NECTA kwa kushirikiana na serikali naona mnaenda kuizika rasmi elimu ya Tanzania

NECTA kwa kushirikiana na serikali naona mnaenda kuizika rasmi elimu ya Tanzania

Inatekelezeka vizuri,siasa zinaiharibu nchi.
Ni bora tungejikita kuboresha miundombinu ya shule zetu&maslahi ya wataalamu wetu,kabla ya kutoa elimu bure.
Cheki shule za private&hizi za serikali,kuna tofauti katika miundombinu&maslahi kwa wafanyakazi wao.
Tunavuna tunachopanda.
Yah
 
Shida ni kwamba hao hao walimu wanatumika sn kipindi cha uchaguz kuiba kura...
Hilo nalo shida mana kwenye kaz za kijinga ndo mwalimu anatumika zaid na wala hata hashtuki

Yeye anachojali ni vi ujira vidogo vidogo ili kukidhi maisha yake
 
Moja kata ya vyama vilivyoshindwa timiza wajibu wake ni hio cwt
CWT Itafanya kazi gani wakati chama hicho kilishakufa watu badala ya kusimamia maslahi ya walimu wao wanagombania posho,hk chama ni cha kijinga sana,kimejaa ugolo mtupu.
 
Hii nchi huwezi kuielewa kabisa hv serikali imewatuma huyu waziri wa Elimu kutengeneza waraka mpya unaokuja na kitu ambacho wao wanaita ni maboresho wakati kwenye mambo mengi failure ni kubwa hasa kwenye Elimu
 
Heri ya mwaka mpya kwa wadau wote,tumshukur Mungu hasa kwa yote anayoendelea kutujalia

Wadau wengi ukiwauliza kuhusu matatizo na changamoto za elimu ya Tanzania bas watakutajia upungufu wa walimu, upungufu wa miundombinu kama madarasa, vyoo n.k

Lkn najua wengi wetu hatujaingia ndani kabisa na kujua matatizo mengine zaidi.
Nikiwa katika harakati za matembezi yangu ya mwisho wa mwaka, safari hii nilibahatika kukutana na baadhi ya waalimu kama sita wa masomo tofauti nadhan walikua tayari wametoka kwenye uchakataji wa mwisho wa vijana wetu wa kidato cha pili na nne.

Kama mdau wa elimu niliyoyasikia kupitia hao walimu kama ni kweli basi elimu yetu haipo mwisho kabla haijaanguka kabisa na kuzikwa rasmi.

Mimi kipindi hicho nilikuwa nikisika mwalimu kapata nafas ya kwenda kufanikisha hatua muhimu kabisa ya vijana wetu bas nilikua nawaonea wivu kwelikweli mana nilijua lazima maslah yatakuwa bora kwelikweli lkn hadi pale nilivobahatika kukaa na hao walimu sita wa masomo tofauti na hapo ndio nikagundua bado kuna tatizo la msingi sn na kama serikal na NECTA wakileta masihara bas tunaenda kuizika rasmi elimu yetu.

Hivi tunaweza amin kwamba hawa walimu licha ya kwamba inaitwa kaz maalumu lkn eti mwisho wa siku huyu mwalimu anapewa sh laki tano (500,000)ya kazi licha ya kufanyishwa kazi siku nzima hadi usiku.

Kwa masikitiko niliyoyaona kupitia walimu hawa naamini wanaenda huko kwa sababu hawana cha kufanya lkn pia hawana furaha kabisa na hicho kinachoitwa kaz maalumu na mwisho wa siku naona siku zijazo kuna uwezekano kazi hii ikawa inafanywa tu irimradi na hivo kupoteza weledi wote na hivo mwisho wa siku kupata watoto ambao uwezo wao haueleweki.

Yan hata tu zile posho mpya zilizotangazwa na serikali hivi karibun pia hawa walimu hawajapewa kwa kisingizio kuwa bado hazijaanza fanya kaz lkn cha ajabu kada nyingine kama polisi, wanajeshi, watendaji, madaktari na wengineo wanaendelea kulipwa hizo posho mpya lkn inapokuja suala la mwalimu kulipwa kila mtu analeta uhuni usiokuwa na maana kana kwamba mwalimu sio mtumishi wa nchi hii.

Walimu hawa pia wanadai kumbe inaonekana kila mwalimu kwa siku katengewa kama sh25000 au 30,000 kama sikosei hio ni kwa ajili ya chakula, vinywaji na malazi lkn cha ajabu kinachofanyika hakilingani kabisa na hio pesa yan kila mtu anataka kupiga hapo hapo.

Mimi naamini serikali inatoa hela nyingi sn tena kwenye tukio la muhimu kama hilo la kumalizia kuwachuja vijana wetu lkn najua kuna watu wachache sana wanatake advantage kitu ambacho si sahihi.

