Ndugu zetu CHADEMA kukosa Ubunge sio sababu ya kuichukia nchi yenu

Ndugu zetu CHADEMA kukosa Ubunge sio sababu ya kuichukia nchi yenu

Duniani hakuna mtu anaweza ichukia Nchi yake, ila serikali sawa, hata waasi uipenda Nchi yao ila huwa wanaasi serikali, na chanzo mara nyingi ni uonevu, kukosa haki na kuto sikiliza malalamiko na kufanyia kazi.
Kwa hiyo tofautisha serikali na Nchi, na mtu anatakiwa awe mzalendo kwa Nchi yake na kuheshimu serikali halali!
 
Una hakika na unachokiongea au ushabiki unakusumbua? Mbinu aliyotumia kuondoka "mashetani watu" waliokuwa wamemkamia kawaachia "manyoya",hawaamini na wametahayari.Yule hakimu waliyemwongezea muda ili akamilishe "mpango mkakati" haramu kabaki na lundo la makaratasi! Kifupi "they are dumb founded"

Muulize Kamanda Ziro alivyowasihi warudi eti atawapa ulinzi baada ya njama zao kuwa kituko.
Wewe ndo hujui unachokiongea, Jamhuri ikikuhitaji haiwezi kukukosa, na infact hakuna mbinu yeyote aliyotumia kuondoka, alikuwa anawapumbaza tu nyie vilaza msiojua vitu ila kaa ufahamu ratiba yake hiyo ya kuondoka ilishakuwepo muda mrefu sema alikuwa anatafuta mbinu ipi atatumia kuondokea.
 
Mnaipaka matope nchi yenu mnasema eti ni nchi isiyothamini wawekezaji je hii ni kweli?

Mmechukia kutopata Ubunge je kwani Ubunge ni ajira? Hapana.

Kwa muktadha huu ni kuwa watanzania wameridhika na CCM.

Sasa mnataka nini? Mnaeneza uongo hapa Jf kuwa wawekezaji wanadhulumiwa bil of Tsh, jambo ambalo sio. Mlishapoteza kuweni wapole na mjipange kwenda kulima ndizi huko Hai.
Wewe unambusu mtu anayekupora haki yako?
 
Una upeo mdogo, jaribu kuelewa indirect language ambayo nimeitumia, kama nchi haifuati mfumo wa sheria na katiba, basi kuna sheria za kimataifa, mikatama, pamoja na makubaliano ambayo yataibana nchi husika

Kamwambie na Jiwe hatuhami ila hatutanyamaza
Kutonyamaza na kuendelea na harakati za kuleta haki na usawa TZ ni haki na wajibu wako kama Mtanzania. Na mimi nautambua mchango mkubwa wa upinzani, maana bila upinzani CCM ilikuwa imepoteza dira. Nchi ilikuwa imechukuliwa na matajiri, wezi, na wauza unga, kwa kifupi na wenyenazo. Baada ya kazi nzuri ya upinzani (ingawaje hawakupata uongozi wa nchi), CCM ilishtuka na kujikuta mahala pabaya. Hata Magufuli mwenyewe alipata nafasi ya uraisi baada ya taharuki na kutoelewana kwa "inner circle" ya CCM. Walipakana madongo, wakachafuana, na hatimaye kutmuana. HGiyop ndiyo ilikuwa ngekewa ya Magufuli. Magufuli alipata uraisi bila kuwa na deni la kulipa, si kwa wala rushwa, si kwa wauza unga, na wala si kwa matajiri. Ndiyo maana alipoingia madarakani, alikuwa mtu huru mwenye maamuzi huru na hakutegemea kurudisha/kulipa chochote maana uongozi aliupata kwa kura na si kwa kusaidiwa na mtu. Paingekuwa na ugomvi kwenye inner circle ya CCM Magufuli hata uwaziri mkuu asingepata.

