Necta na wizara ya elimu mbona siwaelewi?

Necta na wizara ya elimu mbona siwaelewi?

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
Wizara ya elimu imekua inasisitiza kuwa mitihani ya siku hizi inapima uelewa zaidi kuliko kukariri.
Na necta nao wakitoa matokeo watoto wamefaulu na division 1 za hatari kuliko zamani.
Sasa kama hawa watoto wamepimwa uelewa na wamefaulu kwa 1 za 7 na 1 za 3 za kutosha ina maaana wanajua thermodynamics, mechancs, anatomy, organic chemistry, electronics, calculus, algebra n.k
Kama hawa watoto wanaelewa haya mambo kwa upana mkubwa tofauti na sisi kizazi cha mchiki down kwanini maendeleo yetu kwenye science ni madogo mno?
Vifaa pamoja na taaluma zote za kisayansi tuna import kutoka nje, Je elimu yetu ya sayansi haina maana na tuache kuwasukuma watoto wenye akili kwenda huko au shida nini?
 
Hayo maendeleo ya Technology yahojiwe baada ya miaka 10 mtoto aliefaulu sana jana huwezi kumuhoji kuhusu maendeleo ya Technology leo.

Japo uhakika ni kuwa mfumo wa elimu tunaotumia haiwezi ku contribute chochote kwenye maendeleo ya Technology
 
Muhudumu
Ongeza glasi
Acha nilewe
Nilewe tu
Nileeeeeeeeeewe
Nilewe tu.
 
Hayo maendeleo ya Technology yahojiwe baada ya miaka 10 mtoto aliefaulu sana jana huwezi kumuhoji kuhusu maendeleo ya Technology leo.

Japo uhakika ni kuwa mfumo wa elimu tunaotumia haiwezi ku contribute chochote kwenye maendeleo ya Technology
Mada kama hizi ni muhimu sana kuwa mjadala mkubwa wa kitaifa.
Lakini ninajua kwa aina ya elimu tuliyo nayo,wasomi wengi hawavutiwi na mijadala ya kuchambua ubora wa elimu yetu.

Kama kuna ukweli mchungu tu,ni kwamba tuko chini ya utumwa mzito kielimu na ni mfumo uliotengenezwa kuwafanya mamilioni ya watu tutawaliwe.

Kuna siri watu weupe wachache wanaijua kuhusu elimu ambayo sisi hata wenye PhD hawaijui.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Hayo maendeleo ya Technology yahojiwe baada ya miaka 10 mtoto aliefaulu sana jana huwezi kumuhoji kuhusu maendeleo ya Technology leo.

Japo uhakika ni kuwa mfumo wa elimu tunaotumia haiwezi ku contribute chochote kwenye maendeleo ya Technology
Kabla ya hiyo miaka 10, wahadhiri wanalalama watoto hawafundishiki! Wanaotamani chuo pia kuwe na twisheni
 
Sasa mtoto kafaulu mwaka huu unataka uone maendeleo gani … nyinyi mliosoma zamank ndio mngeonyesha tofauti
 
Back
Top Bottom