NEC ndiye FIFA, TFF na refarii wa mchezo wa ligi ya uchaguzi tumwache afanye kazi yake

NEC ndiye FIFA, TFF na refarii wa mchezo wa ligi ya uchaguzi tumwache afanye kazi yake

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Wakuu bila kumumunya maneno kuna baadhi ya wana JamiiForums hasa wa vyama vya upinzani wana uelewa mdogo sana.

Uwezo wao wa ku reason mambo ni mdogo sana.

Wametyuni akili zao kwenye kushabikia siasa bila kukielewa kile wanacho kishabikia.

Wamekariri katiba na baadhi ya vifungu vya sheria ili tujue kwamba wanayaelewa mambo ya uongozi.

Lakini ukweli ni kwamba ushabiki wao umewapumbaza akili zao washindwe kuelewa kanuni za mchezo hata wa Simba na Yanga.

Hawajui kazi za refarii kwenye mchezo, wanaona ni sawa eti refali kumchezesha mchezaji aliye fanya madhambi uwanjani na aliyekwenda kinyume na kanuni za maadili ya mchezo.

Sikariri katiba wala sheria ila natumia uwezo wangu kutafakari kwasababu hata hizo sheria zilitungwa na wanadamu kama mimi.

NEC ni sawa na TFF au FIFA, NEC ndiye sawa na refa. CCM, CHADEMA, ACT, CUF hizi ndio timu zetu. Hizi timu zinawashabiki wao, ambapo wengine hawana akili za kutafakari ila wanashabikia tu.

NEC kama Refali au TFF au FIFA ndiye msimamizi wa ligi inayofanyika kila baada ya miaka mitano mwezi wa 10. Lakini kabla ya mchezo huo kufanyika ni lazima NEC ahakikishe timu zote na wachezaji wa timu zote wanaokwenda kushiriki kwenye ligi hiyo wanakidhi vigezo vya kushiriki ligi hiyo.

Wale ambao hawakidhi vigezo vya kushiriki ligi kamati ya maadili ya NEC au FIFA au TFF huwaondoa kwenye ligi na huwapatia adhabu ya kutoshiriki ligi kwa muda wa miezi au miaka kadhaa.

Hivyo ndivyo mambo yaendavyo. Wachezaji waliokwenda kinyume na kanuni za FIFA au TFF au NEC huenguliwa kwenye ligi ili wakajitathimi na kujifunza kwaajili ya ligi zijazo.

Tujifunze kutafakari mambo kwa kina badala ya kushabikia shabikia tu. Tuwaachie NEC, TFF, FIFA na refarii wafanye kazi yao. Hiyo ndio kazi ya NEC.

Kama wajumbe wamemaliza kazi yao basi huu ni muda wa NEC. Kama timu haijapanda daraja haina haja kuihusisha kwenye ligi. Wachezaji waliofanya madhambi na waliokwenda kinyume na kanuni za maadili za NEC au TFF hao hawafai kuwepo kwenye ligi kwa maana hawakidhi vigezo.

Ni Mimi meneja wa makampuni a. k. a Mr. Newton wa Tz

Sent from HUAWEI MATE 40 PRO
 
Unadhani hizo taasisi kwakuwa zina hayo mamlaka, basi wanaweza kuyatumia watakavyo, au kwa maagizo ya timu moja?
 
Mfano wa FIFA TFF ni mzuri sana na umejitosheleza lakini hujatuambia wanapatikana aje ? Ukishajua wanavyopatikana ndio utafahamu NEC ni chombo cha mtu na kitamtendea mazuri kwa mtu alie kiteua
 
Unaposema uelewa wa watu ni mdogo bila kujipima uelewa wako ni dhahiri upo gizani uzi wako ni kipimo cha kutufanya tuuelewe uelewa wako TFF FIFA ni tafauti kabisa na NEC waulize wadau wa mpira watakufahamisha jinsi ya kuvipata vyombo hivyo
 
Zigii habari za kukipata chombo hicho kipo ndani ya katiba. Unapaswa kuilaimu katiba na sio NEC.
 
Wewe jamaa uwezo wako bado Ni chalii kabisa.Unadhani NEC wao wanafanya wanachotaka,Kuna kanuni zinawaongoza katika Kila maamuzi.Na wakivunja sheria wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kwenda mahakamani.
Halafu tabia ya kuita wapinzani Wana akili ndogo Sana,itakucost maisha,Bora ujihadhali na kauli za kuudhi.
 
Zigii habari za kukipata chombo hicho kipo ndani ya katiba. Unapaswa kuilaimu katiba na sio NEC.

Sasa nitailalamikia vipi katiba wakati ww umezungumzia NEC, FIFA, TFF ? Nadhani labda upo nje ya tz ndio maana husikii malalamiko ya katiba
 
Wewe jamaa uwezo wako bado Ni chalii kabisa.Unadhani NEC wao wanafanya wanachotaka,Kuna kanuni zinawaongoza katika Kila maamuzi.Na wakivunja sheria wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kwenda mahakamani.
Halafu tabia ya kuita wapinzani Wana akili ndogo Sana,itakucost maisha,Bora ujihadhali na kauli za kuudhi.
Ini cost kivipi yaani mkuu. Kwamba wewe una uwezo wa kunicostisha maisha yangu au sijakupata vizuri.

Wewe labda unizidi uchawi tu lkn kwa habari ya nguvu na jeuri ya pesa nimekuacha mbali sanaa. Kwa hiyo tusitishane.

Ninyi mnapo msema vibaya Rais wetu mnadhani yeye anajisikiaje yaani huko aliko. Ninyi mkipigwa mishale mnaanza, kulia, lia

Jibu kwa hoja acha jaziba na nakuomba ujihadhari sana wewe kwanza maana mimi nikija kupewa hii nchi nitaminya, kabisa uhuru wa kuongea, kuongea kwa maana, mnautumia vibaya

Sent from HUAWEI MATE40 PRO
 
Back
Top Bottom