Elections 2010 NEC kushurutisha wapiga kura kurudi majumbani badala ya kusubiri matokeo vituoni!


Hivi sheria si kuwa mbali na kituo kama mita mia moja au mia mbili? Wananchi tukae umbali huo na tuangalie nani anaingia na nani anatoka kwa mbali. Ikiwezekana tutumie binoculars ambazo zipo nyingi tu kwa wamachinga!
 
Tumevamiwa, hawa watu wantupotosha ili tusiendelee kujadili hoja za msingi.

Tuwapotezee!! Maana wasipojibiwa watakaa kimya!!
 
Suala la ulinzi shirikishi wa kura ni muhimu sana hasa kwa kipindi hiki ambacho tunaelekea katika uchaguzi. Pamoja na kutaka kuwa na ulinzi shirikishi wa kura hasa kwa wapiga kura kukaa jirani na kituo cha kupiga kura mpaka matokeo yatakapotangazwa, kuna mamabo ya msingi kabisa yanayotakiwa kuwekwa wazi na kwa ufahamu mpana zaidi. Mfumo huu wa kulinda kura umekuwa ukitumika sana kule Tarime kwa kusimamia kwuwa suala la kuondoka kituoni baada ya kupiga kura haliko katika sheria. Pia suala hili la kuondoka kituoni bado limekuwa likihubiliwa sana kiasi cha kutisha, na wakati huohuo mpiga kura anatakiwa asikilize matokeo ktk kituo alichopigia kura. Je kisheria zaidi suala hili linakaaje?
 
Ninavyofahamu mimi (ref. 2005 election) unatakiwa kuwa mita 100 kutoka kituoni.

Kama kuna mabadiliko wana JF tuelimishane.

LINDA KURA YAKO.... 2010 HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!
 
National Elections Act 1985
86. (1) No persons other than the following may be present at the counting of votes–
(a) the Presiding Officer;
(b) a polling assistant;
(c) a polling agent or an alternate polling agent;
(d) a candidate;
(e) a police officer or such other person responsible for security at the place where votes are being counted;
(f) a Returning Officer, Assistant Returning Officer, or a Regional Election Co-ordinator;
(g) a member of the Commission;
(h) the Director of Elections or an electoral officer of the Commission; and
(i) an election observer duly authorised in writing by the Commission.
(2) No person other than those referred to in subsection (1) shall be permitted to be within the vicinity of the place where votes are being counted

See highlighted. Vicinity kwenye maisha ya kawaida imetafsiriwa kuwa ni mita 100 kutoka kituo cha kupigia kura.
 
Kuhusu kulinda kura mwaka huu Chadema wamejipanga kwanza tayari wana cds za wapinga kura wa kila kituo kutoka tume ya uchanguzi na kila atakae kuwa anasimamamia kituo atakuwa na copy ya wapiga kura wa kituo husika kutoka tume siyo kutegemea yanayo bandikwa...msimamizi wa kitu atakuwa akihakiki kwa ku-tick kwa kufata list yake kutoka tume...watatoa semina ya wasimamizi wote jinsi ya kuzuia udanganyifu...kuhusu kukaa karibu na kituo ulichopingia kura sizani kama inakubalika ngoja tusubili wana sheria watalitolea ufafanuzi.....Maana kutengemea msimamizi tu haitoshi
 

KATIKA MAMBO YOTE TUNAYAOJADILI HUMU HILI NDILO JAMBO LA MUHIMU SANA KULIFAHAMU. ni wazi kuwa sio rahisi watu wakaruhusiwa kukusanyika baada ya upigaji kura na hata katika zoezi la kuhesabu kura. Lakini kama raia wemye mapenzi mema na nchi yao ni lazima waonyeshe shauku ya kufahamu kura zinvyopigwa na kuhesabiwa kwa kukaa mita 100 kutoka kituo cha kura. Hivi ndivyo ilivyofanyika katika majimbo yote ambapo upinzani ulishinda ikiwemo Tarime n.k

Kitendo cha wananchi kukusanyika kwa wingi kufuatilia mchakato wa uhesabuji wa kura kwa kuaa mita 100 kutoka kituo cha kuhesabia kura huwafanya wachakachuaji wa kura kuingiwa na woga, mawakala wanaotaka kuuza haki za wagombea kuingiwa na woga; na kubwa zaidi viongozi wa Serikali hususan wakuu wa wilya na mikoa ambao hushinikiza kubadilishwa kwa matokeo nao kuingiwa na woga wa kuvunjika kwa amani na hivyo hukubali kuwa ccm imeshindwa katika jimbo husika.
 
Naombeni tujadiri ni mikakati gani tutatumia hili jamaa wasiendeleze kaufundi kao,,uwanja huo!
 
