Uchaguzi 2020 NEC isipomuengua Tundu Lissu, ni go-ahead ya kuipoteza CCM Zanzibar. Je, Muungano utasalimika?

Sijui huwa mnakwama wapi....yaani chama tawala kikongwe kishindwe uchaguzi hapa Africa?...kama ndiyo mimi rais ningeivunja hiyo tume ya uchaguzi....swali rahisi...Hivi Lissu akichukua nchi niambie kama ana timu ya kuongoza nchi.....nani waziri mkuu? nani spika?etc mi sina chama lakini sipatani na haya mambo ya mkumbo na jazba
 
wali kubwa linalopiga kichwa changu ni je, usalama wa Muungano upo kwa kiasi gani mara tuu CCM itakapofungasha virago huko Zanzibar? Kwa jicho langu, naona muungano hautabaki salama.

Ama hili la Muungano ni wewe unasema tu kuwa hautakuwa Salama.
Yaani unataka kutuaminisha kuwa CCM ndio Muungano Na Muungano ni CCM? bila ya wao hakuna Muungano?

Mimi naona si vyo hivyo bali Muungano ni jambo la kikatiba.
Maalim Sefu hatoweza kuvunja katiba kirahisi hiivyo.
Nenda kawadanganye CCM wenzako vijijini uwongo wako huu.
Kuhusu Lisu na Maalim kuusemea Muungano kuwa ni Ukoloni , hii ni CCM ndiyo wanvyougeuza Muungano kinyume na Ktiba.
Kwa kuwa CCM huwa hawafuati katiba wala Sheria.

Nifuatilie kwa makini nitakuweka sawa.
 
Kwani kabla ya mungano siilikua Zanzibar IPO na Tanganyika ipo na watu walikua wakifanya shuhuli zao kwa nafasi
 


Mkuu utanielewa uchaguzi ukimalizika. Kwa sasa tubaki watazamaji
 
E imekua zanzibar Tena sio Bara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Nani huteuwa watumishi wa NEC
 
Katiba ilisema wazi tokea miaka ya 80 baada ya Zanzibar kulalamika kuhusu mapato ya pamoja ya Muungano na matumizi yake na Mgao wa mapato kwa pande mbili za Muungano pawepo na Account ya pamoja ya fedha za Muungano.
Hadi leo hii serikali za CCM hazija tekeleza Takwa hilila katiba, na kwa hiyo Zanzibar inaendelea kudhulumiwa Stahiki yake katika Muungano.

labda nadhani Pesa hizo zinapenyezwa Kisiwandui na wanazitumia CCM kichama ndio maana SMZ imenyamaza kimyaaaaa haiendelea kulidai hilo.

Niwazi kwa hili serikali ya Malim sefu Haitalinyamazia ,na itaitaka Tanganyika iilipe zanzibar malimikizo ya Tokea siku ya Kuanzishwa Muungano kitu ambacho Tanganyika haitaweza na kwa Hili latosha kuuweka Muungano kikaangoni.

Maana Moyo wa nchi ni mapato.
-Tanganyika watajitowa kwenye Muungano ili kukimbia deni walilotudhulumu tokea tuunganishe nchi zetu.
-wengi hudhani kuwa Zanzibar hawana haki katika hili la fedha za Muungano.
hebu tafakari hivi.!:-
- Viza zote za watalii zitolewazo malipo yanakwenda Muungano.
ambapo 1/3
ya watalii hutembelea Zanzibar.
-Bidhaa zote zinazoingizwa nchinihutolewa VAT ka kodi nyingine Muungano kudhibitimapato.
-Mashirika ya simu yote huilipa serikali kwa kusajiliwa na kupokea kodi za wateja na huduma.
- Zanzibar tukiwa sehemu ya wateja na wahusika wakubwa wa mapato kama washirika wa Muungano.
Gawio la mapato haya ni lazima liwe wazina kila upande ujuwe quarter yake.
sas serikali za CCm wamezira juu ya hili na Zanzibar inaendelea kudidimia kiuchumi.

