Uchaguzi 2020 NEC yataka wagombea wasiwe na matokeo mfukoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea wanaowania nafasi za kuchaguliwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani, utakaofanyika wiki ijayo waache kuwa na matokeo mifukoni mwao, bali watambue kuna kushinda na kushindwa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Willson Mahera, alitoa tahadhari hiyo kwenye kongamano la amani, lililoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Twariga jijini Arusha.

Alitahadharisha kuwa wagombea wakiamini ni lazima watashinda, itasababisha vurugu na uvunjifu wa amani matokeo yakitoka tofauti na matarajio yao.

“Tatizo ninaloliona wapo baadhi ya wagombea wanakwenda kupiga kura wakijiaminisha tayari wameshashinda na inapotokea wameshindwa kihalali wanakataa matokeo,” alisema.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa dini, wa vyama vya siasa na wa mila wa makabila mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kusisitiza wananchi walinde amani wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Dk Mahera alisema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza wagombea watakaoshinda kihalali kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Aliwataka wagombea watakaoshindwa, wakubali matokeo na wasiwe sehemu ya kuanzisha vurugu.

“Mgombea yeyote atakayeshinda uchaguzi atatangazwa bila kujali anatoka chama kipi cha siasa hivyo wanaotaka kujitangaza kuwa wameshinda kabla ya upigwaji kura wanajidanganya,” alisema.

Dk Mahera alisema NEC itatenda haki kwa kila mgombea kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, katiba ya nchi, kanuni na taratibu za uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu madai kuwa matokeo ya baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani hubadilishwa, Dk Mahera alisema jambo hilo haliwezi kutokea kwa kuwa sheria hairuhusu kubadili matokeo ila kumtangaza mtu aliyeshinda kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wengine.

“Vyama vya siasa vitaweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura na wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kutangaza matokeo watashiriki kikamilifu, hivyo siyo rahisi mawakala wa vyama vyote wawepo kwenye vituo halafu matokeo ya kura kubadilishwa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi katika kongamano hilo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Naibu Katibu Mkuu wa Misioni na Uinjilisti, Jasson Kahembe, aliwataka wananchi kutambua kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo waepuke vurugu.

“Kuna maisha baada ya uchaguzi, Tanzania kwanza watu wasifikirie leo bali waangalie na kesho itakuwaje, neno la Mungu kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia linasema haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote,” alisema.

“Mungu aliwaahidi wana wa Israel kama watamsikiliza, kumtii na kufuata maagizo yake atawabariki, lakini pia aliwaambia watalaaniwa kama watakwenda kinyume na maagizo yake, hivyo taifa lenye utii mbele za Mungu hubarikiwa.”

“Tunapoelekea katika uchaguzi tutambue tunataka mafanikio ya Watanzania na siyo ya tunaowapenda, hivyo tuchague aina ya maisha tunayohitaji kuishi na siyo watu tunaowapenda sisi, pia tusifurahishwe na maneno mazuri ya wagombea wakiwa majukwaani kwa kuwa hizo ni harakati za kutafuta mchumba na uzuri, lakini ubaya wa mchumba hujulikana baada ya harusi,” alisema.

Msemaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Twariqa, Shehe Haruna Hussein aliwataka viongozi wa dini wasimame kwenye nafasi yao, wahubiri amani, wasiwe sehemu ya wanasiasa na wasiwachagulie wananchi mgombea, kwa kuwa wakifanya hivyo wanawagawa waumini.

“Viongozi wa dini hatupaswi kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kusema mgombea huyu anafaa kuwa kiongozi na mgombea mwingine hafai, naomba tuache wananchi wafanye uamuzi wao wenye kwenye sanduku la kura,” alisema Shehe Haruna.

HabariLeo
 
Bora chadema waambiwe kabisa maana watakufa na presha siku yakutangaza mshindi.
 
Anaeamini kuwa lazima ashinde ni huyu bwana bichwa kubwa wa kubebwa hapa[emoji116]
1583840766_1583840766-picsay.jpg
 
NEC ni mmoja kati ya taasisi zilizo na matokeo mfukoni, mpaka sasa ina wapiga kura 29m+ kutoka raia 59m+ wa nchi hii. Inawezekana vipi nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kupiga kura?

