Uchaguzi 2020 NEC yavitahadharisha Vyama vya Siasa na Wagombea kuhusu uvunjifu wa Sheria za nchi

Uchaguzi 2020 NEC yavitahadharisha Vyama vya Siasa na Wagombea kuhusu uvunjifu wa Sheria za nchi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wakati vyama vya siasa nchini vikiendelea na zoezi la kuomba kuchaguliwa na wananchi kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Tume ya uchaguzi NEC ivitahadharisha vyama hivyo kutofunja dheria za nchi kwa kigezo cha uchaguzi.

Katika hotuba ya Mwenyekiti wa NEC iliyosomwa na Mkurugenzi wa Mipango, ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Adam Mkina wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RAS Kagera octoba 05, mwaka huu, ameeleza kuwa pamoja na masuala yote ya uchaguzi suala la utulivu na amani vinatakiwa kupewa kipaumbele.

Amesema kuwa Tume imekuwa ikisisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao, ikiwemo kuepuka lugha za kashfa maneno ya uchochezi yanayotishia amani na usalama wa nchi pamoja na kuhakikisha wanaepuka kufanya kampeni ambazo zinaashiria ubaguzi katika misingi ya jinsia, ulemavu, ukabila, udini, maumbile au Rangi.

“Tunaendelea kuwasisitiza vyama na wagombea kuwa kunapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo,kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliyowekwa na sio kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.” Amesisitiza Adam

Mkina ameongeza kuwa Tume inaendelea kuratibu kusimamia na kuendesha Uchaguzi huu kwa kutumia Sheria za Uchaguzi, ambapo amesisitiza kuwa vyama vya siasa wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki, sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama matamshi ambayo yanaweza sababisha vurugu kwa kisingizio cha Uchaguzi.

Aidha ameongeza kuwa katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umewezesha daftari hilo kuwa na jumla ya wapiga kura 29,188,347 nchi nzima, ambapo pia wagombea kutoka vyama vya siasa 15 waliteuliwa na kugombea nafasi za U rais huku wawili kati yao wakiwa wanawake pamoja na wanawake 5 kuteuliwa kuwa wagombea wenza.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi manispaa ya Bukoba ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amewahakikishia wananchi wa Manispaa hiyo kuwa Uchaguzi utakuwa wa huru na haki hivyo wanao wajibu wa kujiokeza kupiga kura kwa ajili ya viongozi wanaowataka.

Mkutano huo umewakutanisha wadau ambao ni waandishi wa habari, vongozi wa dini, asasi za kiraia, watu wenye ulemavu na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na elimu ya mpiga kura.
 
Kila nikiangalia, mahesabu yangu yananiambia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020MAGUFURI anapigwa asubuhi na mapema tu

1. Kura za Kaskazini zitamkataa vibaya mno
2. Kura za kusini zitamkataa katakata....
Nani alikuambia Africa madaraka yanaachiwa kwa kipande cha karatasi.......waambieni hao wabelgiji wajipange vizuri tarehe 28 tunabaki na mkimbizi wao
 
NEC wajitathimini kwanza wao wenyewe wanapofanya kazi zao kwa kufuata matakwa ya watawala na CCM huo siyo uvunjaji wa sheria?.
 
Kila nikiangalia, mahesabu yangu yananiambia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020MAGUFURI anapigwa asubuhi na mapema tu

1. Kura za Kaskazini zitamkataa vibaya mno
2. Kura za kusini zitamkataa katakata...
Nami natoa ramli yangu,Magufuli na CCM watashinda na baada ya uchaguzi Magufuli atabadilka sana.Zanzibar itakuja Jecha part two na pre emptying itakayofanyika hakuna atayeketoka nje kwa siku tatu!!!
 
Nami natoa ramli yangu,Magufuli na CCM watashinda na baada ya uchaguzi Magufuli atabadilka sana.Zanzibar itakuja Jecha part two na pre emptying itakayofanyika hakuna atayeketoka nje kwa siku tatu!!!
Naam ndugu MIGNON nakubaliana na utabiri wako, isipokuwa hapo kwenye Magufuli kubadilika, tafadhali fafanuwa atakuwa mbaya zaidi?( kwangu mimi naona tayari ni mbaya/ hafai) au atakuwa mzuri?
 
Nani alikuambia Africa madaraka yanaachiwa kwa kipande cha karatasi.......waambieni hao wabelgiji wajipange vizuri tarehe 28 tunabaki na mkimbizi wao
Katibu mkuu wizara ya Elimu, Dkt Avemaria Semakafu amesema wizara imefuta mafunzo ya ualimu wa S/M ngazi ya cheti

Baada ya saa sita

Rais Propesa. Magu amewataka walimu kupuuza taarifa ya kipumbavu inayoeleza kuwa serikali imefuta mafunzo ya ualimu S/M ngazi ya cheti

Ukisikia utawala uliofitinika basi ni huu wa Jiwe
 
Nani alikuambia Africa madaraka yanaachiwa kwa kipande cha karatasi.......waambieni hao wabelgiji wajipange vizuri tarehe 28 tunabaki na mkimbizi wao
Kwahiyo unashauri wananchi waingie barabarani kwakuwa CCM haiwezi kuachia madaraka kwa kushindwa uchaguzi?
 
Katibu mkuu wizara ya Elimu, Dkt Avemaria Semakafu amesema wizara imefuta mafunzo ya ualimu wa S/M ngazi ya cheti

Baada ya saa sita

Rais Propesa. Magu amewataka walimu kupuuza taarifa ya kipumbavu inayoeleza kuwa serikali imefuta mafunzo ya ualimu S/M ngazi ya cheti

Ukisikia utawala uliofitinika basi ni huu wa Jiwe
Mbele kwa mbele nini Dhambi kwa mwenyeziiii....
 
Mbele kwa mbele nini Dhambi kwa mwenyeziiii....
“You don't necessarily need atomic bombs to destroy a nation. Politicians who value their pockets than the life of citizens always do that every day.” ~ Israelmore Ayivor
 
Kuna mgombea anawafokea wapiga kura kwamba atawashughulikia wasipomchagulia awatakao, anatumia kilugha, anasimama njiani kuwasalimia watu, anatoa ahadi za uongo, anatukana watu, anatoa rushwa hapa NEC wanasaemaje.
 
“You don't necessarily need atomic bombs to destroy a nation. Politicians who value their pockets than the life of citizens always do that every day.” ~ Israelmore Ayivor
Don't ask what your nation will do for you, ask yourself what will you do for your nation.......
 
Nani alikuambia Africa madaraka yanaachiwa kwa kipande cha karatasi.......waambieni hao wabelgiji wajipange vizuri tarehe 28 tunabaki na mkimbizi wao
Amini amini nakwambia jiandae kumuona Tundu Antiphas Lissu akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 
Wanazungumza kwa kuuzunguka mbuyu. Kama kweli wanamaanisha wamite Rais Magufuli wamhoji kwa nini anaendesha siasa zenye harufu ya ubaguzi. Namna nyingine, NEC inachofanya ni unafiki mkubwa.

Ukienda kwenye uhalisia, ukweli ni kuwa mgombea wa CCM na NEC, ni hatari kwa umoja wa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom