onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,356
- 1,309
Ni muda Sasa NEC kupitia picha na video kurudia rudia mafuriko na mikutano ya Lissu kusoma alama za nyakati. Mikutano ambayo haipewi matangazo ya kutosha, mikutano isiyorushwa live, mikutano isiyopewa kipaumbele kwenye taarifa za habari redioni, magazetini na vituo vya televisheni, mikutano isiyo na makundi makubwa ya wasanii, mikutano isiyokuwa na wanafunzi wanaolazimishwa kufunga shule na mikutano isiyo na mabasi na malori ya kusomba watu. Mtu anayepita na kuomba michango kuendesha kampeni kubwa ya kutisha. Mtu aliyekosa mabango makubwa, lakini umashuhuri na nyomi Ni wali wa kushiba mfungwa aliyetoka jela.
Kama NEC watakuwa makini Basi wasichezee hisia za umma. NEC watimize wajibu wao Kama wasimamizi wakuu wa uchaguzi unaoelezwa Ni wa kihistoria. Juhudi au njama za kutaka au kuwaza kupindua matokea haiwezi kuvumiliwa na umma wa wapenda amani. Hili zoezi linaweza kuingia doa endapo tu hiyo NEC ikaboronga kwa namna itakavyoshindwa kuusimamia vizuri.
Yapo Mambo mengi ambayo yanasemwa na kauli hizi sijui kwa Nini NEC haijazisikia na kutoa ufafanuzi. Upo uvumi usiothibitishwa kuwa CCM kupitia kwa makatibu wakuu wake wanakutana na makundi ya watumishi na kuwahimiza waombe kusimamia uchaguzi kwa lengo la kubadili matokeo vituoni. Kama hili wazo lipo Basi wahusika wakome Mara moja kuendelea kuratibu huo hujuma na NEC wapeleleze na kukemea au kutoa onyo.
Kwa namna wapiga kura walivyo watulivu na kuhudhuria kampeni za Lissu na Magufuli basi ni wazi uchaguzi huu ni vuta nikuvute. Nia mbaya za upendeleo hazitavumilika, kauli na uvumilivu Ni kitu muhimu Sana. Siyo busara kwa NEC kusema ukiukwaji na taratibu watumie nguvu za kipolisi Kama ilivyotumika Nyamongo. Muda Fulani kwa sababu za kijografia Ni kuketi na wadau meza moja kutazama juu ya ratiba.
Polisi wakae Kando maana kujikuta uko kituo A badala ya B siyo makusudi Bali Ni kosa la kawaida tu. Hivyo isije kuwa suluhu ya polisi na NEC Ni kuagiza watu kupigwa mabomu. Uchaguzi huru, Kama umakini utakuwepo utawezekana. Vifaa visambazwe mapema na mawakala wote wapewe fomu na kuruhusiwa kusimamia vyama vyao. Itambulike eneo muhimu Ni hapa kwenye vifaa na mawakala toka vyama vyote.
Uchaguzi na maandalizi mema. Niwatakieni busara na lugha Safi wagombea. Si kila tuhuma dhidi ya NEC Ni tusi au khasifa Bali Ni maono ya njama zilizopita. Pia NEC irahisishe rufani za wagombea waliobaki kwa kuwekewa pingamizi. Hii inaichafua NEC kitaifa na kimataifa, haikuwahi kutokea wakati wa kina Mkapa na Kikwete Sasa iweje kipindi hiki?
Uoga wa CCM isije kutafasiriwa kuwa Ni kutaka kubebwa na NEC . Kikubwa Ni kuwa atakayeshindwa ndiye atangazwe toka kituo Cha kupigia kura Hadi kituo Cha kutolea matokeo. Vyama pia visiingiliwe kwenye talling centres zao. Waachwe kuwa huru maana Ni haki yao kuwa na matokeo na kufuatilia vyama vyao. Narudia polisi na watumishi toka NEC wasikipendelee chama Chochote.
Amani idumu Tanzania