Uchaguzi 2020 NEC tumieni mafuriko mikutano ya Lissu kusoma alama za nyakati

Anahamasisha chuki na vurugu nchini.

Kumuacha afanye atakavyo ni kujiweka rehani
 
Ha

lowassa alishinda ule uchaguzi lakini alitangazwa mwingine hivyo umakini unahitajika zaidi katka huu uchaguzi
Lowassa alishinda jwa sabuni za CHADEMA walivyomtakasa baada ya kumtia dhambi?

Sikiliza wewe parody, Lissu hana uwezo wa kushinda hata asilimia 10 za kura
 
Lissu sio Lowasa wa kumuachia Mungu,pili hoja ya awajaajiandikisha ni hoja mufilisi kabisa,kwani hao nyomi wa CCM wamejiandikisha.
Hahahaha
Bwege sana wewe. Unadhani Lissu anaweza kupata idadi ya kura zaidi ya baraza kuu la Chadrama?
 
Unamkumbuka Agustino mrema, seifu,w.slaa na lowasa na bado walipigwa chini

Wewe utakuwa mgeni kwenye siasa za bongo
Wizi wa kura mara zote..mwaka huu sasa basiiii..Magu atafurahi aibe kura aone
 
Wameshasoma kila kitu , shida ni pressure wanayoipata kutoka kwa watu waliozoea kushiriki uchaguzi kwa mazoea! Wananchi wa leo wale wa mwaka 1995, ambapo utapindua matokeo mchana kweupe wasijue kama umefanya visivyoeleweka! Nawashukuru Marekani tayari wametupia jicho uchaguzi wetu ujao, Tuzidi kuendelea kumuomba Mungu, anyooshe mambo yote kwa haki, na wale wote wenye nia ovu walegee na washindwe kabisa!
 
Mafuriko ndo nini,Chadema mmeanza kuchanganyikiwa!!
 
Mafuriko yake yanazidi yale ya Lowassa?

Je wanaokuja tena kwa idadi ndogo ni wapigakura?

Sisi wapiga kura tupo majumbani tunasubiri tarehe tukampigie Magu tena
Sijui sisi watanzania tulikua wapi kudai tume ya Uchaguzi , majirani zetu Kenya wanashangaa, mgombea ndiye anayeteua wajumbe, wakurugenzi na makamishna wa tume kweli tutegemee mkurugenzi atamwangusha aliyempa ugali?? Tuamke tuamke
 
Mafuriko ya Lissu yanajaa kwenye kiganja kimoja
 
Awe nazo asiwe nazo zingatieni uchaguzi huru na wa haki. Hofu ya nini mbona silaha zenu mnaelekeza kwa Lissu kama si hofu ni nini. Hila mbaya na mipango ovu iko hadharani. Kwa nink hayo

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Machafuko pekee ndio huleta heshima kwenye box la kura hapa Afrika. Kinyume na hapo huo ushauri wako mzuri huwa unaitwa malalamiko na wanaofaidika na huo mfumo wa dhuluma. Kama unataka huo ushauri wako ufanyiwe kazi, jiandae kuingia mtaani. Kinyume na hapo hili bandiko lako litabaki kuwa bandiko lenye busara, lakini lisilo na madhara yoyote.
 
Huu ni wakati ambao Mungu ametaka mabadiliko kwa Watznzania kutoka mikononi mwa CCM. Yote haya kuanzia CCM kumuweka Magufuli awe ndiye mgombea na kisha Rais wa Tanzania ni mipango ya Mungu. Mungu alipanga kuwa aje Magufuli ambaye atakibomoa na kukididimiza chaama cha CCm ili chama kingine cha upinzani kiingie. Angalia amenyang'anya chama kutoka ikononi mwa waliolienzi na kukipeleka kwa wapinzania akina Bashiru Ally, Polepole, Kitila Mkumbo na Anna Mgwira.

Hata kuamua kumshambulia mzalendo wa haki za madini Bwana Tundu Lissu na kisha Tundu Lissu kupita aliyoyapitia yote hiyo ni kwa njia ya Mungu. Wananchi wa Tanzania wanyonge kwa wenye nguvu, maskini kwa matajiri, wazee kwa vijanana wana CCM kwa wapinzani wote wanamtaka TUNDU ANTIPAS LISSU awe Rais wao kwa kipindi 2020-25.

Hakuna mwanadamu atakayeweza kupindisha alichopanga Mungu. Hata huyo Dr Wilson Charles Mahera atachakachua takwimu na kumtangaza Magufuli kuwa ndiye aliyeshinda lakini Magufuli kwa mapenzi ya Mungu hawezi kutawala Tanzania kuanzia kipindi hii cha 2020- 25.
 
Tume ambayo muundo wake nitokana mgombea mmoja wapo yaaani yeye ndiye anatengeneza timu yake ya ushindi kwakifupi NEC nitume ya CCM ambayo pia haishishirikishi vyama pinzani kwa uwazi
 
That was the case in 2015! Na wewe na wenzako wote hapo ufipa, mnajua kilichowapata. Mafuriko au nyomi SI HOJA!
 

..Ni kweli kabisa unachokisema.

..Nccr ya Mrema kilikuwa chama kichanga sana.

..Pia Watz wa mwaka 1995 walikuwa hawana imani, na mazoea, na mfumo wa vyama vingi.

..Sasa hivi mazingira kisiasa yamebadilika, na ni tofauti kabisa na ilivyokuwa mwaka 1995.

..Kwanza, wananchi wameukubali na wameuzoea mfumo wa vyama vingi vya siasa.

..Pili, vyama vya upinzani vina uzoefu mkubwa zaidi wa kushiriki uchaguzi kulinganisha na miaka iliyopita.

..Chadema kusimamisha wagombea ubunge 200+ na wa udiwani 3000+ ni ushahidi wa jinsi siasa zetu zilivyobadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…