Uchaguzi 2020 NEC: Wagombea muwe makini, tusilaumiane

Kwani Kuna wagombea vichaa?
Kama mgombea kiti cha urais hawezi kujaza fomu kwa usahihi, hafai
UKIKOSEA SPELLING TUU TUNAKUKNOCKOUT, MAANA UTAKUWA UNAUDHALILISHA UMMA WA WATANZANIA KUTOJAZA FOMU YAKO KWA UMAKINI
 
Hii tume haina Uhuru wowote, hawa wanapokea maelekezo kimyakimya toka ccm.kwa tume hii kazi bado mbichi...
 
Hazipendezi na zinaashiria mwanzo wa jammbo fulani lisilopendeza!
 
Da jamaa wewe una akili na Roho nziri Sana.
Hivi vijamaa vya CCM vimekaa kudhulumu tu.
 
Sina la kuongeza, baba...
 

Hilo la kuweka copy ni lazima, maana Tume huwa inaagizwa kuchezea fomu za wapinzani. Halafu sioni mantiki ya kukosea fomu kisha uenguliwe, badala ya kupewa nyingine ili ujaze kwa usahihi. Sehemu zote huwa kuna makosa kwenye ujazaji wa fomu, lakini sijawahi kuona ukinyimwa huduma, badala yake hupewa nyingine ili ujaze kwa usahihi.

Ni vyema vyama vya upinzani waangalie fomu zote, kisha kutoa muongozo kwa wagombea wake ili wajaze kwa usahihi. Huo ujazaji wa fomu unawekwa wa kuchanganya, ili wagombea hasa wa upinzani waenguliwe.
 
Hahahaaaaaaaa kukosea ndio moja ya kuonesha huwezi kazi.

Mwanafunzi anayefaulu vizuri haimaanishi kuwa amepata asilimia 100. Sasa kama mtu anaenguliwa eti kwa kuandika jina la mtaa kwa spelling error, kama sio upuuzi ni nini? Kibaya zaidi makosa hayo yanatumika kwa wapinzani tu, lakini ccm haihusiki. Ingekuwa mtu kakosea kwa asilimia zaidi ya 50 japo sawa. Sio huo upuuzi unaofanyika, na wakati mwingine wasimamizi wa uchaguzi, huongeza herufi zao ili kupata sababu ya kumuengua mtu hasa wa upinzani.
 
Mtuhakikishie kuwa wakurugenzi wa halmashauri hawatakimbia ofisi zao wakati wa kuchukua na kurudisha fomu, maana tunajua utawala wa awamu ya 5 ni waoga sana wa uchaguzi.
 
Huu ni mtego wa panya sitoshangaa ya UCHAGUZI SM YAKIJIRUDIA UCHAGUZI MKUU...
 
Inamaana hao wa Nchi zilizoendelea Walimu huwasaidia hadi kujibu mitihani?
 
Ndiyo,CHADEMA kuna mgombea chizi.
Angalia waweza kuwa unataka sifa au unasifiwa... ila ukichunga mdomo wako yaweza kuwa vema ili usitukanishe watu wenye hishma zao.
Je wanaojinadi ukichaa ni vichaa?
 
Inamaana hao wa Nchi zilizoendelea Walimu huwasaidia hadi kujibu mitihani?
Sijasema hivyo. Wanachofanya ni kuwaeleza wanafunzi mahitaji ya mtihani. Kwa mfano, kama mwanafunzi anatakiwa kutumia penseli badala ya peni kujibu maswali atawaambia hivyo na atahakikisha kila mwanafunzi ana penseli, na akikuona una tumia peni atakwambia usitumie na atakupa penseli. Kama mwanafunzi anatakiwa kuandika namba badala ya jina, atakusahihisha akiona umeandika jina lako. Hatakusaidia kujibu maswali kwa sababu hata kama umekosea kujibu swali ushiriki wako katika mtihani utatambulika.

Amandla...
 
Hivi tunachagua viongozi waende kutufanyia kazi za kujaza fomu au kuongoza na kuwaletea maendeleo?

Dosari za kujaza Fomu hazipaswi kuwa kigezo cha kuengua watu mahiri katika kutafuta nafasi za uongozi.

Kosa ktk fomu iwe Kama mjaza fomu kadanganya, au kaacha wazi maeneo muhimu. Lakini habari ya spelling ikipewa nafasi inatunyima haki ya kupata viongozi Bora. Na uwezekano wa fumu kiharibiwa Ni mkubwa.
 
Mchakato Huu ni sawa na ule wa uzabuni (Tendering). Bahasha haifunguliwi mpaka siku maalumu ya ufunguzi na ukaguzi iliyopangwa. Ndio maana wagombea wengine wanarudisha fomu siku ya mwisho wa mchakato kuzuia uwezekano wa siri zao za uongo walizojaza zisionekane wakawekewa mapingamizi. Vyama ndio vinatakiwa kuweka watu wa kuwasaidia wagombea wao kujaza fomu inavyotakiwa sio tume. Hiyo itakuwa sawa na kuitaka tume, ili kura zisiharibike, iweke watu wao vituoni kuwaelekeza wapiga kura namna ya kupiga kura zao. Mnataka kiingiza tume kwenye mgogoro wa kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…