mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema Tume hiyo haijapokea taarifa za uwepo wa kura feki katika majimbo ya Kawe, Pangani na Kigoma.
Amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika muda huu mchache uliobaki.
Jaji Kaijage amesema ''Kuna taarifa kuwepo masanduku ya kura feki katika Jimbo la Buhigwe, Kawe na Pangani, taarifa hizo hazijathibitishwa na hazijawasilishwa rasmi tume. NEC inataka wananchi wapuuze taarifa hizo kwa kuwa hazijathibitishwa"
Amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika muda huu mchache uliobaki.