Mdondoaji,
..pamoja na Gavana kuwa mwenyekiti wa bodi kuna wajumbe wengine 4 au 5 wanaoteuliwa na waziri wa fedha. wajumbe hao wana haki ya kupiga kura ikiwa jambo lolote lile litashindwa kupita by concensus.
..pia wapo makatibu wakuu wa hazina ya muungano na ya zanzibar ambao wanaingia kwenye vikao kutokana na dhamana zao. hawa hawana haki ya kupiga kura.
..katika mazingira kama hayo naamini bado Gavana anaweza kuwa challenged humo ndani ya bodi kwasababu hana mamlaka ya kuteuwa board members. anayo mamlaka ya kumchagua makamu mwenyekiti toka manaibu gavana ambao wanateuliwa na Raisi kama yeye gavana.
..sidhani kama Gavana ana nguvu kubwa kiasi hicho. kitu cha kujiuliza ni kwamba ujasiri wa kufanya madudu yote hayo unatoka wapi? na huyu siyo gavana wa kwanza kufanya madudu.
Fundi Mchundo,
..nakubaliana na mawazo yako kwa kiasi kikubwa.
..lakini ili tufanikiwe inabidi tuchague wananchi ambao wana mawazo kama yako waende bungeni wabadilishe sheria zetu.