NECTA Wasalimu amri, mitihan ya kidato cha 4 sasa kurudiwa upya.

Hahaha warudie hahaha haijatangazwa popote pale
 
Wakuu hebu msiwe walalamishi ktk kila jambo, kwa mwenye macho ataona kuwa ni kweli NECTA wamefanya uzembe ktk usahihishaji wa mitihani hiyo, kumbukeni hata madai ya waislamu ktk somo la islamic knowledge, ambapo baada ya kurudiwa tukashuhudia wanafunzi waliopata F wakapa B na wengine A kabisa na C, tukubali tukatae NECTA ni wazembe sana mfano pia kuna kituo cha mtihan kina wahitimu 600 lakin hakuna hata C zinazozidi 15.
 
wewe habari umezitoa wapi?

Mkuu usiwe mvivu wa kusoma, huko nyuma nimeandika source kuwa ni gazeti la habari leo uk 4, Pia kahama Fm wametangaza habari hii na kama we ni tomaso huamin mpaka uone subiria habari ya saa2 usiku uone.
 
You said it very well. Tuna hizo kesi za wanafunzi kufika chuo kikuu wakiwa hawajui hata kuandika essay. hilo ni tatizo na tumekuwa nalo hili kwa muda mrefu sana. Ila sasa ndiyo hivyo, inaonekana bado hakujagunduliwa mechanism ya kushughulikia hilo tatizo. Lakini kama pia tutaacha hawa wanafunzi 250000 waingie mitaani bila vyeti, itakuwa ni hatari zaidi, kama hatuwezi kuwarudisha wafanye tena mtihani basi hata tushushe passmarks. Kwa maana ya baadala ya div 4 kuanzia marks 40 ianzie 30 na ziro ianzie 20 au 10, ili angalau wale waliojaribu japo kujibu maswali kadhaa wapandishwe kidogo na kupata vyeti vya kuwapeleka hata kusomea ufundi.
Hata mimi napenda sana vijana wasiwe mitaani ni hatari sana, ila cha muhimu ni wao waje na SCIENTIFIC REASONS kwanini hali hii imejitokeza, kutokujua chanzo cha tatizo ni tatizo kubwa sana kuliko hata hilo tatizo lenyewe, hicho unachokisema kuhusu kushusha marks nahisi kimefanyika ila ndio hivyo tena bado hali ilikuwa mbaya wakaona hawana jinsi ni bora tu kutangaza kwanini huko chini wanaweza fanya hivyo washindwe kwa form 4, ila wasiwasi wangu wakifanya haya ya kushusha unaweza jikuta unaletewa wanafunzi sio tu kutokujua kuandika essay ila wasio jua kusoma kabisa kama tatizo hilo wanavyolalamika baadhi ya walimu wa sekondari, si unajua shule ni mwendelezo unapo mpitisha hapa ujue anakwenda ngazi nyingine
 
walekebishe na mishahara ya waalimau,pamoja na mazingira ya kufundishia,lasivyo watakuwa wanacheza malida each year! Chezea mateacheri ww.pamoja pamoja hadi kieleweke!

Mkuu hebu acha ujinga na harakati za kipumbavu yani we unasema hadi kielweke na wakati haya ni maisha ya watu, siku nyingine usirudie huu utumbo wako.
 
Kutokana na ufahulu mbaya wa wanafunzi wa kidato cha 4 wa mwaka 2012, sasa mitihani hiyo kurudiwa upya na serkali itagharamia gharama zote na hii ni kwa ajili ya kuliepusha taifa aibu ambayo haijawahi tokea nchini kwa anguko la elimu.

Mods naomba msihamishe habari hii wala kunipiga ban, Mimi ni mjumbe tu na mjumbe siku zote hafi.
Mungu ibariki Tanzania.

Inarudiwa kusahihishwa au kufanywa? Kama ni kufanywa huyo alieyamua hivyo atakuwa ana matatizo makubwa sana ya kimaamuzi
 
Wakuu hebu msiwe walalamishi ktk kila jambo, kwa mwenye macho ataona kuwa ni kweli NECTA wamefanya uzembe ktk usahihishaji wa mitihani hiyo, kumbukeni hata madai ya waislamu ktk somo la islamic knowledge, ambapo baada ya kurudiwa tukashuhudia wanafunzi waliopata F wakapa B na wengine A kabisa na C, tukubali tukatae NECTA ni wazembe sana mfano pia kuna kituo cha mtihan kina wahitimu 600 lakin hakuna hata C zinazozidi 15.
Hakuna uzembe wa kufanya wanafunzi zaidi ya 86% yaani Div 4 na ziro
 
Hata mimi napenda sana vijana wasiwe mitaani ni hatari sana, ila cha muhimu ni wao waje na SCIENTIFIC REASONS kwanini hali hii imejitokeza, kutokujua chanzo cha tatizo ni tatizo kubwa sana kuliko hata hilo tatizo lenyewe, hicho unachokisema kuhusu kushusha marks nahisi kimefanyika ila ndio hivyo tena bado hali ilikuwa mbaya wakaona hawana jinsi ni bora tu kutangaza kwanini huko chini wanaweza fanya hivyo washindwe kwa form 4, ila wasiwasi wangu wakifanya haya ya kushusha unaweza jikuta unaletewa wanafunzi sio tu kutokujua kuandika essay ila wasio jua kusoma kabisa kama tatizo hilo wanavyolalamika baadhi ya walimu wa sekondari, si unajua shule ni mwendelezo unapo mpitisha hapa ujue anakwenda ngazi nyingine

Mkuu hapo umenena.
 