Hivi kweli unamtoa mtoto wa mtu Ruvuma huko unakuja kumpa shilingi laki sita sijui saba au tano hela ambayo amezoea kuipata kwenye mitihani yao ya ndan ya MOKO lkn unakuja kumpa huyu mwalimu bila kuangalia athari zake mbelen.
Tena mbaya zaidi hela yenyewe inatolewa mwishon wakati kazi imeisha kitu ambacho kinaonesha kutojiamin na kuficha ukweli makusud mana kama mnajiamin na kazi yenu kwanini msiwaambie hao walimu mwanzon kabisa wa kazi kiwango watakachopokea had hio kaz inakuja kuisha na kwanini mnafanya siri kwenye tukio muhimu la nchi kama hilo maana ndo sehem pekee ambapo maisha ya vijana wetu yanaandaliwa lkn watu wanaleta uhuni kana kwamba hawajui athari zake.

Ni wakati wa serikali kwa kushirikiana na NECTA kuanza kulipa umuhimu mkubwa wa kimaslahi suala hili nyeti la nchi ili kuongeza weledi zaid na kupata vijana kweli wenye sifa na wanaostahili lkn ikiwa tu watazingatia utulivu wa akili kwa mwalimu huyu kwa kujitahidi angalau kutimiza maslahi yao kama inavyotakiwa.

Mwanajeshi anakwenda kulinda aman nje anapewa hela nzur ni kwa sababu anashika silaha lkn huyu mtu anaetengeza watoto wetu kila siku tunashindwa mpa hata milion 2 kweli tunaishia kumpa malaki tano sijui sita huko.

Kama imeshindikana na inaonekana labda kwenye elimu kuna mzigo mkubwa pelekeni mapendekezo ya sisi wazazi kuchangia sh 5000 kwa mtihani wa kidato cha nne na sh3000 kwa mtihani wa kidato cha pili ili angalau kukidhi baadhi ya mahitaji ya hawa wataalamu wetu.

Hii haikubaliki jamani hebu hawa wataalamu wetu waanze kutazamwa kwa jicho la tatu mana tunachokitafuta tutakuja kukipata baada ya miaka 15 au 20 mbeleni huko

Mana kuna msemo usemao taifa linalodharau elimu ni taifa linalojichimbia kifo chake chenyewe

Naomba kuwasilisha kama mdau muhimu wa elimu
Unawatetea wezi wa kura za 2020, acha wafe tu Kwa stress siwapendi hatari
 
Labda awe waziri ndoanamark, anyway iko hivi mwalimu kupata million moja ni mpaka akakope tu hakuna sehemu yoyote ya kazi yake atatunza au kupokea million
Mkuu unayosema ni kweli kabisa. Ila kwenye suala la marking pale barazani wanakunja zaidi ya m2 na hiyo ndiyo kazi pekee ya mwalimu inayompa pesa nyingi.

Kumbuka pia kazi hiyo sio nyepesi maana wengi wakitoka huko hufikia kulazwa kwanza kwa kutumika kupita kiasi.
 
Cha ajabu unakuta mwalimu kahonga kupata hio nafasi au katoa mbususu mwezi mzima kwa Mkuu wa shule, mratibu au afisa elimu Kwa ahadi hio, au akiwa huko center ya marking kaluwa mbususu na wasimamizi kwa ahadi ataendelea kushiriki hilo zoezi., wengine wanaroga na kuiba nyota ili wapate wao.
Mungu awasaidie hao walimu,
 
Kupata nafasi yenyewe kwa connection, utasikia tunaenda Bukoba mwaka huu, ila walimu wanasikitisha sana
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa. Ila kwenye suala la marking pale barazani wanakunja zaidi ya m2 na hiyo ndiyo kazi pekee ya mwalimu inayompa pesa nyingi.

Kumbuka pia kazi hiyo sio nyepesi maana wengi wakitoka huko hufikia kulazwa kwanza kwa kutumika kupita kiasi.
Wewe upo Nchi Gani ?? Unaropoka tu marking anaepewa pesa nyingi ni laki 9 tuu hata 1M hakuna anayepata.

Labla kama unazungumzia Makatibu wakuu.
 
CWT Itafanya kazi gani wakati chama hicho kilishakufa watu badala ya kusimamia maslahi ya walimu wao wanagombania posho,hk chama ni cha kijinga sana,kimejaa ugolo mtupu.
Cwt ni ukoo wa panya wameshindwa jua wajibu wao kazi yao kubwa saiz ni kupambana kila mtu apate chake
 
Hii nchi huwezi kuielewa kabisa hv serikali imewatuma huyu waziri wa Elimu kutengeneza waraka mpya unaokuja na kitu ambacho wao wanaita ni maboresho wakati kwenye mambo mengi failure ni kubwa hasa kwenye Elimu
Serikali lazima ibadilike sn la sivo elimu ina hali mbaya
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa. Ila kwenye suala la marking pale barazani wanakunja zaidi ya m2 na hiyo ndiyo kazi pekee ya mwalimu inayompa pesa nyingi.

Kumbuka pia kazi hiyo sio nyepesi maana wengi wakitoka huko hufikia kulazwa kwanza kwa kutumika kupita kiasi.
Tupe ushuhuda kaka,hizo milion 2zinatoka wapi
 
Back
Top Bottom