Ndugulile: Tozo za Daraja la Kigamboni zipunguzwe kurahisisha maisha

Kama hazipotei, tozo ni nzuri. Anadhani ni rahisi yeye kulipwa m12 bila wengine kuumia?
 
Mtakoma mnaoishi huko pumbavu sana,hata kama mzazi angekuwa huko ningemwambia koma. Maana mlimshukuru xana kwakupiga makofi n'a vicheko.
Pesa za watz wenzenu zipo hapo,mifuko y'a hifadhi iliunganishwa ili kufuta ushahidi wa madai.
lipeni hela hizo. hakuna CHA NYOOO
 
Huyu Mbunge nae hamna kitu kabisa, issue sio daladala..ni kwamba daraja la Kigamboni ni Huduma kama Huduma nyingine wananchi wanatakiwa kupita Bure kabisa maana nao wanalipa kodi kama wananchi wengine...kwa nini wananchi wa kusini hawalipi kuvuka daraja la Mkapa? Kule Mwanza wanajenga daraja kubwa na la gharama kubwa kuliko yote, je wananchi watalipishwa kuvuka? Wamejenga daraja la baharini hapo Aghakhan kuunganisha na masaki kwa matajiri je hao matajiri watalitumia kwa kulipia kama wananchi wa kigamboni? Yes, tunajua daraja la Kigamboni limejengwa kwa PPP na nssf wanatakiwa warudishe gharama zao lakini hatuambiwi kwa miaka mitano iliyopita wamekusanya kiasi gani na wataendelea kukusanya mpaka lini
 
Wananchi wa Kigamboni wanashukuru sana kwa ujenzi wa Daraja la Nyerere. Ni mkombozi mkubwa. Changamoto ni tozo. Daladala moja inatozwa Sh5,000 ikienda mara kumi kwenda na kurudi ni Sh100,000 kwa siku. Hapo hajaweka mafuta, hajaweka hela ya tajiri-@DocFaustine

“Nakuomba sana Rais twende tukaliangalie jambo hili. tuangalie jinsi gani tunaweza kuleta nafuu kwa wananchi wa Kigamboni na kufanya maisha yawe mepesi. Wananchi wamenituma hilo niweze kulifikisha kwako,” amesema Ndugulile wakati Rais
@SuluhuSamia aliposimama Kibada, kusalimia.
Yuko sahihi. Wangewapangia tozo za siku, za wiki na za mwezi. Kwa siku mathlani 30000 kwa wiki 150000 na kwa mwezi 500000. Wangepata pesa nyingi bila usumbufu wa kulipia kila hivyo. Hivyo hivyo kwa vyombo vingine vya moto. Watu waweze kulipia kwa muda mrefu kwa bei nafuu.

Amandla...
 
Si kupunguza bali wafute kabisa, hilo deni lishukuliwe na Serikali, haiwezekani daraja moja tu ndilo lilipiwe nchini wakati mengine yote watu wanapita bure, kwani watu wa kigamboni wamekosea nini.
 
Wananchi wa Kigamboni wanashukuru sana kwa ujenzi wa Daraja la Nyerere. Ni mkombozi mkubwa. Changamoto ni tozo. Daladala moja inatozwa Sh5,000 ikienda mara kumi kwenda na kurudi ni Sh100,000 kwa siku. Hapo hajaweka mafuta, hajaweka hela ya tajiri-@DocFaustine

“Nakuomba sana Rais twende tukaliangalie jambo hili. tuangalie jinsi gani tunaweza kuleta nafuu kwa wananchi wa Kigamboni na kufanya maisha yawe mepesi. Wananchi wamenituma hilo niweze kulifikisha kwako,” amesema Ndugulile wakati Rais
@SuluhuSamia aliposimama Kibada, kusalimia.
Rais kasema watalifanyia Kazi haraka.kwa sababu Kigamboni itakuwa eneo la viwanda.
 
Hili daraja limejengwa kwa bei ya kifisadi kutumia mfuko wa NSSF...wizara ya ujenzi chini ya Magufuli walipinga sana gharama hizo lakini mwisho wake Rais Kikwete alimpelekaMagufuli wizara ya vitoweo na katibu mkuu wake Mhandisi Kijazi akapelekwa ubalozi India..daraja likajengwa ...mpaka leo huo mzigo unalipwa na watanzania.
Kwa hiyo tunalipia daraja pamoja na ganji za waheshimiwa sana humo sio?
 
Kama madereva wa daladala wanalalamika kulipia hiyo 5000 basi waruhusiwe kupandisha nauli, raia atakayeona ni gharama apige mbizi...hakuna huruma, hizi kauli za wananchi wanyonge ndio zinachelewesha maendeleo, Tozo ni muhimu kwa ujenzi wa taifa!

Ndio maana bei ya daladala kwa route ya kigamboni iliwekewa ongezeko la shilingi 50 na nauli yao ni 450 au 550 kama sijakosea kariakoo kigamboni
 
Sisi wenye akili tunajua mradi wa kigamboni umegeuzwa miliki ya watu binafsi ndiyo maana wanakataza hata kupiga picha pesa zinapigwa 70% inakwenda mifukoni mwa watu furani 30% ndiyo inayo kwenda panapo stahili
 
Yaani unafuu wa maisha uletwe kwa kupunguza tozo hiyo ya daladala?hiyo 5000 si ni kama gharama ya lita 2 tu tu za mafuta?wakizungukia kongowe ni zaidi ya hizo lita 2, kwa hiyo hesabu iko pale pale tu, wanashindwa kupigia kelele vitu vya msingi eti tozo ya daladala/magari madogo!!
Soma kwanza uelewe siyo unakurupuka kama umepigwa finger 5000 kila ikipita hiyo ikifanya safari 20 ni 5000 x 20 = 100000 kwa siku mola
 
Daaaa!!wewe ndio umekurupuka kujibu bila kuelewa, hiyo 5000, ya tozo ya kuvukia hapo, kwa mala moja, ni sawa na lita 2 za diesel, sasa kama ana ona ni gharama sana, hilo daladala litoke machinga complex lipitie mbagala kwenda kigamboni alinganishe mafuta atakayotumia kuzungukia kule na hiyo tozo ya hapo!!kwanini hata wenye magari binafsi wanakimbilia kupitia hapo?kulinganisha na kuzungukia mbagala?!!sasa kwa akili yako unafikiria hizo tata kwa siku nzima wanatumia mafuta kiasi gani hadi uone hiyo laki 1, ya kulipia daraja ni kubwa sana?kwani akishamaliza tu daraja ni tayari amefika stendi ya feri, haya , na nauli yake ni kubwa kulinganisha na umbali uliopo hapo, kwani hiyo tozo wakati wanaiweka waliingiza kwenye nauli kabisa , na ndio maana kigamboni na kariakoo hapana umbali sana kulinganisha na nauli hiyo, angalia umbali uliopo toka mbagala hadi kawe na nauli, yake, au kariakoo hadi kisemvule!!SHAME ON U!!
 
Kama madereva wa daladala wanalalamika kulipia hiyo 5000 basi waruhusiwe kupandisha nauli, raia atakayeona ni gharama apige mbizi...hakuna huruma, hizi kauli za wananchi wanyonge ndio zinachelewesha maendeleo, Tozo ni muhimu kwa ujenzi wa taifa!
Wewe bila shaka ni mmoja wa makarani wanaokusanya tozo, ni mmoja wwanufaika wa tozo hizo.
 
Daaaa!!wewe ndio umekurupuka kujibu bila kuelewa, hiyo 5000, ya tozo ya kuvukia hapo, kwa mala moja, ni sawa na lita 2 za diesel, sasa kama ana ona ni gharama sana, hilo daladala litoke machinga complex lipitie mbagala kwenda kigamboni alinganishe mafuta atakayotumia kuzungukia kule na hiyo tozo ya hapo!!kwanini hata wenye magari binafsi wanakimbilia kupitia hapo?kulinganisha na kuzungukia mbagala?!!sasa kwa akili yako unafikiria hizo tata kwa siku nzima wanatumia mafuta kiasi gani hadi uone hiyo laki 1, ya kulipia daraja ni kubwa sana?kwani akishamaliza tu daraja ni tayari amefika stendi ya feri, haya , na nauli yake ni kubwa kulinganisha na umbali uliopo hapo, kwani hiyo tozo wakati wanaiweka waliingiza kwenye nauli kabisa , na ndio maana kigamboni na kariakoo hapana umbali sana kulinganisha na nauli hiyo, angalia umbali uliopo toka mbagala hadi kawe na nauli, yake, au kariakoo hadi kisemvule!!SHAME ON U!!
Hivi hiyo picha uliyo weka hapo kwenye avata yako siyo lile jizi na fisadi kuu [emoji849][emoji849]ndiyo maana unaunga mkono mambo ya kihuni ya kifisadi bila ya akili
 
Mkuu!!huyo ni koffi anan, mwafrika wa kwanza kuwa katibu mkuu wa UN, mwenye busara mingi kuliko hata wazungu!!!hilo suala la daraja huyo ndungulile anatafuta kiki tu hana lolote, kwani kipindi kile linaanza na SUMATRA, kuanzisha route hiyo yote hayo yaliwekwa kwenye calculations za nauli, ndio maana nauli ya kutoka machinga complex hadi kigamboni ni kubwa kulinganisha na umbali uliopo hapo!!tozo ina miaka karibia 5 leo ndio unaona inatesa , tena matajiri wenye magari?!
 
Wananchi wa Kigamboni wanashukuru sana kwa ujenzi wa Daraja la Nyerere. Ni mkombozi mkubwa. Changamoto ni tozo. Daladala moja inatozwa Sh5,000 ikienda mara kumi kwenda na kurudi ni Sh100,000 kwa siku. Hapo hajaweka mafuta, hajaweka hela ya tajiri-@DocFaustine

“Nakuomba sana Rais twende tukaliangalie jambo hili. tuangalie jinsi gani tunaweza kuleta nafuu kwa wananchi wa Kigamboni na kufanya maisha yawe mepesi. Wananchi wamenituma hilo niweze kulifikisha kwako,” amesema Ndugulile wakati Rais
@SuluhuSamia aliposimama Kibada, kusalimia.
sidhani kama daladala lenye hesabu ya 100,000/= kwa tajiri linaweza kuzalisha 100,000/= ya ziada ya kuvuka daraja

kwa hiyo kabla ya kutumika daraja stuff ya daladala (dereva konda ) walikuwa wanakula laki moja ya ziada kwa siku ????

please....basi kila mtu angeenda kuwa konda na dereva wa dala dala
 
Back
Top Bottom