Ndugu zangu wenye mioyo ya kutoa kuweni makini na wanaoonekana ombaomba mitaani, wengi wao matapeli na vibaka

Ndugu zangu wenye mioyo ya kutoa kuweni makini na wanaoonekana ombaomba mitaani, wengi wao matapeli na vibaka

Changia tu bila kujaji na Mungu atakubaliki kwa Imani,

Kodi zetu zinaliwa kila siku na matapeli ya kisiasa wapo radhi wasifanye kazi za B.O.T na Banker ili wawe wanasiasa ili watupangie matumizi ya kod zetu.

Kuna family moja na siasa ni mapacha wa kufanana

Kuna bibi mmoja kaonja siasa sasa amekuwa balaaa umwambii kitu siku alivyopewa fungua za pepo ya uongoo akaambiwa kila kitu kioo chini yako hakuamini akatest kama anajirushia muamala ngoma ikatiki akauliza wamsonga tunafaje akaambiwa rudi nyumbani kamnywe dam mzazi wako ndo utapaweza hapo kifo ni kifo sasa jini linataka limnywe na abdubanda analifosi kulipekea radha tofauti alitak yaani yupo radhi amtoe mtu kafara mchana mchana.

PDidy lubricant oils products....
 
Inawezekana kua wewe ndio hujaelewa ulichokiandika,

Unaposema Utapeli ni bora kuliko kua wezi au vibaka una maanisha nini?
Kipi kinafanya utapeli kua ni bora kuliko kua kibaka/wezi?
Hawajachukua mali ya mtu bila idhini yake wenyewe wanakuja na hoja yao ni wewe sasa kuwapa au kutowapa,mbona watu wanapiga mahela huko ya kueleweka na hakuna mtu anakemea ila mnaangaika na mtu aliejipa kazi ya uchangishaji kweli
 
NIKO powa,ina maana huwezi kuchangisha mchango wa ujenzi wa msikiti au kanisa la kijijini kwenu kusa mlevi,au nikiwa na bar sitakiwi kusali wala kutoa sadaka
Nadhani jambo sio kuchangisha bali kufikia makusudio ya michango wenyewe ndiko kunakoleta maana nzima ya utapeli na ulaghai.

Unapoomba hela ya kula hali ya kuwa wewe umeshiba isipokuwa una mambo mengine binafsi wewe ni tapeli kama matapeli wengine ingawa kuomba hela ya kula sio utapeli.
 
Hawajachukua mali ya mtu bila idhini yake wenyewe wanakuja na hoja yao ni wewe sasa kuwapa au kutowapa,mbona watu wanapiga mahela huko ya kueleweka na hakuna mtu anakemea ila mnaangaika na mtu aliejipa kazi ya uchangishaji kweli
Hao wanachangisha hela za kutumia wao wakijifanya ni za Nyumba ya ibada,huo ni utapeli,

Fraud ni criminal offense,hiyo ni kesi,na kama ni kesi basi hilo ni kosa kisheria,ndio hoja yangu ipoa hapa,
Obtaining money illegally by using deception tactics is a Fraud,
wizi sio lazima mtu akutishe kwa silaha au achukue chako kwa nguvu.
 
Changia tu bila kujaji na Mungu atakubaliki kwa Imani
Kodi zetu zinaliwa kila siku na matapeli ya kisiasa wapo radhi wasifanye kazi za B.O.T na Banker ili wawe wanasiasa ili watupangie matumizi ya kod zetu...
Kauli hii ndio inazalisha matapeli na walaghai.

Mola wetu mlezi ametupa ufahamu ili zitufae kwenye kukabiliana na maisha yetu ya kila siku. Pia mola wetu mlezi ametoa utaratibu wa namna ya kuchangia au kutoa msaada ili watu waeupukane na matapeli
 
Hao wanachangisha hela za kutumia wao,huo ni utapeli,

Fraud ni criminal offense,hiyo ni kesi,na kama ni kesi basi hilo ni kosa kisheria,ndio hoja yangu ipoa hapa,
Obtaining money illegally by using deception tactics is a Fraud,
wizi sio lazima mtu akutishe kwa silaha au achukue chako kwa nguvu.
Huu uzi umewaibua vibaka wengi sana.....

Watu wanaoghushi stakabadhi za malipo kwa waajiri wao hawawezi kuona ubaya wa jambo hili.....
 
Wengine wanawauzia wenzao Udongo,Chumvi na mafuta ili wawe matajiri kimiujiza!
Dah mkuu mbona umepoint penyewe? Yani sisi wagalatia sometimes bana tunamuabisha Yesu. Japo dini yetu ya kweli lakini mambo mengine tunazidiwa na wengine wasiojuwa kweli wako gizani.

Wagalatia wenzangu tubadilike asee tusiendeler kuingiza giza nuruni na kumuaibisha Yesu.

JESUS FIRST JESUS FOREVER

Nyau de adriz
 
Hawajachukua mali ya mtu bila idhini yake wenyewe wanakuja na hoja yao ni wewe sasa kuwapa au kutowapa,mbona watu wanapiga mahela huko ya kueleweka na hakuna mtu anakemea ila mnaangaika na mtu aliejipa kazi ya uchangishaji kweli
Samahani sana ndugu mdau, lakini mawazo kama haya ndio yanayofanya uozo kuendelea kuwepo kwenye jamii yetu
 
Samahani sana ndugu mdau, lakini mawazo kama haya ndio yanayofanya uozo kuendelea kuwepo kwenye jamii yetu
Hawa ndio wale wanaoghushi nyaraka za malipo kwa waajiri wao.....hawa ndio wale wanaoongeza bei za pindi watumwapo kununua BIDHAA na waajiri wao.... hawa ndio wale wanaoweka chajuu kwenye miradi ya serikali........sasa unategemea mtu kama huyo atakuja na wazo badala ya kuwashangaa wanaoshangaa matapeli wenzie
 
