Ndugu zangu wenye mioyo ya kutoa kuweni makini na wanaoonekana ombaomba mitaani, wengi wao matapeli na vibaka

Dah!! Watu hawana huruma na binadamu wenzao.....😂
 
Noma sana...
 
Nilivyosoma kichwa cha habari nikaona nisome nini kimewasibu ombaomba mana na mimi ni mdau wa kuwapa chochote kitu.

Hao uliowaona siyo ombaomba bali ni wachangishaji wa mchango kwa ajili ya jambo fulani mfano ujenzi wa taasis nk.

Ombaomba ni wale ambao wanaomba kwa ajili ya maisha binafsi.

Turudi kwenye hoja.

Ukimuona mtu mzee sana au mlemavu wa viungo anaombaomba, wewe kama unacho mpe tu, kama hauna mwambie sina.

Wazee na walemavu wanahitaji msaada sana mana hawana namna ya kujikwamua. Hivi mzee sana anaweza kinyenyua zege?

Usianze kusema; "mara ooo! huyu mlemavu ombaomba ana mjengo kutokana na kazi hii"

Hiyo ndio kazi yake! Kama unacho mpe, kama hauna mwambie sina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…