NEC igeni Mfano wa IEBC ya Kenya

NEC igeni Mfano wa IEBC ya Kenya

Kwa taarifa yako, vyombo vya habari vilisitisha kutangaza matokeo siku tatu kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa. Kwa hiyo pointi yako haina uzito, hasa ukijua ni kwa nini walisitisha.
Lakini walitangaza japo kdgo
 
Tume hii hii ambayo ndani ilikuwa na magenge yaliyolanguliwa na kila upande?????

Hapo labda tume yetu ikaongeze uhuni tu hakuna la maana la kujifunza.
 
Tarehe 09.08.2022 taifa la Kenya lilifanya uchaguzi mkuu ili kupata viongozi mbalimbali wa taifa hilo.

Upigaji kura ulifanyika vizuri kwa amani kwa mujibu wa waangalizi wa Kimataifa, kwa muktadha huo naipongeza IEBC yenyewe, serikali na police wa Kenya kwa kutekeleza majukumu yao vizuri.

Jambo muhimu NEC ya Tanzania inalopaswa kujifunza kutoka IEBC ya Kenya ni kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki. Huko Kenya tangu mwanzo hakuna Cha mgombea kutekwa akapoteza form na hapakuwa na mgombea yeyote aliyepita bila kupingwa hili NEC walichukue.

Jambo jingine ni uwazi wakati wa kutangaza matokeo, NEC iige kuruhusu vyombo vya habari kama ilivyotokea kwa wenzetu huko Kenya, vyombo vya habari viliruhusiwa kutangaza idadi za kura alizopata mgombea wa nafasi fulani katika jimbo fulani.

Hii Itasaidia viongozi wote wenye mamlaka kuogopa kuingilia tume ya Uchaguzi kwani jamii itakuwa inajua idadi ya kura mgombea fulani alizopata katika jimbo fulani hivyo sio rahisi kuzigeuza kuzibadili kura.

Police wa Tanzania wakati wa uchaguzi wawe walinda amani na mali za watu wasigeuke kuwa wapiga kampeni wa viongozi wa Chama kilichopo madarakani.

Mwisho NEC wanapaswa wasiwe waoga wasimamie haki, aliyeshinda atangazwe na aliyeshindwa asitangazwe.
Tatizo ni kuwa NEC siyo huru..
Wizi, hila, uhalifu na uchakachuaji unaotekelezwa na NEC huwa ni maelekezo kutoka juu
 
Nina wasiwasi kama kweli hii tume ilikuwa huru. Mwenyekiti wa tume Chibukati kabla ya kutangaza matokeo kulikuwa na mikiki mingi. Kati ya wajumbe 7 zaidi ya nusu hawakukubaliana na hayo matokeo kwa sababu ya irregularities lakini akaamua kutangaza bila makubaliano na wenzake ambao ndo wengi include makamu wake. Kwa maana hiyo hiyo tume pia ilishaingiliwa na haikuwa huru. Lakini nami niwasifu kwa uwazi walioonyesha lakini nadhani kulikuwa na shida kwenye verification ndo maana kuna Afisa mmoja mpaka sasa hajulikani alipo.

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: F4B
Raila sijui ana hali gani hapo alipo!
Kenya hawatakagi ujinga !
 
Tume hii hii ambayo ndani ilikuwa na magenge yaliyolanguliwa na kila upande?????

Hapo labda tume yetu ikaongeze uhuni tu hakuna la maana la kujifunza.
La kujifunza ni kwamba hata chama ambacho hakipo madarakani mgombea wake wa URais akishinda atangazwe kwamba ameshinda !!
 
Back
Top Bottom