Elections 2010 NEC kushurutisha wapiga kura kurudi majumbani badala ya kusubiri matokeo vituoni!

Bila Dr Slaa na CHADEMA kampeni za mwaka huu zingekuwaje?
 
Watu makini wote dunia nzima watakushangaa, lakini kwa watu hovyohovyo upo sahihi.
Angalia umakini wa JK katika utawala wake wa miaka mitano iliyopita.
1. Baada ya kukosoa mikataba ya madini ya watangulizi wake akaingia mkataba na kampuni hewa Richmond na kampuni tapeli RITES (Hiyo ni serikali ya rais makini?).
2. Alikataa wizi wa pesa za umma EPA na kudai kuwa hizo ni kelele za wapinzani tu hakuna wizi huo. World Bank waliposhinikiza ufanyike uchunguzi huru JK kajiumbua (Rais makini?).
3. Akilihutubia bunge kuhusu kashfa ya EPA, alitoa msamaha kwa wezi wa EPA watakaorudisha pesa hiyo ndani ya miezi 3. Bila kujijua kavunja sheria na kuingilia uhuru wa mahakama, in short kavunja kiapo chake cha urais (rais makini?).
4. Alisaini sheria ya gharama za uchaguzi bila kuisoma, Dr. Slaa akamuumbua kwamba vipengele vimeongezwa kinyume na sheria iliyopitishwa na bunge (kapitisha sheria batili , rais makini?).
5. Kachomekewa barua feki ati TUCTA walichelewa kuhudhuria kikao, TUCTA wakamuumbua (rais makini?).
Uoza ni mwingi kuliko huo umakini unaouzungumzia ndugu. Labda utueleze kwa vielelezo sahihi si takwimu za kufikirika. ALIFANYA NINI AKIWA IKULU MIAKA MITANO ILIYOPITA?
 
wachochezi ni kina nani?ccm wanaojiandaa kuiba kura au Chadema wanao himiza watu kulinda haki zao.CCM mnatumia amani kama gia ya unyanyasaji.Amani unayo zungumzia ni ipi?mwanakijiji kufia kwenye baiskeli akienda kujifungua huku mawaziri wakila kiyoyozi?2010 hatudanganyiki.
 
kUMBE GAZETI LENYEWE mTANZANIA, LA FISADI? HAHAHAA, MBONA ULALAMIKI WANAOKWENDA KUCHAPISHA KARATASI ZA ZIADA ZA KUPIGIA KURA? HAO WATU WA ZIADA YA WALIOJIANDIKISHA WAMETOKA WAPI? UNACHEKESHA. CHAMBUA OJA NDIO UTOE HUKUMU.
TUSUBIRI NI NANI HATAKUFA KWA UTABIRI WA MLINZI WA RAIS KWA NGUZI ZA GIZA ZISHAONDOLEWA SASA, TEH TEH EH EHEHEEEEEEEE
 

Inawezekana we bwana mdogo unamatatizo sio bure? Ulichokifanya huyo JK awamu iliyopita ni kipi? zaid ya kuendeleza na kumalizia kazi za Mzee Mkapa. We inaonyesha tayari umefisadishwa kimawazo na fikra na hao mnaowaita SISIEMU.DR.SLAA ni Mtanzania wa Pili baada ya Nyerere so ni kwa nn asiwafundishe Kuukataa ufisadi? "TIME FOR NEW CHANGES WITH CHADEMA SAY" YES WE CAN!!!
 
Kwa taarifa yako, CCM imejiandaa kuanzisha vita ikishindwa uchaguzi. Najua kwa umbumbumbu wako utapinga. Ukweli ni kwamba CCM imeanzisha jeshi linaitwa green guards, walipewa mafunzo ya kijeshi katika kila jimbo kwa miezi mitatu. Silaha wanazotumia ni mapanga na marungu. Mnajinadi mmeleta amani, jeshi hilo kubwa mmeunda la nini? Mapanga na marungu ni ya kumpigia nani? Jeshi la polisi hamliamini nyie CCM? Hata mkitumaliza wote hatutawasujudia kamwe.
Tuambieni ni chama gani kingine chenye jeshi lake?
 
