Atakwenda vyombo vya kimataifa
Amtumia salamu RC Mwakipesile
Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa.
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa, amesema chama chake kitalifikisha katika vyombo vya kimataifa duniani kote kulalamika ikiwa kura zake zitaibwa wakati wa uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni katika uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma mjini baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Mbeya kabla ya kuelekea katika mkoa wa Rukwa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Slaa alisema hatua ya kulalamika katika vyombo vya kimataifa kuhusu hali hiyo kunatokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, kwamba baadhi ya wanasiasa wanahatarisha amani kutokana na kueleza kuwa damu itamwagika katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba atakayekataa matokeo atashughulikiwa. [/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na kauli ya Shimbo, natangaza kuwa japo sina nia mbaya ya kulichafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu nalipenda sana, lakini mtu kama Shimbo tutaendelea kumpeleka kwenye vyombo vya kimataifa, tutapiga kelele dunia kote kwamba JWTZ wana nia ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu," alisema Dk. Slaa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema JWTZ na serikali watoe kauli kama tamko alilolitoa Shimbo ni lake binafsi au ni la JWTZ ambao wanalipwa mishahara kwa kodi za Watanzania.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Nikisema haya hatutanii, nataka kumwambia Shimbo na askari wake wote wenye sura ya aina hiyo kwamba Tanzania ya leo haiogopi, haitishiki, JWTZ wanaweza kuwa na mabomu, lakini yakashindwa kuwa na nguvu mbele za umma," alisema Dk. Slaa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Slaa aliongeza kuwa Shimbo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, wanajua sheria kwani badala ya kulalamikia kwa wananchi kuhusu matamko ya wanasiasa waliotishia kwamba damu itamwagika walitakiwa kuwakamata wahusika. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema sheria ya nchi haiwataki askari kuegemea chama chochote cha siasa. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Slaa pia alimgeukia Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbozi, (OCD) SSP Dudu na kumtaka ajiuzulu nyazifa hiyo kama hatamfukuza kazi askari wake anayetembelea makanisani na kueleza kuwa Mgombea Urais kupitia Chadema alishawahi kusaini mkataba wa kutaka Tanzania ijiunge katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC). [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akihutubia mkutano mweingine wa kampeni, alimtahadharisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, kwamba iwapo ataingia madarakani atamshughulikia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema hayo juzi katika mji mdogo wa Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini katika siku ya pili ya ziara yake ya kampeni mkoani Mbeya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Slaa alisema atamshughulikia Mwakipesile kwa madai ya kuhusika kuhujumu mikutano yake ya kampeni aliyoifanya katika Wilaya za Kyela na Mbeya Vijijini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Mwakipesile amehujumu mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Kyela kwa kumuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyela (OCD), SSP Male asilinde helikopita inayotumiwa na mgombea huo, ambayo ililala katika uwanja wa Mwakangale mjini humo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema hujuma nyingine iliyofanywa na Mwakipesile, ni agizo lake kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kukata umeme katika mji wa Mbalizi ili mkutano wake wa kampeni usiweze kufanikiwa.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Tanesco wamekata umeme kwa shinikizo la Mkuu wa Mkoa. Nampa onyo. Kama amezoea kuchezea watu wengine hapa kwangu amefika na ninamwambia baada ya Oktoba 31 mwaka huu nikiingia tu Ikulu atafute pa kwenda," alisema Dk Slaa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Slaa alisema kutokana na wananchi wa Mbeya kuwa na imani na Chadema, chama hicho kitahitimisha kampeni zake Oktoba 30, mkoani hapa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema chama chake kinahitaji wabunge wakakamavu na si kama wale wanaoingia bungeni na kuanza 'kuchapa usingizi' na hivyo kushindwa kutetea wananchi waliowachagua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Askofu Pentekoste na wizi wa kura[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God Tanzania, Daniel Awet, ameishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka mazingira ambayo yatakayowezesha kuziba mianya ya wizi wa kura.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Askofu Awet alisema hayo akizungumza katika ofisi za NIPASHE mjini Dodoma jana ambako alifika kuzungumzia mambo mbalimbali yaliyojiri katika Mkutano wa Uchaguzi wa Viongozi wa Kanisa hilo uliofanyika juzi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Askofu Awet alisema hatua hiyo itasaidia kujiepusha na malalamiko yanayotolewa na vyama vya siasa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Askofu Awet alisema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwamba vitaibiwa kura hivyo akasema ni vizuri Tume hiyo ikaweka mazingira yatakayoziba mianya ya wizi wa kura ambayo inalalamikiwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, askofu huyo aliitaka Tume kufikisha vifaa vitakavyotumika katika uchaguzi kwa wakati kwenye vituo vya kupigia kura ili kuondoa usumbufu usio wa lazima.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, aliwataka wagombea wa vyama vya siasa wajiepushe na kampeni zinazoshabikia udini, ukabila, jinsia na rangi kwenye majukwaa wanapozungumza na wananchi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema tabia hiyo inachafua sifa ya taifa na pia inaharibu umoja wa kitaifa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Askofu huyo aliwataka wagombea walisimamishwa na vyama mbalimbali vya siasa kukubali matokeo yatakayotolewa na kutangazwa na Tume ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataka viongozi wa dini kuwaelimisha waumini juu ya umuhimu wa kwenda kwenye vituo vya kupiga kura kwa wale waliotimiza masharti yote ili kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Imeandikwa na Augusta Njoji, Dodoma, Thobias Mwanakatwe na Muhibu Said, Tunduma.[/FONT]