HAYA MTOA MADA HII SI NDIO TAARIFA ILIYOPO KWENYE GAZETI LA HABARI LEO.UJIFUNZE KUSOMA HABARI VIZURI SIO UNAKURUPUKA TU.
SERIKALI imesema inaangalia utaratibu wa
watahiniwa 240,903 wa kidato cha nne waliopata
daraja sifuri katika matokeo yaliyotangazwa hivi
karibuni, kurudia mtihani mwaka huu kwa
gharama zake.
Aidha, imesema matokeo mabaya ya mwaka huu
yamesababishwa na mambo makuu manane,
kubwa likiwa ni wanafunzi waliopita bila kuchujwa
katika mtihani wa kidato cha pili walioufanya
miaka miwili iliyopita.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philipo Mulugo alisema hayo jana alipozungumza
na gazeti hili kuhusu hatua zitakazochukuliwa na
Serikali kutokana na idadi kubwa (asilimia 60.6)
ya watahiniwa wa kidato cha nne kufeli mtihani
wa Taifa kwa daraja sifuri na hatima yao ya
kujiuzulu.
Akifafanua, Mulugo alisema, suala la kujiuzulu
lipo nje ya mipaka yangu ya kazi kwa kuwa
halihusishi wizara moja wala Serikali pekee.
Lakini kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa
waliopata sifuri, Serikali inafikiria warudie
mtihani mwaka huu.
Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini
hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia
watahiniwa zaidi ya 240,000 waliopata alama
hiyo, kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za
Serikali. Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa
480,036.
Katika kuchambua hilo, tumeangalia namna ya
kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana
walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi, likipita hilo
la kurudia mtihani, Serikali italipia ada hiyo na
wataufanya kama watahiniwa binafsi, alibainisha
Mulugo.
Sababu za kufeli
Kuhusu matokeo mabaya, Mulugo alisema
sababu kubwa ni kutokuwapo mchujo kwa
watahiniwa waliopata chini ya asilimia 30 wakati
walipofanya mtihani wa kidato cha pili na hali
hiyo inaweza kujitokeza hata kwa watahiniwa wa
kidato cha nne mwaka huu.
Hawa ni waliofanya mtihani wakati mfumo wa
kuwachuja walipokuwa kidato cha pili ulikuwa
umeondolewa, walipita wote, iwe alipata F au A,
na walipita kwa miaka miwili, hivyo hata mwaka
huu athari zinaweza kutokea, ila watakaoingia
kidato cha nne mwakani, walichujwa na sifuri
zilikuwa zaidi ya 136,000, hivyo tofauti inaweza
kuwapo, alifafanua.
Hata hivyo, alisema matokeo hayo mabaya
hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza
idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu,
bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la
kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea.
Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la
nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28
wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.
Kujiuzulu?
Akielezea shinikizo la kuwataka yeye, Waziri Dk
Shukuru Kawambwa na Katibu Mkuu wa Baraza la
Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako
wajiuzulu, Mulugo alisema suala hilo liko nje ya
mipaka yake ya kazi kwa kuwa linahusisha Wizara
zaidi ya moja.
Si sahihi kulizungumza hilo la kujiuzulu, kwa
kuwa liko nje ya mipaka yangu ya kazi, si suala la
Wizara ya Elimu pekee, ni mtambuka na
linashughulikiwa na wizara zaidi ya moja, hata
hivyo hatua tayari zinachukuliwa kutafuta kwanza
kiini cha tatizo na mpaka sasa tumegundua
mambo manane.
Akiyataja, Mulugo alisema ni pamoja na jamii
kutosaidia wanafunzi kufikia malengo, wanafunzi
wenyewe, mitandao ya kijamii nje ya masuala ya
elimu, wazazi, Sayansi na Teknolojia na Serikali
katika mipango na sera, mwingiliano wa
uwajibikaji kitaasisi (wizara zaidi ya moja,
ikiwamo Tamisemi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Kuhusu madai ya mtihani mgumu uliokuwa na
mbinu za kitaalamu zaidi, Mulugo alisema hakuna
mtihani mwepesi duniani na kuongeza, kwamba
uwajibikaji wa wanafunzi katika elimu umefifia
kutokana na uhuru mkubwa walionao kupitia
mitandao ya jamii na vyombo vya habari, huku
akidai baadhi wanaiga kwa kasi mabaya
wanayoyaona humo na kuyahamishia katika
mitihani.
Utungaji
Pia alieleza namna mtihani unavyotungwa na
kubainisha, kuwa Necta huandika barua kwa Ofisa
Elimu wa Mkoa akiomba walimu makini walio
kazini, watunge maswali ya mwongozo wa mtihani
na maswali hayo hupelekwa katika Baraza na huko
walimu baadhi kuyapitia tena.
Baada ya hapo walimu angalau wawili au watatu
kutoka kila mkoa huweka kambi ya siku si chini
ya 10 kuhakiki na kupitia maswali hayo, kisha
Necta huunda kamati ndogo inayapitia miongoni
mwao maswali yanakuwa mtihani na si nje ya
hapo. Utaona anayetunga mtihani ni mwalimu
anayemfahamu mwanafunzi, alisema Mulugo.
Katika kusahihisha, kwa mujibu wa Mulugo,
walimu makini kutoka kila mkoa huchukuliwa kwa
uwakilishi na kupangiwa vituo vya kusahihisha
mtihani, na walimu wa somo moja hukaa kituo
kimoja tofauti na wa somo lingine na mwalimu
mmoja husahihisha swali moja na kumpa
mwenzake.
Haiwezekani kumpendelea mtu, unakuta mtihani
wa hesabu uko Kilimanjaro, Kiingereza uko Dar es
Salaam, labda wa Kiswahili unasahihishwa
Mbeya, sasa walimu wote wanakujua ama
wakupendelee au kukuonea?
Alisema na kusisitiza kuwa matokeo ya mwaka
huu yalitokana na udhibiti wa wizi wa mitihani
uliofanywa na Serikali na utaendelea miaka yote.
Aliitaka jamii kushirikiana kuwawezesha
wanafunzi kufikia malengo ya elimu kwa kudhibiti
katika matumizi ya simu, mitandao ya jamii na
wizi wa mitihani na kuongeza kuwa suala la elimu
linapaswa kuwa la wote, huku Serikali ikiwa ni
mtunga sera na msimamizi.
Yamekuwapo malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi wa kada mbalimbali kuhusu kufeli kwa
kiasi kikubwa wanafunzi waliomaliza kidato cha
nne mwaka jana.
Like 24 people like this. Be the first of your friends.
Imeandikwa tarehe 22 Februari 2013 By Gloria Tesha Imesomwa mara: 813
Tweet Tweet 1
Name * Email *
Type the code shown * Subscribe to
COMMENT COMMENT _ _ AND A