Uchaguzi 2020 NEC: Kila Chama cha Siasa kimeruhusiwa kuweka wakala kwenye kila kituo ili kulinda maslahi ya Chama na Wagombea

Uchaguzi 2020 NEC: Kila Chama cha Siasa kimeruhusiwa kuweka wakala kwenye kila kituo ili kulinda maslahi ya Chama na Wagombea

Hawa ni kuwa nao makini. Mawakala wataenguliwa na kuwekwa mawakala feki. Hivi kama nchi nzima wameunguliwa wagombea wa chadema pekee na hakuna wa ccm aliyeenguliwa hata mmoja bado tunatarajia hii tume ifanye haki?
Hapa hakuna uchaguzi ni uchafuzi tu. Ila ipo siku itafika kwa sababu taratibu naona tunasogea hapo
Labda uwe na wasiwasi na mawakala wenu juu ya swala zima la njaa.
 
Umeelewa nini kwenye phrase 'kimeruhusiwa'?
Sikutaka kuizingatia phrase ya mleta mada, nimezingatia maelezo yako kwamba "huwa ni utaratibu mawakala kuwepo",jambo ambalo ndio ukweli wenyewe, hivyo sikupingi kumkosoa mleta mada.
Swali langu ni, kwanini baadhi ya vyama hulalamika kuibiwa Kura baada ya uchaguzi, licha ya kuwepo kwa Hawa watu?
 
Kuweka is not an issue ila ni wale masimamizi wa NEC katika majimbo ambao si wafanyakazi huru wa Tume bali mawakala wa CCM, jinsi watakavyo leta vigisu wakati wa kuwaapisha na kuwaruhusu mawakala katika vituo vya kupigia kura ili tu chama fulani kifanye uovu wake katika kubaka demokrasia
 
sio kazi ya wanachama kulinda kura.

kazi ya wanachama ni kupiga kura kisha kwenda nyimbani kusubiri matokeo.
Wapo watu tunaowalipa kwaajili ya kulinda raia na mali zao, ukishamaliza kumpigia kura JPM wewe nenda nyumbani kaburudike.

Tumpigie kura JPM kwa wingi mpaka Ufipani wachanganyikiwe.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hahaaa, hivi Mawakala wanaruhusiwa kuingia na simu?
 
Sikutaka kuizingatia phrase ya mleta mada, nimezingatia maelezo yako kwamba "huwa ni utaratibu mawakala kuwepo",jambo ambalo ndio ukweli wenyewe, hivyo sikupingi kumkosoa mleta mada.
Swali langu ni, kwanini baadhi ya vyama hulalamika kuibiwa Kura baada ya uchaguzi, licha ya kuwepo kwa Hawa watu?

Umejiuliza vema, jibu ni sio mara zote kura huibiwa... lakini hata pale inapotokea wizi, mwizi ni yule mwenye 'nguvu' hivyo anaweza kuwaahidi/kuwapa chochote kitu mawakala wenye njaa kali.

Kwa chaguzi nyingi hapa nchini, vyama 'vingine' hushindwa kuajiri mawakala kila kituo sababu ya ukata.
 
Hata hivyo amesema “Tayari vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi, vimepata nakala tepe ya orodha ya wapiga kura waliomo katika orodha ya daftari la kudumu la wapiga kura hii ni kuwawezesha mawakala kutimiza wajibu wa kuhakiki wapiga kura wanaofika kituoni” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi

Sheria inasema daftari liwe na picha za watu na miaka yote imekuw ahivyo, mwaka huu naiskia wametoa daftrai lisilo na picha.
yani unangalia jina tu ila kujua huyu ni nani hakuna.
BAO LA MKONO HILO.
 
Umejiuliza vema, jibu ni sio mara zote kura huibiwa... lakini hata pale inapotokea wizi, mwizi ni yule mwenye 'nguvu' hivyo anaweza kuwaahidi/kuwapa chochote kitu mawakala wenye njaa kali.

Kwa chaguzi nyingi hapa nchini, vyama 'vingine' hushindwa kuajiri mawakala kila kituo sababu ya ukata.
Kwamaana hiyo bado hatujawa na watu wenye uchungu,wanaopigania maendeleo ya watu kutoka upinzani,kiasi kwamba wananunulika kirahisi🤔? Au ndo kusema kwamba kila mtu kwenye siasa yupo kwaaliji ya tumbo lake eeh🤔?
 
Baada ya kupiga kura wanachama wataruhusiwa kulinda kura zao?

Kwani kanuni zinasemaje kuhusu hilo?kama kuna mawakala huko ndani ya kituo cha kupigia kura unasubiria nini tena hapo nje?kukwepa matatizo yasiyo ya lazima na vyombo vya dola ukishamaliza kupiga kura kapuumzike nyumbani mengine tume itafanya kwa mujibu wa sheria na kanuni
 
sio kazi ya wanachama kulinda kura.

kazi ya wanachama ni kupiga kura kisha kwenda nyimbani kusubiri matokeo.
Na asipoenda nyumbani? Mathlani akienda kanisani au msikitini? Kazini? Shambani? Kwa mpango wake wa kando? Kwenye kijiwe cha jirani? Akifanya vyote badala ya kwenda nyumbani atakuwa amekiuka kifungu kipi cha sheria ipi?

Amandla....
 
Sasa kila mtu akitaka abaki kituo Cha Kura ili alinde Kura za chama chake itakuwaje 🤔?
Itakuwa shwari kabisa. Kama hapatakuwa na jaribio la kuiba kura. Au kubadilisha matokeo kwa njia yeyote.

Amandla...
 
Kwamaana hiyo bado hatujawa na watu wenye uchungu,wanaopigania maendeleo ya watu kutoka upinzani,kiasi kwamba wananunulika kirahisi[emoji848]? Au ndo kusema kwamba kila mtu kwenye siasa yupo kwaaliji ya tumbo lake eeh[emoji848]?

Umehitimisha vema, lakini pia njaa haihalalishi 'rushwa' kwa mnunuaji.
 
Back
Top Bottom