Kukomaa mpaka dk ya mwisho kwenye maeneo ya kupiga kura
 
Kukomaa mpaka dk ya mwisho kwenye maeneo ya kupiga kura

Kukomaa pekee haitoshi, inalazimu kufanya upekuzi wa kina katika vyumba/Nyumba ambayo tume wamechukulia kuwa kituo cha kupiga na kuhesabia kura. Nasema haya baada ya Jumamosi iliyopita askari mmoja alinieleza alipata kushiriki kusimamia zoezi zima la kupiga na kuhesabu kura katika kituo kimoja, mbinu aliyonieleza ambayo ilitumiwa katika wizi wa kura sijawahi kuisikia wala kuisoma katika baadhi ya mbinu zilizowahijadiliwa humu JF. alisema
  1. CCM wakati mwingine mtu huweka kambi darini akiwa na masanduku ambayo yana kura zinazompatia ushindi mgombea wa ccm katika kituo hicho, wakati wa chakula ukifika mkuu wa askari huja na kuamrisha watu wote kula chakula kwa pamoja na sehemu moja lakini nje ya chumba, wasimamizi wote hujiridhisha kwa kuangalia huku na huko katka nyumba husika na wote hutoka kwend ambapo chakura kimeandaliwa na kituo cha kura kufungwa na askari kwa ushuhudiwaji na mawakala wote. HILO HUWA KOSA, KUFANYA HIVYO TU YULE ALIEWEKA KAMBI DARINI MASAA KADHAA KABLAYA KITUO KUGUNGULIWA HAFANYI KOSA HUSHUKA NA KUBADIRISHA MASANDUKU AMBAYO HUWA YANAFANANA KABISA
  2. Wakati mwingine askari huletewa Bites kila mara katita mifuko/bahasha ya kaki, bahasha zingie huwa zimechakachuliwa bites pamoja na mlungula(hongo) hivyo kila askari hushngaa na hawezi kumwambia mwenzake aliniambia kiasi hicho kwa mwaka huo kilifikia Sh. 100,000/= baadaye mkuu waaskari huja na kuwauliza askariwake kama wote wamekuwa wakipata bites, huitikia tumeletewa mkuu, baada ya kitambo gari hiyo ya mkuu wa askari huja muda wa chakula na huegeshwa nyuma ya kituo cha kupigia/kuhesabia kura na kitendo bila kuchelewa masanduku hubadilishwa kupitia milango ya nyuma. na alisisitiza kuwa katika mwaka huo wa uchaguzi vituo vyote kwa asilimia kubwa ilitakiwa viwe na mlango zaidi ya mmoja.
Kwa haya ndio maana nasema TUNAHITAJI ZAIDI YA KUKOMAAA, NI LAZIMA KUWA ZAIDI YA MAKACHERO
 
Naombeni tujadiri ni mikakati gani tutatumia hili jamaa wasiendeleze kaufundi kao,,uwanja huo!

Tunaweza hata kutumia mtindo wa Jerry Muro kwani simu zetu wengine zina camera na hivyo ukiwa karibu na kituo basi piga picha/video tukio lolote unalolishuku kwa wizi wa kura. Tena picha zikiwa uploaded humu JF zitasaidia.

Mbinu hii tuliitumia Mwakyembe alipoata ajali tuliona picha saa zilezile anaingizwa hospitali kule Iringa wakati hata magazeti hayajaanza kutoka.

Mbinu hii ilitumiwa na waliomnyonga Sadam Hussein hivyo jeshi lisijidanganye kuwa watafukuza watu kituoni kwa kisingizio cha fujo wakati kila kitu kitakuwa live.

Ma-wakalawa vyama wapelekewe na wasikubali kutoka ndani ya chumba cha kura hadi wame-sign matokeo.

Ikiwezekana michango tunayotoa kwa CHADEMA zinunuliwe photocopy za kutosha mawakala wakishahesabu matokeo wayapige photocopy palepale na kila mmoja aondoke na copy yake signed.

Wengine changieni kuisambaratisha ile mbinu ya kwamba unapiga kura kwa SLAA halafu ukikunja karatasi basi wino unafutika kwa SLAA unahamia kwa JK.

Mbinu hii hutumika kwa wahasibu wakorofi na kuna kalamu za aina hiyo ambazo wino wake ni matata kihivyo.

Mbinu nyingine ni kwamba mawakala hata kama wana njaa gani wafikirie kwamba hata ukihongwa mamilioni bado katika taifa lililooza hutaweza kufanya kitu kwani biashara yoyote utakayoanzisha hutaenda popote kwani mafisaid wameshamiliki kila kitu na hakuna biashara hapa nchini bali ni ufisadi, kwani ingekuwa biashara inalipa wasingekimbilia siasa na matrilioni yao.
 
jatropha umeongea kitu kizuri sana,lazima kama tunataka ushindi wa CHADEMA hatuna budi kufanyahivyo.
 
muhimu ni kuweka mawakala waaminifu na wanaopenda mabadiliko, ambao wapo tayari hata kufa kwa kukataa uchakachuaji, mimi nipo tayari hata kufa ili nikumbukwe na taifa langu miaka ijayo. (kutetea na kuilinda nchi yako sio lazima uingie JESHI.)
 
Naombeni tujadiri ni mikakati gani tutatumia hili jamaa wasiendeleze kaufundi kao,,uwanja huo!

Nani kasema ataiba !! kuraz enyewe hata robo ya wa tanzania hazitofika
 

Rudia tena TAFADHARI!!!:llama:
 

Ninyi wenye mawazo ya kuombaomba ndiyo mnatuletea shida nchi hii. Hivi unafikiri TZ itaendelea kwa kuombaomba. Mawazo yako ni sawa na ya JK tu. Ndiyo maana uko busy humu kutetea ili mafisadi ili upate mahitaji yako kirahisi tu. Amka rafiki, fanya kazi upate kipato chako, siyo kutegemea kupiga debe humu ili upate malipo. Haya mambo yana mwisho wake.
 

:A S 13::A S 13::A S 13::llama::llama::llama::llama::llama:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…