Kwani vijana hawarusiwi kujipongeza baada ya Kaz zito
 
Attachments

  • Screenshot_20240916-154459_1.jpg
    Screenshot_20240916-154459_1.jpg
    119.8 KB · Views: 2
Kuna wengine wanavaa jezi full wanaingia mtaani wanachangisha mchango ili Timu inunue mipira au Jezi
 
Hii haina haja ya kusalimiana,

Jana nikiwa kwenye harakati zangu za kutafuta mkate wangu wa kila siku kama ilivyo Ada kwa watu tuliombiwa tutakula kwa jasho. Niliibahatika kuingia kwenye jengo moja mitaa ya Masaki.

Wakati natoka kwenye hilo jengo nje nikakutana na kundi watu wanaoonekana ni MAUSTAADH wakiwa wamewazunguka walinzi wa jengo hilo na watu wengine wa karibu na hapo katika hali inayoonekana kama kuna mazungumzo ya kidini yanayoendelea.

Lakini kadri ninavyosogea karibu ndio naziona zile sura za wale MAUSTAADH. Sio sura ngeni ni vijana wa mtaani ninapoishi wapo kama wa nne lakini pia kwa ninavyo wafahamu sio watu wa dini bali ni hawa walevi hizi vipombe vikali huku kwenye maduka ya mtaani.

Wale MAUSTAADH baada ya kumalizana na pale wakaendelea na jambo lao mbele kwa mbele ndio nikasogea kuwauliza wale waliokuwa wakipatiwa ilimu na kuwauliza nini kilikuwa kinaendelea wakasema wale MAUSTAADH wanachangisha fedha za ujenzi wa msikiti na Madrasa maeneo ya Chalinze.

Kweli dunia inaelekea kubaya, nikafikiria kuwachoma lakini nikahofia usalama wao.
Utapeli upo wa wingi. Hudusan kwa mgongo wa imani za watu. Hilo halipingiki.

Unenikumbusha watu wanavyochapwa (tapeliwa) sijui na mchungaji gani yule na wazo la udongo aliloliona JF.

Kuna Bi Zainab Tamim hapa JF anautangaza udongo wake wa tiba na urembo wa ngozi kwa zaidi ya miaka kumi sasa hapa JF. Hakuna malalamiko.

Huyo mchungaji tapeli kayaona hayo JF sasa anawachapa wajinga ndiyo waliwao mitaani huko.
 
Hii haina haja ya kusalimiana,

Jana nikiwa kwenye harakati zangu za kutafuta mkate wangu wa kila siku kama ilivyo Ada kwa watu tuliombiwa tutakula kwa jasho. Niliibahatika kuingia kwenye jengo moja mitaa ya Masaki.

Wakati natoka kwenye hilo jengo nje nikakutana na kundi watu wanaoonekana ni MAUSTAADH wakiwa wamewazunguka walinzi wa jengo hilo na watu wengine wa karibu na hapo katika hali inayoonekana kama kuna mazungumzo ya kidini yanayoendelea.

Lakini kadri ninavyosogea karibu ndio naziona zile sura za wale MAUSTAADH. Sio sura ngeni ni vijana wa mtaani ninapoishi wapo kama wa nne lakini pia kwa ninavyo wafahamu sio watu wa dini bali ni hawa walevi hizi vipombe vikali huku kwenye maduka ya mtaani.

Wale MAUSTAADH baada ya kumalizana na pale wakaendelea na jambo lao mbele kwa mbele ndio nikasogea kuwauliza wale waliokuwa wakipatiwa ilimu na kuwauliza nini kilikuwa kinaendelea wakasema wale MAUSTAADH wanachangisha fedha za ujenzi wa msikiti na Madrasa maeneo ya Chalinze.

Kweli dunia inaelekea kubaya, nikafikiria kuwachoma lakini nikahofia usalama wao.
Dah!...mjini mipango.
 
Segerea mwisho kulikuwa kuna kundi kila Jumapili wanatembea na kanzu zao na makaratasi wakisema wanachangisha pesa za madrasa na kituo cha watoto yatima kilichopo Chanika.

Kuna mmoja wao kwa bahati nzuri ama mbaya alishanichangisha mara 2 tofauti hivyo nilimkariri sura. Na alikuwa na mfano wa kovu kubwa usoni kumfanya iwe rahisi kuweza kumkumbuka.

Siku moja nilikuwa maeneo ya Banana nikaona kundi kubwa wakiwa wamevaa fulana za sare ya kanisa (kutokana na maandishi ya kwenye fulana) wakizunguka na biblia zao kuomba msaada wa ujenzi wa kanisa na kituo cha watoto yatima kilichopo Pugu. Walipopita karibu yangu nikamkumbuka yule kijana wa Segerea akiwa mmoja katika hilo kundi.

Ilibidi nimsimamishe yule kijana na kumuuliza kama kabadili dini. Mwanzo alijifanya hanielewi ila nilipomkazia ikabidi awe mpole. Akasema bro kausha tunatafuta rizki tu.

Nilichogundua jamaa ni wasanii mno wa kucheza na akili za watu. Alipokuwa anaomba kama muislam na lafudhi pia aliiweka kiislam slamu na alipokuwa anachangisha kikristo, halkadhalika dialect aliiweka kikanisa kanisa.

Kiuhalisia hawana kanisa wala msikiti wanaoombea. Ni mradi wao tu, wanazunguka kukusanya pesa na mwisho wa siku wanaenda kunywea pombe.
 
Back
Top Bottom