Maalim Sefu hatakubali hilo atadadisi na pakikosekana majibu stahiki Tanganyika watakimbia ukweli na wata sepa kwenye Muungano.

Zanziba Tunauhitaji sana Mungano, lakini si kwa mfumo huu.

Kule UAE kuna muungano mzuri tuu na kila upande unahaki zake na uchumi wake na kuna mambo ya pamoja wanashirikiana kigharama na uendeshaji kwa kuwa kuna ukweli na GOOD WILL

Muungano unahitaji GOOD WILL na si ubabaishaji kama huuwa CCm.

Ikiwi umenielewa ndo maana Muungano unaweza kuwa hatarini.
 
..wasichotaka waZnz ni uchaguzi wao kuporwa na waTanganyika.

..Tanganyika imekuwa ikisimika serikali ya Znz kinyume na matokeo ya sanduku la kura, na matakwa ya waZnz.

..sasa matendo hayo ya Tanganyika ndiyo yanayochochea hoja kwamba Zanzibar inatawaliwa, au ni koloni la Tanganyika.

..ikiwa ACT itashinda uchaguzi Znz kitakachobadilika ni MUUNDO WA MUUNGANO, na utakwenda kuwa wa serikali 3.

..Tume ya Katiba ya Jaji Warioba ilikutanisha watu wa mitizamo mbalimbali, ikiwemo waZnz waliokuwa wakitaka kujitenga na Tanganyika, lakini walipoangalia hali halisi ya maingiliano ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi, baina ya mataifa yetu, walifikia conclusion kwamba muungano wa SERIKALI 3 ndio unaofaa.

NB:

..kuna masuala ya EAST AFRICAN COMMUNITY ambayo wengi hatuyafuatilii, lakini moja ya malengo ya jumuiya hiyo ni kuziunganisha nchi wanachama kisiasa. Sasa muungano wa serikali 3 baina ya Tanganyika na Zanzibar utasaidia kufikia azma na malengo ya kuwa na muungano mkubwa zaidi wa nchi za Afrika Mashariki.
 
Chadema ni chama cha mioyo ya watz wkt ccm ni chama cha mioyo ya polisi, NEC na msajili wa vyama
 
NEC haiwezi Kumwondoa mgombea wa CCM kwa sababu ndiye mtu aliyeitengeneza hiyo NEC na hapo ule usemi wa NEC ni vibaraka wa CCM ndipo unapokamilika
Hivikwanini NEC isimuengua mgombea wa CCM!?

Kwa kufanya kampeni miaka 5 kabla ya wakati, kunyamazia risasi 38 alizopigwa mbunge hadharani n.k?
 
Forex traders make it sound like they the only ones making money and we are just playing around. What I've realised is that most of them make more money teaching people how to trade than actually trading themselves.
 
Ilikuwaje kipenzi cha wangonge/wapumbavu akapata kura lukuki kiasi hicho ?
 
..mtoa mada hebu soma heading ya uzi wako tena.

..unazungumzia "kuipoteza Zanzibar."

..Je, inamaanisha Znz imekuwa "mali" ya watu/kikundi/dola/taifa fulani?

..Huyo ambaye Znz ni "mali" au "miliki" yake, na kuna hatari ataipoteza, ni nani?

cc Rubawa
 
Lissu atashinda kwa zaidi ya 70% , tumefanya utafiti kwa siku 45 , kabla na baada ya Lissu kurudi , sasa hiyo hesabu yako ya 40 /50 % haina uhalali
 
au unataka tuweke namba za cyprian Musiba na Le mutuz madalali wa siasa watesi wakubwa wanaotafuna pesa za umma kwa njia haramu kwa kisingizio kuwa wanaisaidia CCM kutokomeza chadema na kurejesha mfumo wa chama kimoja.
kuuwa upinzani sio rahisi kama kufanya ngono,upinzani unaunderground wengi sana vichwa subiri bunge lijalo
 
hatuwezi shinadana na wakati ikifika waznz wanautaka uhuru wao wapewe kama ni muungano wataamua ni aina gani ya muungano kama ni wa kiuchumi,kisiasa au kijamii sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…