Pia inawezekana vipi watu wazima 18+ kwenye nchi, wakawa nusu sawa kabisa na walio chini ya 18+? NEC wamejiandaa kupika matokeo, kisha wanataka wakubaliane na matokeo ya tume iliyopika idadi ya wapiga kura.
 
Ni haki mgombea kupata nakala matokeo ili inapotokea kinyume awe na vielelezo kupinga.
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea wanaowania nafasi za kuchaguliwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani, utakaofanyika wiki ijayo waache kuwa na matokeo mifukoni mwao, bali watambue kuna kushinda na kushindwa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Willson Mahera, alitoa tahadhari hiyo kwenye kongamano la amani, lililoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Twariga jijini Arusha.

Alitahadharisha kuwa wagombea wakiamini ni lazima watashinda, itasababisha vurugu na uvunjifu wa amani matokeo yakitoka tofauti na matarajio yao.

“Tatizo ninaloliona wapo baadhi ya wagombea wanakwenda kupiga kura wakijiaminisha tayari wameshashinda na inapotokea wameshindwa kihalali wanakataa matokeo,” alisema.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa dini, wa vyama vya siasa na wa mila wa makabila mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kusisitiza wananchi walinde amani wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Dk Mahera alisema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza wagombea watakaoshinda kihalali kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Aliwataka wagombea watakaoshindwa, wakubali matokeo na wasiwe sehemu ya kuanzisha vurugu.

“Mgombea yeyote atakayeshinda uchaguzi atatangazwa bila kujali anatoka chama kipi cha siasa hivyo wanaotaka kujitangaza kuwa wameshinda kabla ya upigwaji kura wanajidanganya,” alisema.

Dk Mahera alisema NEC itatenda haki kwa kila mgombea kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, katiba ya nchi, kanuni na taratibu za uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu madai kuwa matokeo ya baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani hubadilishwa, Dk Mahera alisema jambo hilo haliwezi kutokea kwa kuwa sheria hairuhusu kubadili matokeo ila kumtangaza mtu aliyeshinda kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wengine.

“Vyama vya siasa vitaweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura na wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kutangaza matokeo watashiriki kikamilifu, hivyo siyo rahisi mawakala wa vyama vyote wawepo kwenye vituo halafu matokeo ya kura kubadilishwa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi katika kongamano hilo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Naibu Katibu Mkuu wa Misioni na Uinjilisti, Jasson Kahembe, aliwataka wananchi kutambua kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo waepuke vurugu.

“Kuna maisha baada ya uchaguzi, Tanzania kwanza watu wasifikirie leo bali waangalie na kesho itakuwaje, neno la Mungu kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia linasema haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote,” alisema.

“Mungu aliwaahidi wana wa Israel kama watamsikiliza, kumtii na kufuata maagizo yake atawabariki, lakini pia aliwaambia watalaaniwa kama watakwenda kinyume na maagizo yake, hivyo taifa lenye utii mbele za Mungu hubarikiwa.”

“Tunapoelekea katika uchaguzi tutambue tunataka mafanikio ya Watanzania na siyo ya tunaowapenda, hivyo tuchague aina ya maisha tunayohitaji kuishi na siyo watu tunaowapenda sisi, pia tusifurahishwe na maneno mazuri ya wagombea wakiwa majukwaani kwa kuwa hizo ni harakati za kutafuta mchumba na uzuri, lakini ubaya wa mchumba hujulikana baada ya harusi,” alisema.

Msemaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Twariqa, Shehe Haruna Hussein aliwataka viongozi wa dini wasimame kwenye nafasi yao, wahubiri amani, wasiwe sehemu ya wanasiasa na wasiwachagulie wananchi mgombea, kwa kuwa wakifanya hivyo wanawagawa waumini.

