Ndugu zangu wenye mioyo ya kutoa kuweni makini na wanaoonekana ombaomba mitaani, wengi wao matapeli na vibaka

Ndugu zangu wenye mioyo ya kutoa kuweni makini na wanaoonekana ombaomba mitaani, wengi wao matapeli na vibaka

Utapeli upo wa wingi. Hudusan kwa mgongo wa imani za watu. Hilo halipingiki.

Unenikumbusha watu wanavyochapwa (tapeliwa) sijui na mchungaji gani yule na wazo la udongo aliloliona JF.

Kuna Bi Zainab Tamim hapa JF anautangaza udongo wake wa tiba na urembo wa ngozi kwa zaidi ya miaka kumi sasa hapa JF. Hakuna malalamiko.

Huyo mchungaji tapeli kayaona hayo JF sasa anawachapa wajinga ndiyo waliwao mitaani huko.
Dah!! Watu hawana huruma na binadamu wenzao.....😂
 
Segerea mwisho kulikuwa kuna kundi kila Jumapili wanatembea na kanzu zao na makaratasi wakisema wanachangisha pesa za madrasa na kituo cha watoto yatima kilichopo Chanika.

Kuna mmoja wao kwa bahati nzuri ama mbaya alishanichangisha mara 2 tofauti hivyo nilimkariri sura. Na alikuwa na mfano wa kovu kubwa usoni kumfanya iwe rahisi kuweza kumkumbuka.

Siku moja nilikuwa maeneo ya Banana nikaona kundi kubwa wakiwa wamevaa fulana za sare ya kanisa (kutokana na maandishi ya kwenye fulana) wakizunguka na biblia zao kuomba msaada wa ujenzi wa kanisa na kituo cha watoto yatima kilichopo Pugu. Walipopita karibu yangu nikamkumbuka yule kijana wa Segerea akiwa mmoja katika hilo kundi.

Ilibidi nimsimamishe yule kijana na kumuuliza kama kabadili dini. Mwanzo alijifanya hanielewi ila nilipomkazia ikabidi awe mpole. Akasema bro kausha tunatafuta rizki tu.

Nilichogundua jamaa ni wasanii mno wa kucheza na akili za watu. Alipokuwa anaomba kama muislam na lafudhi pia aliiweka kiislam slamu na alipokuwa anachangisha kikristo, halkadhalika dialect aliiweka kikanisa kanisa.

Kiuhalisia hawana kanisa wala msikiti wanaoombea. Ni mradi wao tu, wanazunguka kukusanya pesa na mwisho wa siku wanaenda kunywea pombe.
Noma sana...
 
Hii haina haja ya kusalimiana,

Jana nikiwa kwenye harakati zangu za kutafuta mkate wangu wa kila siku kama ilivyo Ada kwa watu tuliombiwa tutakula kwa jasho. Niliibahatika kuingia kwenye jengo moja mitaa ya Masaki.

Wakati natoka kwenye hilo jengo nje nikakutana na kundi watu wanaoonekana ni MAUSTAADH wakiwa wamewazunguka walinzi wa jengo hilo na watu wengine wa karibu na hapo katika hali inayoonekana kama kuna mazungumzo ya kidini yanayoendelea.

Lakini kadri ninavyosogea karibu ndio naziona zile sura za wale MAUSTAADH. Sio sura ngeni ni vijana wa mtaani ninapoishi wapo kama wa nne lakini pia kwa ninavyo wafahamu sio watu wa dini bali ni hawa walevi hizi vipombe vikali huku kwenye maduka ya mtaani.

Wale MAUSTAADH baada ya kumalizana na pale wakaendelea na jambo lao mbele kwa mbele ndio nikasogea kuwauliza wale waliokuwa wakipatiwa ilimu na kuwauliza nini kilikuwa kinaendelea wakasema wale MAUSTAADH wanachangisha fedha za ujenzi wa msikiti na Madrasa maeneo ya Chalinze.

Kweli dunia inaelekea kubaya, nikafikiria kuwachoma lakini nikahofia usalama wao.
Nilivyosoma kichwa cha habari nikaona nisome nini kimewasibu ombaomba mana na mimi ni mdau wa kuwapa chochote kitu.

Hao uliowaona siyo ombaomba bali ni wachangishaji wa mchango kwa ajili ya jambo fulani mfano ujenzi wa taasis nk.

Ombaomba ni wale ambao wanaomba kwa ajili ya maisha binafsi.

Turudi kwenye hoja.

Ukimuona mtu mzee sana au mlemavu wa viungo anaombaomba, wewe kama unacho mpe tu, kama hauna mwambie sina.

Wazee na walemavu wanahitaji msaada sana mana hawana namna ya kujikwamua. Hivi mzee sana anaweza kinyenyua zege?

Usianze kusema; "mara ooo! huyu mlemavu ombaomba ana mjengo kutokana na kazi hii"

Hiyo ndio kazi yake! Kama unacho mpe, kama hauna mwambie sina
 
Back
Top Bottom