NECTA, kwanini msitumie teknolojia ya malipo kwa wasimamizi wa mitihani ili kuepusha malalamiko kama mkoani Tabora?

Waalimu wanajidhalilisha sana, tujifunze kutumia vizuri mitandao, njaa ya sh 5000 unadhalilisha taaluma nzima, na umeambiwa pesa zipo utalipwa, we tayari kwenye mitandao. Inaonyesha JPM haku wa displine vya kutosha, mnasababisha watu watamani JPM mwingine
 
Sasa shida ya walimu baadhi wakishalipwa Either hawaj au wanakuja wamelewa katika seminar...rejea zoez la sensa baada ya malipo ya kwanza kuna watu waliondolewa kutoka a na ulevi
 

NECTA, wakitumia teknolojia ya malipo itaiokolea serikali ya Tanzania zaidi ya Bilion 900 zinazoibiwa na ofisi Za elimu mkoa na wilaya nchi nzima.​

Hiki ni chanzo kikubwa cha wizi wa fedha Za serikali.​

Pili ifike mahali sasa mitihani ya darasa la saba ifutwe Ili Wanafunzi wakurane na mtihani wa kidato cha pili na Kuendelea.​

Wizi mkubwa na upotevu wa fedha ni mtihani wa darasa la saba nchini Tanzania.​

 
Na wenyewe ndiyo kipindi chao cha mavuno hicho.
Yaani kama Dar Jamani wamezidi semina 50k Ila msishangae kulipwa 40k mkaambiwa elf10 mtalipwa nadai elf 10 zangu km mbili hivi na elf 5 pia
Kiukweli kama wanasoma hapa wajue kabisa Maafisa elimu mradi wao mkubwa ni necta walimu wanapigwa Sana

Kwenye usimamizi mikoani kama shule Ina siku 11 wasimamizi mtalipwa Pesa ya siku 11 yotee bil shida hata km mko 10 ,Ila dar Sasa mnapunguzwa Kila siku mnajikuta mmebaki wawili au Mmoja wakati Necta wanatoa Pesa Kulingana na idadi ya siku na idadi ya vyumba Vya mitihani vilivyopo shuleni...
Sijuagi Hawa Viongozi wanatuhi saa ngapi hizi dhulma
 
Taasisi za serikali zinaogopa sana teknolojia katika kutekelezwa majukumu yao!

Ni kama Baba mkwe!! sijui KWA nini aiseh!
 
Nasikia kwenye mtihani wa darasa la saba walilipwa semina 40000/= badala ya 50000/= HUKO Tabora pia nauli sh. 5000 wakati kuna wale wa kanda maalumu!

Juzi kwenye semina ya Darasa la nne wametangaziwa kulipwa 25000/= usimamizi KWA siku mbili sawa na 50000/=,Sasa hawaelewi Ndio muongozo au fix!

Hata form four imekuwa 30000/= KWA 35000/= msimamizi mkuu! Na practicals waandaaji 40000/= ngoja waone hatma yao!!
 
Kwani mleta mada kuja na mapendekezo ya Namna ya kuzuia upigaji na kuepusha malalamiko kama haya amedhalilisha nini katika taaluma yake hata kama ni Mwalimu kweli!!?

Ifike hatua tuwe wakweli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…