“Viongozi wa dini hatupaswi kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kusema mgombea huyu anafaa kuwa kiongozi na mgombea mwingine hafai, naomba tuache wananchi wafanye uamuzi wao wenye kwenye sanduku la kura,” alisema Shehe Haruna.

HabariLeo
Binti mahera akichakachua matokeo , asilalamike kwa litakalompata
 
NEC ni mmoja kati ya taasisi zilizo na matokeo mfukoni, mpaka sasa ina wapiga kura 29m+ kutoka raia 59m+ wa nchi hii. Inawezekana vipi nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kupiga kura? Pia inawezekana vipi watu wazima 18+ kwenye nchi, wakawa nusu sawa kabisa na walio chini ya 18+? NEC wamejiandaa kupika matokeo, kisha wanataka wakubaliane na matokeo ya tume iliyopika idadi ya wapiga kura.
Kwa akili za kawaida watoto lazima wawe wengi kuliko wazazi wao au watu wazima! Ni Tanzania pekee ambayo watoto na watu wazima idadi yao ni sawa!
 
Kabisa, halafu hiyo tume inataka tukae pembeni tuamini matokeo watakayotoa. Kama wameweza kupika idadi ya wapiga kura, watashindwa kupika matokeo?
 
Kitu cha ajabu ni kuwa si Tume ya Uchaguzi wala viongozi wa dini wanaosema cho chote kuhusu HAKI!
 
NEC ni mmoja kati ya taasisi zilizo na matokeo mfukoni, mpaka sasa ina wapiga kura 29m+ kutoka raia 59m+ wa nchi hii. Inawezekana vipi nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kupiga kura? Pia inawezekana vipi watu wazima 18+ kwenye nchi, wakawa nusu sawa kabisa na walio chini ya 18+? NEC wamejiandaa kupika matokeo, kisha wanataka wakubaliane na matokeo ya tume iliyopika idadi ya wapiga kura.

Kwanini swali kuhusu hizi takwimu huwa hawaulizwi NEC na waandishi wa habari ama vyama vya siasa vishiriki ili kujua ukweli na uhalali wa takwimu hizi?

Na mwaka 2015 hivi kulikuwa na wapiga kura wangapi halali walioandikishwa?

Kati ya 2015 na 2020 wameongezeka wangapi? Projection ya ongezeko hili in relation to the county's total population ikoje agewise? Je ingezeko hili linakubalika?

Maana kwa mfano tu;

Kama ongezeko ni wapiga kura 9,000,000 toka 20,000,000 wa mwaka 2015 na kuwa 29,000,000..

Swali litakuwa ongezeko hili linawiana na population yenye sifa za kuwa wapiga kura ambao mwaka 2015 hawakuwanazo hizi sifa..?

Basically, hata mimi takwimu hizi za NEC zinanipa mashaka makubwa. Siziamini hata kidogo..!

Ni eneo lingine hatari na lililojificha na wanaotaka kushinda kwa nguvu watalitumia kuiba kura..!!
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea wanaowania nafasi za kuchaguliwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani, utakaofanyika wiki ijayo waache kuwa na matokeo mifukoni mwao, bali watambue kuna kushinda na kushindwa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Willson Mahera, alitoa tahadhari hiyo kwenye kongamano la amani, lililoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Twariga jijini Arusha.

Alitahadharisha kuwa wagombea wakiamini ni lazima watashinda, itasababisha vurugu na uvunjifu wa amani matokeo yakitoka tofauti na matarajio yao.

“Tatizo ninaloliona wapo baadhi ya wagombea wanakwenda kupiga kura wakijiaminisha tayari wameshashinda na inapotokea wameshindwa kihalali wanakataa matokeo,” alisema.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa dini, wa vyama vya siasa na wa mila wa makabila mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kusisitiza wananchi walinde amani wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Dk Mahera alisema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza wagombea watakaoshinda kihalali kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Aliwataka wagombea watakaoshindwa, wakubali matokeo na wasiwe sehemu ya kuanzisha vurugu.

“Mgombea yeyote atakayeshinda uchaguzi atatangazwa bila kujali anatoka chama kipi cha siasa hivyo wanaotaka kujitangaza kuwa wameshinda kabla ya upigwaji kura wanajidanganya,” alisema.

