Uchaguzi 2020 NEC tumieni mafuriko mikutano ya Lissu kusoma alama za nyakati

Sijui natamani wangekuwa wanauliza hao wanaofurika kama wana kadi za mpiga kura na ingekuwa kushangiliwa ndio kushinda team za mpira zisingeshida ugenini
 
mashabiki wengi wa lissu wana miaka 17-30 ambao wengi wao 2010-2015 hawakuwa na access ya taarifa kujua hali ilikuwaje??

mwaka huu hakuna mafuriko.
 
Ujamuona mgombea wenu anapiga hadii magoti Hali tete zile spana si za nchi hii amepigwa spana Hadi kuomba poo na kwenda garage kurekebisha nati nati bolti zilizolegea.Hadi marefa kina mahera na Igp kuingia kuokoa jahazi
 
Sijui natamani wangekuwa wanauliza hao wanaofurika kama wana kadi za mpiga kura na ingekuwa kushangiliwa ndio kushinda team za mpira zisingeshida ugenini
Nguvu ya mabadiliko huwa haitegemei kadi ya kura
 
Trump yuko sibitali kakibali yaishe. Nilimsikua Lissu kwenye mkutano na wandishi wa habari, eti,eti, eti.... Ushindi ni mapema asubuhi. Jamaa ni kana tahira flani hivi unajua. Katika hali ya Mikutano ya kampeni ya CCM ya wagombea wao wote inavyoendeshwa kwa umahiri mkubwa cdm wakipata 5% kwao itakuwa ni matokeo ya kishindo.

Lissu hajielewi hata kidogo, he is doomed and the man is consumed by his own madness.
 
Mzee Yusuf aliimba wimbo Fulani wenye kibwagizo "utanibeba Leo, umekula pesa yangu ....." NEC is no exception.
 
Ujamuona mgombea wenu anapiga hadii magoti Hali tete zile spana si za nchi hii amepigwa spana Hadi kuomba poo na kwenda garage kurekebisha nati nati bolti zilizolegea.Hadi marefa kina mahera na Igp kuingia kuokoa jahazi
Basi hongereni kwa ushindi wanachadema
 
Unamkumbuka Agustino mrema, seifu,w.slaa na lowasa na bado walipigwa chini

Wewe utakuwa mgeni kwenye siasa za bongo
Kijana aliyezaliwa 1995 hajui hayo mafuriko ya Mrema.sa hizi ni ana miaka 25,in mpiga kura mwaka huu,na ana elimu ya chuo ameelimika usimweleze huu utopolo wako,na hawa ndio wana mwamko na mabadiliko,wamezaliwa wakakuta mfumo Wa vyama vingi.wengi wanaochukia ccm maana kwa miaka hii mitano wengi walinyimwa mikopo kosa wamesoma shule za private nk.
Asilimia kubwa ya wananchi ni vijana,wazee ambao ndio mtaji Wa ccm sio wengi kama vijana ,pia wazee wengine hawaitaki ccm,huu utawala Wa awamu hii ya tano ulikuwa Wa mateso kwa asilimia kubwa ya wananchi.
 
Ha
Mafuriko yake yanazidi yale ya Lowassa?

Je wanaokuja tena kwa idadi ndogo ni wapigakura?

Sisi wapiga kura tupo majumbani tunasubiri tarehe tukampigie Magu tena
lowassa alishinda ule uchaguzi lakini alitangazwa mwingine hivyo umakini unahitajika zaidi katka huu uchaguzi
 
Upuuzi mtupu. Mafuriko kama yanasaidia ya Mrema na Lowassa yangewafanya ma Rais zamani. Watu hatuchagui mafuriko, tunachagua Sera.
 
Lissu ana uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya 70% endapo yafuatayo yatafanyika na CDM.

Kuziba mianya ya wizi wa kura kwa ili kuhakikisha mizengwe ya CCM haifanyiki kwenye vituo vya kupigia kura
1. Mawakala wote wa CDM waapishwe na kupata barua za utambulisho kwa muda sahihi
2. Kura za Rais, Ubunge na Udiwani zihesabike hapo hapo kituoni na wakala wapatiwe nakala halisi ya matokeo
3. Matokeo yabandikwe kituoni - na mwisho kabisa
4. Mshindi atangazwe.

