'Ndugu Zetu' Yanga SC Hili Ni Ombi Langu Kwenu.

'Ndugu Zetu' Yanga SC Hili Ni Ombi Langu Kwenu.

Klabu ni za wanachama, hivyo unataka atokee mjomba kuendesha timu? Kumbuka kabla ya akina gulamali na azim timu zilikuwa zinaendeshwaje? Kama siyo ada za wanachama.
Mkuu.. Kwa idadi ya wanachama klabu hizi ilizonazo.. Na kwa tabia ya wanachama kulipa ada pindi uchaguzi unavyokaribia.. Na ikumbukwe wengi wanaopiga kura ni wale wanaokaa dar.. Sasa kuna kitu hapo mnategemea kupata?
 
Simba ni bingwa mtetezi wa KOMBE LA FA lipi hilo ...mtibwa awe mtetezi wa KOMBE lipi!!?? Hakika simba ni mambumbumbu
 
Mimi niliwaza sana jana, nikasema hivi Mo hawezi kuwasaidia ndugu zetu Yanga hata Milioni mia tisa angalau wapate hata kununua Luku pale jangwani, kulipia Dawasco na other expenses? Lakini pia awalipe malimbikizo wachezaji ambao mpaka sasa hawajalipwa mishahara yao? Hebu mkuu Sembo unifikishie ombi langu hili kwa Dewji
 
Baada ya mechi ya 30/09/2018 ambapo Simba SC alitawala kila kona, isipokua mambo ya ulozi, mapato yaliyopatikana yalikua zaidi ya milioni 400. Katika fungu hilo, Bingwa mtetezi wa TPL na FA, Simba SC alipata zaidi ya milioni 190 huku Ndala wakipata milioni 0.

Sasa;
1. Kwakua 'ndugu zetu' Ndala mna hali ngumu sana ya kiuchumi.. Na kuhusu hili Tanzania inajua.. Africa inajua.. na Dunia inajua.
2. Kwakua sisi Simba SC tumejaariwa roho ya huruma na fedha tunayo (Si tunayo tu bali ni yakutosha).
3. Kwakua hatutaki 'ndugu zetu' mfutike katika ramani ya soka.

Ombi langu kwenu 'ndugu zetu' Ndala mnaonaje mkaomba mechi ya kirafiki nasi katika kipindi hiki cha mapumziko ya mechi za kimataifa.
Katika mechi hiyo, sisi mabingwa watetezi wa TPL na FA tutajaza uwanja wote, alafu mapato yote tutawaachia mhangaike nayo.

Huu utakua mchango mkubwa sana toka kwetu, kuja kwenu 'ndugu zetu' katika kipindi hiki kigumu mnachopitia.
'Ndugu zetu' Ndala, udugu si kufanana bali ni kufaana. Na sisi Simba SC tumeamua kuwasaidia.

Nawasilisha.
Level ya kucheza na Yanga iko hapo chini
 

Attachments

  • IMG_20181007_165242.jpg
    IMG_20181007_165242.jpg
    50.8 KB · Views: 17
Back
Top Bottom