Dk Mahera alisema NEC itatenda haki kwa kila mgombea kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, katiba ya nchi, kanuni na taratibu za uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu madai kuwa matokeo ya baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani hubadilishwa, Dk Mahera alisema jambo hilo haliwezi kutokea kwa kuwa sheria hairuhusu kubadili matokeo ila kumtangaza mtu aliyeshinda kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wengine.

“Vyama vya siasa vitaweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura na wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kutangaza matokeo watashiriki kikamilifu, hivyo siyo rahisi mawakala wa vyama vyote wawepo kwenye vituo halafu matokeo ya kura kubadilishwa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi katika kongamano hilo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Naibu Katibu Mkuu wa Misioni na Uinjilisti, Jasson Kahembe, aliwataka wananchi kutambua kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo waepuke vurugu.

“Kuna maisha baada ya uchaguzi, Tanzania kwanza watu wasifikirie leo bali waangalie na kesho itakuwaje, neno la Mungu kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia linasema haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote,” alisema.

“Mungu aliwaahidi wana wa Israel kama watamsikiliza, kumtii na kufuata maagizo yake atawabariki, lakini pia aliwaambia watalaaniwa kama watakwenda kinyume na maagizo yake, hivyo taifa lenye utii mbele za Mungu hubarikiwa.”

“Tunapoelekea katika uchaguzi tutambue tunataka mafanikio ya Watanzania na siyo ya tunaowapenda, hivyo tuchague aina ya maisha tunayohitaji kuishi na siyo watu tunaowapenda sisi, pia tusifurahishwe na maneno mazuri ya wagombea wakiwa majukwaani kwa kuwa hizo ni harakati za kutafuta mchumba na uzuri, lakini ubaya wa mchumba hujulikana baada ya harusi,” alisema.

Msemaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Twariqa, Shehe Haruna Hussein aliwataka viongozi wa dini wasimame kwenye nafasi yao, wahubiri amani, wasiwe sehemu ya wanasiasa na wasiwachagulie wananchi mgombea, kwa kuwa wakifanya hivyo wanawagawa waumini.

“Viongozi wa dini hatupaswi kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kusema mgombea huyu anafaa kuwa kiongozi na mgombea mwingine hafai, naomba tuache wananchi wafanye uamuzi wao wenye kwenye sanduku la kura,” alisema Shehe Haruna.

HabariLeo
NEC msijihami. Kwa nini nanyi mna matokeo yenu mfukoni?
 
Kwanini swali kuhusu hizi takwimu huwa hawaulizwi NEC na waandishi wa habari ama vyama vya siasa vishiriki ili kujua ukweli na uhalali wa takwimu hizi?

Na mwaka 2015 hivi kulikuwa na wapiga kura wangapi halali walioandikishwa?

Kati ya 2015 na 2020 wameongezeka wangapi? Projection ya ongezeko hili in relation to the county's total population ikoje agewise? Je ingezeko hili linakubalika?

Maana kwa mfano tu;

Kama ongezeko ni wapiga kura 9,000,000 toka 20,000,000 wa mwaka 2015 na kuwa 29,000,000..

Swali litakuwa ongezeko hili linawiana na population yenye sifa za kuwa wapiga kura ambao mwaka 2015 hawakuwanazo hizi sifa..?

Basically, hata mimi takwimu hizi za NEC zinanipa mashaka makubwa. Siziamini hata kidogo..!

Ni eneo lingine hatari na lililojificha na wanaotaka kushinda kwa nguvu watalitumia kuiba kura..!!

Hii idadi ya wapiga kura ni ya kupika, na ndio maana NEC hawataki watu walinde kura, na sasa kuruhusu matumizi ya passport, driving license nk kupigia Kura. Hii ya yote ni kuhakikisha yanapatikana matokeo waliyoyapanga.
 
Duu sensa ya ajabu kabisa Wakubwa na Watoto 50/50 hata huko Japani kwenye uzazi wa mpango hamna hiyo
 
Back
Top Bottom