Kama hawataki kutatua matatizo ya waalimu wetu nina hakika bora ya leo make waalimu wameapa tena ama zao ama serikali ..
 
Mkuu hebu acha ujinga na harakati za kipumbavu yani we unasema hadi kielweke na wakati haya ni maisha ya watu, siku nyingine usirudie huu utumbo wako.
kwani hao walimu si watu ni ngendere? Cha msingi si quantity bali quality mnapenda matokeo kuwa yanachakachuliwa la saba wamechakachuo wakafaulu wengi kundi kubwa hawajui kusoma wala kuandika faida gani iliyopatikana?kwa mtu mwenye ufikiri mkubwa anaweza refer back matokeo ya form 2 kwa hao waliorudia ingekuwa wamepitishwa tu kuendelea kidato cha nne nini kingetokea zaidi ya hiki?
 
Naunga mkono hoja. Kama ningekuwa napewa nafasi ya kupendekeza, kwa hakika hata mimi ningependekeza iwe hivyo, maana kwa hali hii, 2015, vyuo vikuu na VETA na vyuo vya diploma havitakuwa na wanafunzi. Kwahiyo ni bora tu kurudia mitihani. Wanafunzi watangaziwe ili warudi kwenye vituo vyao kwenda kufanya mtihani mwingine. Kuacha wanafunzi 250000 wapoteleee mtaaani hii si sawa kabisa. Lakini haya yalitakiwa yafanyike kabla ya kutoa matokeo. lilikuwa ni suala tu la kutangaza kwamba matokeo ni mabovu kwa hiyo mtihani unarudiwa.

Vipi walioshinda ?, nao wapewe hii option au wasipewe.., ?, by the way wapewe wenye zero tu au wapewe wenye 2, 3 na four as well, na wawe na choice ya kuchagua ya mwanzo au ya sasa ?, By the way wapewe muda wa kujiandaa au wasipewe ?, this is not an easy task
 
Kama kweli mitihani itarudiwa hii itakua kali kuliko zote,maana ilitakiwa irudiwe kabla ya kutangaza.
Binafsi siungi mkono kurudia maana mdogo wangu alikua anapiga sana book na kapata 1:17 ilala sec,hivi ninavyoandika hapa yuko brussels kwa mapumziko ya miezi 4 na atarejea hapa two weeks before join advance.

Kwahiyo kama kuna mpango huo ntaenda mahakamani kupinga marudio ya mtihani!
 
Sijui kama wakirudia watafanya vizuri bila kuwepo maadalizi mazuri na ya muda wa kutosha ya kuwaandaa/kuwafundisha.
Hawawezi kurudia na mtoa mada katunga tu hana Source
Kinachoweza kufanyika ni kuteua ile % inayotakiwa kwenda Vyuoni na Vyuo Vikuu na hapo hawatajali Madaraja huenda wakachukua hata Div III na wale wa Div IV wakaenda vyuo vya kawaida

Kurudiwa kufanya Mtihani kusikowezekanika
Kuna baadhi ya Watahiniwa hawakufanya kabisa Mitihani, wako walioandika mitusi wako waliokosa Ada wakafutiwa matokeo sasa wote hao utawapata wapi saa hizi kwani wapo waliokuwa wakilala Mabwenini nk
 
Mtoa mada kasema sorce ni habari leo uk-4.
 
Kutokana na ufahulu mbaya wa wanafunzi wa kidato cha 4 wa mwaka 2012, sasa mitihani hiyo kurudiwa upya na serkali itagharamia gharama zote na hii ni kwa ajili ya kuliepusha taifa aibu ambayo haijawahi tokea nchini kwa anguko la elimu.

Mods naomba msihamishe habari hii wala kunipiga ban, Mimi ni mjumbe tu na mjumbe siku zote hafi.
Mungu ibariki Tanzania.
Hiyo habari si yakweli walichokieleza kwenye hilo gazeti ni kuwa wanafikiria kuwa saidia kulipia ada ya mitihani na bado hawajaamua, fuata link hii,
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/9168-waliofeli-kusaidiwa
 
Hawawezi kurudia na mtoa mada katunga tu hana Source
Kinachoweza kufanyika ni kuteua ile % inayotakiwa kwenda Vyuoni na Vyuo Vikuu na hapo hawatajali Madaraja huenda wakachukua hata Div III na wale wa Div IV wakaenda vyuo vya kawaida

Kurudiwa kufanya Mtihani kusikowezekanika
Kuna baadhi ya Watahiniwa hawakufanya kabisa Mitihani, wako walioandika mitusi wako waliokosa Ada wakafutiwa matokeo sasa wote hao utawapata wapi saa hizi kwani wapo waliokuwa wakilala Mabwenini nk

Mkuu Ukwaju acha kuishi kwa hisia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom