Mchungaji naona umekuwa mkali kweli kweli bila kutueleza kilichokufanya utake hao akina knuckleheads wawe fired!
Naam Ndulu nilidhani ana msimamo wa maana baada ya madudu yaliyotokea Benki kuu lakini kumbe na yeye ni kichwa mbovu tu! Haingii akilini kwa kiongozi iwe wa Serikali ama Shirika atake kumiliki nyumba ya kifahari kwa kutumia fedha za wavuja jasho! Ama kweli Watanzania wanaonewa na kuoneana!
Nakubaliana nawe, kwa ubadhilifu uliotokea BOT wa kutumia bilioni za fedha kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja tu Board nzima inastahili kujiuzulu na kutakiwa warejeshe fedha walizoacha zikatumiwa isivyo halali. Mkulo angeliweza kujijengea jina kukemea vitendo vya ubadhilifu kama hivyo. Hayo yako ndani ya uwezo wake kama Waziri muhusika.