Sasa haya yakifanyika vyema nchi itakuwa na amani!!

Vinginevyo ..... ni kumwaga mboga ili wote TULUMANGIE.
 
Mafuriko yake yanazidi yale ya Lowassa?

Je wanaokuja tena kwa idadi ndogo ni wapigakura?

Sisi wapiga kura tupo majumbani tunasubiri tarehe tukampigie Magu tena
Uko sahihi kabisa. Hata NEC ingekuelewa au ingeelewa kama wewe, haingekua na haja ya kupata hiyo hofu. Mafuriko yenyewe yanayokua kwa Lissu ni madogo, pia hao wanaokusanyika kwa Lissu siyo wapiga kura. Ungefanya utaratibu wa kuwatuliza NEC kwamba huyu mtu hana madhara, watulie tu.
 
NEC wakiharibu uchaguzi itawagharimu... Watu hawana uoga ktk kudai haki.... Haki aiombwi haki inadaiwa..
 
MAGUFULI =NEC

"Magufuli aliwahi kisema Mimi mtu akinishauri ndio ameharibu kabisa maana sitofanya anacho nishauri"

"Aliwaambia wakurugenzi.
Nimekupa kazi.
Nimekupa mshahara.
Nakupa gari zuri.
Nakuapa posho.
Nakupa Nyumba bado unaenda kutangaza ushindi kwa mpinzani iiii??????"

MSITEGEMEE KUWA NA UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA SI RAHISI KIASI HICHO TUNA RAIS DIKTETA YEYE NDIO KILA KITU ALFA NA OMEGA.
 
Mafuriko yake yanazidi yale ya Lowassa?

Je wanaokuja tena kwa idadi ndogo ni wapigakura?

Sisi wapiga kura tupo majumbani tunasubiri tarehe tukampigie Magu tena
Acha dharau. We unaona Tl ana busara za Lowasa? Unadhani viongozi wako wasingekaa na kukubaliana na Lowasa atulize wafuasi wake ingekuwaje? Hatari ya machafuko IPO na ni kubwa na watu hawalali wakihakikisha hayatokei.
 
Ndg yangu nataka nikueleze kuhusu mafuriko unayoyapigia chapuo.Hayo mafuriko yana aina tatu au nne,nitaongelea upande wa JPM maana nikiongelea LISSU mtasena mnazi wa CCM.(1) Kuna kundi linahudguria kwa mapenzi ya kweli
(2)Kundi la pili kumuona JPM huyu RAIS yukoje kwasababu wengi wetu tumezoea kumuona kwenye vyombo vya habari, wengine wanasikia sauti tu kwenye Radio.
(3)Kundi la tatu wapenda burdani,na kundi hili wengi wao ni vijana.
(4) Kundi la yeye anahudhuria kusikiliza kitakachoongelewa pale.
Mwisho wa makundi yote haya nikupata ujumbe wa dhamira ya mkusanyiko huo.Matokeo ya kura ni suala jingine tusidanganyike na na wingi wa watu tujali kufikisha ujumbe.
 
NEC wakiharibu uchaguzi itawagharimu... Watu hawana uoga ktk kudai haki.... Haki aiombwi haki inadaiwa..
Sijui kwa nini NECCCM hawasomi alama za nyakati,hawakuona kule nyamongo watu walipigwa mabomu na hawakukimbia.watu wengi wanatamani utawala huu Wa ccm uondoke.
 
Mwaka huu uchaguzi huu,asipoangalia huyo uchwara,uchaguzi huu utamshangaza watu wanaweza wasiikubali kuibiwa kura zao.Mark My words.
 
Acha dharau. We unaona Tl ana busara za Lowasa? Unadhani viongozi wako wasingekaa na kukubaliana na Lowasa atulize wafuasi wake ingekuwaje? Hatari ya machafuko IPO na ni kubwa na watu hawalali wakihakikisha hayatokei.
Mjinga katika ubora wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…