudi nyuma, wala hakuna kushusha silaha, ni mbele kwa mbele mkuu. Hii ni vita. Ahsante kwa kujali
 
Kunywa bia utakavyo.. nakuja kulipa bili.[emoji111]
 
Wewe ni mwana Lumumba mwenzangu kweli ? Mbona unaongea vitu vya uchochezi .
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Kwani anaetumia picha ya Magufuli kuikosoa CCM lazima awe Magufuli mwenyewe?

Hiyo picha simply ina symbolise mtu wake, mentor, idol, hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu yake kuwa mpinzani.
 
Habarini wanabodi,

Kwanza naomba nitamke wazi kwamba mimi ni mwanaccm kindakindaki na nimepanga 2025 kuonana na wajumbe.

Naomba niseme wazi kwamba ccm tulikosea kwenye vipaumbele vyetu, tuliegemea upande mmoja zaidi.( ujenzi wa miundombinu zaidi). Ni kweli Rais wetu kafanya mambo mengi sana mazuri na yenye tija kwa Taifa letu ila yote aliyofanya ilitakiwa yaendane na hali ya kiuchumi ya mtanzania mmoja mmoja. Rais wetu angekuwa Rais bora zaidi Duniani kama spidi yake ingeenda sambamba na yafuatayo:

1. Utoaji wa ajira kwa watanzania wanyonge (maskini) ambao wengi wao walisomeshwa na wazazi wao kwa shida kubwa na ndio wamejaa kwenye kada ya kilimo, Uvuvi, Ualimu na majeshi. RAIS ANAPOSEMA NI RAIS WA WANYONGE BILA KUFANYA HAYA ANAFIKIRISHA SANA kwa sababu hao wanyonge aliyofanya mengi hayawanufaishi kabisa ndio maana katika hili hatuna hoja.

Kuwaambia vijana wajiajiri ni kuwakosea sana mana Madaktari na maprofesa waliopo CCM wangekuwa mifano katika hili, pia wabunge wote baada ya kupokea 240M wangekuwa mifano mizuri sana katika hili, lakini wapiiii !! Wote wameenda majimboni kutafuta ajira kwa wananchi pamoja na kwamba wana mitaji.

Juzi Donard Trump alikuwa anajidai kwa kuzalisha ajira 1.5M ndani ya miezi miwili. Hili tunalizungumziaje wana CCM?

HOJA YA AJIRA TUKUBALI TUMEFELI VIBAYA SANA, tumefikia hatua kuwaambia wananchi wajitolee huku majukwaani tukijidai nchi ina pesa na ni tajiri. Vituko kwa kweliii

2. Mishahara kwa wanafanya kazi wa nchi hii. Hapa pia tukubali kwa miaka 5 hatukutenda haki kwa wafanyakazi, tuliwaongopea miaka yote minne labla tulidhani miaka 5 ni mingi sana. UKWELI MCHUNGU HAPA TUSHAUMIA SANA. WANACCM HAPA HATUNA HOJA, TUCHUTAME.

3. Vyeo na madaraja. Tumeshuhudia majeshi yetu yakipewa vyeo na kupanda madaraja kwa kipindi chote cha miaka 5 ila kada zingine tangu 2013/2014 watu hawajapanda madaraja kwa kuwa hakuna pesa, hapa tulikosea sana tungepandisha kidogo kidogo tangu 2015 sa hivi tungekuwa hili tatizo tushalimaliza kabisa. Kwenye kada ya Elimu hiki ni kilio kikuu.

4. HAKI, SHERIA NA WAJIBU, nadhani hatujui kutofautisha hivi vitu vitatu.

5. RUSHWA. Hapa napo CCM hamna kitu tumefeli pia. RUSHWA AKITOA MASKINI AU ASIYE NA JINA, AKITOA TAJIRI AU MWANACCM NI TAKRIMA.

6. Ule msemo wa wanaolalamika ni wezi au wamebanwa kwenye mambo yao ulikuwa wa KUPOTOSHA na kumpoteza Mh: Rais. Wanyonge wengi wa Mh.Rais walikuwa wakilalama hali ngumu WATEULE wake walikuwa wana mwambia hao ni wale MAFISADI uliowatumbua. WASAKATONGE MMETUHARIBIA CHAMA.

Mwisho

Wana CCM tujipange kisawasawa kutengua hoja za wapinzani wana hoja muhimu sana, kamwe huwezi kusifia ujenzi wa miundombinu wakati tumbo lipo tupu (wanufaika wa utawala huu kaeni pembeni kidogo tuokoe chama).

TUSIKOSEE TENA KWENYE ILANI YETU IJE KUMNUFAISHA MTANZANIA MMOJAMMOJA NA SIO PESA ZOTE KWENDA NJE KWENYE UNUNUZI WA NDEGE.

Mwisho kabisa

Tuombe msaada kutoka kwa comrade kinana, Nape na Makamba. Watusaidie mbinu maana tumeshikwa pabaya.

Ahsanteni sana.
Watanzania wore tungekuwa wakweli na wawazi kiwango hicho leo Tanzania tungeizidi Marekani na Ulaya kwa. Mambo mengi sana
 
Kwa ajiri ya Hoja no. 6
Kura yangu inaenda kwa Lissu!

Hiyo ndo namna pekee ntapaza Sauti yangu!
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani sukari ikiuzwa 1,800/= leo inauzwa 2,800/= (bei elekezi) bado unaminyana na wanaotoa hoja?
 
Back
Top Bottom