Upinzani nao sasa wameanza kupoteza kwa wananchi. Badala ya kuendelea na harakati za kuwaonyesha Watanzania uovu wa CCM na ni kwa nini bado wana nafasi ya kuleta maendeleo, wameanza kustaki kwa mama au baba eti kaka kanifinya au kanipiga. Wameanza kuiita au kuilinganisha CCM na makaburu. Tatizio la kuwaita CCM makaburu ni kuwa watru wataangalia ni yupi kaburu halisi yule anayesema CCM ni kaburu au yule anayekimbilia kwa wazungu kuishtaki TZ. Tuseme, kwa mfano upinzani unafanikiwa kukatisha misaada na TZ tunapata shida, huoni hapo CCM itawashtaki kwa wananchi jinsi mlivyoihujumu nchi.

Chaguzi katika nchi nyingi zimedhihirisha kusema ni rahisi kuliko kutenda. Hata upinzani wanajuwa kuwa wakipata (na kuna siku watapata) hawataenesha nchi jinsi wanavyodhania. Watakapokumbwa na shida za watu na kushindwa kuzitatua kwa sababu uwezo haupo, ndiyo wataona ugumu wa kutawala. Siasa siku zote ni mbinu na waklati mwingine mbinu chafu. Leo wewe ni mzuri, kwa sababu umefanya jambo jema, lakini kesho unaweza kujikuta unachukiwa na wengi. Nafikiri kila mtu alikuwa anadhani demokrasia imekomaa Marekani, lakini ukweli enzi hizi za utandawazi, demokrasia iko mashakani USA. Wote mnajuwaq kuwa USA kuna nvyama vikubwa viwili na kila siku wanatafuatiana mbinu za kuongoza nchi. Najuwa watu wengi (wa nje) wanakipenda chama cha democratics. Lakini mnaojuwa historia chama kilicholeta mapinduzi makubwa USA na kufutilia mbali utumwa ni Republicans. Republicans ndiyo walipigana na kusini ili kuinusuru Marekani isisambaratike. Mizozo mingi ya ubaguzi wa rangi iliyopo kusini ilitokana na democrats.

States zza kusini ziliwachukia saana republicans na ilikuwa si rahisi republican kupata uongozi kusini. Baadaye, democrats walitafuta mbinu za kuingia kaskazini. Ili kufanya hivyo ilibidi wawe na agenda zinazoendana na watu wa kaskazini. Democrats walianza kutetea na kuweka sheria zilizowapa watu weusi uhuru wa kweli. Hii iliwafanya waanze kupendwa kaskazini. Republicans kuona hivyo wakaanza kuwatetea watu wa kusini, utamaduini wao, na pia kuwa upande wao. Kilichotokea, ni historia. Kusini yote sasa iko chini ya republicans na republicans ina mvuto kwa wazungu. Laikini pia hii haitakuwa maisha, kwa sababu katika miaka 50 minority wa sasa watakuwa majority na kuwa na nguvu za kura.

Tanzania pia inatakiwa tujuwe ukweli kuwa vyama vya siasa ili kupata uongozi ni lazima kuangalia mwenzangu anateleza wapi, na tunaweza kutumia vipi kuteleza huko. CHADEMA/Upinzani ulikuwa umeona upenyo. Matatizo ya uongozi, madawa ya kulevya, matajiri kuwa juu ya serekali, watumishi kuacha kutoa huduma nzuri yalitumiwa vizuri na upinzani na kwa mara ya kwanza wakapata wabunge wengi. Lakini Magufuli alipopata uongozi, aliiona nguvu ya upinzanio iko wapi, na hapo ndiyo alianzia, hiyo ilikuwa ni political preemptive strike. Alianza kazi kwa kushughulikia matatizo na malalamiko ya upinzani. Alianzia zile kero kubwa, matokeo yake upinzani ukkanza kupwaya maana turufu yao ilichukuliwa na Magufuli. Sasa hivi upinzani unatakiwa uanze upya, lakini kufanya hivyo, kwanza unatakiwa kuwa na viongozi makini na pia wagombea makini. Kwa mfano mtu ukichaguliwa kupreperusha bendera ya chama chako inabidi ujikite kwenye kuonyesha jinsi utakavyofanya kazio kutatua kero za wananchi. Wakati wa kuomba kura siyo wakati wa kuishtaki CCM kwa wanachi, maana kufanya hivyo unaonyesha unyionge wako, na kama wewe ni mnyonge utawasaidiaje wanyonge?
 
Back
Top Bottom