Ulikuja humu kuvote kwenye hiyo JF poll hapo juu umwongezee JK point. Amin amin nakwambia , kabla halijawika jogoo tarehe 31/10/2010 tutakuwa umemkana JK mara tatu.

...utakuwa umechelewa...inatakiwa iwe hivi: AMIN AMIN NAKWAMBIA, kabla jogoo hajavaa chupi TAREHE 31/10/2010 TUTAKUWA tumeikana CCM mara tatu!
 
JF imevamiwa!!! Hawa watu wametoka wape mbona amani na UTULIVU wa humu ndani unaanza kupotea. Ni nadra kusikia taarifa MFU kama hizi!!! Wamepandwa na baadaye kuzalishwa kwa wingi ili waje ku POLL nashangaa jinsi KIKWETE anavyoongeza kura kumbe ni hawa mamluki. UTAWATAMBUA KWA MATENDO YAO.
 
HAWAJAWAFIKIA WANACCM KWA UCHOCHEZI HATA CHEMBE!




Be wiser than other people if you can, but do not tell them LIES!
 

heri kufa maskini ukiwa huru kuliko kuwa tajiri uchwara huku ukiwa mtumwa wa mawazo!
 
Rubbish. how can someone give comments to this stupidity?
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi akanukuu hizo toilet paper za RA, yeye huyo bwana wenu RA ndiye mchochezi na siku zake zinahesabika kabla hatujamtundika. Hivi nyie mnao mshabikia RA na genge lake ni watz kweli au ndiyo rushwa imeshawapofusha? Hivi kuna uchochezi zaidi ya kuwaambia waathirika wa ukimwi wana kiherehere?
 

wewe dadakuona kwa kawaida napenda kuheshimu kila mtu na maoni yake lakini akiwa mvivu wa kufikiri au kilaza mimi huwa simwelewi.kwanza naomba tuchambue kauli hizi mbili ndipo tutajua mchochezi ni nani? nakama zote zitakuwa za kichochezi ninani alikuwa wa kwnza kutoa kauli na tutoe hukumu ya haki kwa mustakabali wa nch yetu tukufu iliyonajisiwa na kikundi cha watu wachache.naomba usiwe na jazba.kaa.utulie ukishirikiana na wote waliokugongea thanks.
nchi ni ya kidemokrasia inapata serikali kupitia uchaguzi,kuna vyama vingi vya siasa nawagombea watano kwa nafasi ya urais na katikaa demokrasia anaeongoza ndiye anaeunda srikali kama sio aliyepata 51% sasa naombeni tuchambue hizi kauli mbili nafikiri jibu liko hapa na baada ya jibu tumpatie adhabu inayomstahili mchochezi bila kumtazama usoni,hii nchi ni ya watz zaidi ya milioni 40 vikongwe,walemavu aina zote,watoto vichaa, na wengi wasiojiweza ambao wanahitaji msaada wetu.sasa kampeni zinaanza mmoja anasema USHINDI NI LAZIMA baada ya mwezi na ushee wapili nae anahamashisha wanachama wake TUACHE WOGA TULINDE KURA KWA GARAMA ZOTE naomba kuwakilisha na mungu awabariki kwa sababu najua mtatumia busara zaidi ya jazba
 
Kura ni lazima zilindwe,tuachane na hawa jamaa wenye kutaka ushindi wa mezani.
 
Heri kuwa mchochezi kwa ajili ya walalahoi kuliko kuwa mjinga kwa ajili ya utulivu ( Tanzania hakuna amani kuna utulivu wa kijinga)

Unataka kuwapigia watu magoti ili kuwanadi wagombea????

 
Amani ipo nyumbani kwenu Masaki!!!

mh...mh...................!!!!!!!!!!!!!!!!!!
no ...no..no ,,..Not true,
Let us be honest,nowhere in Tanzania there is peace and Liberty.Everything is already kachachuadi.
 

Mh! Huyu lazma atakuwa ni RizK-wala asituumize vichwa.
 


The Following 3 Users Say Thank You to dadakuona For This Useful Post:
Kakalende (Today), Kibunango (Today), Malaria Sugu (Today):becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…